Nasikitika sana tena kuona viongozi wanongoza mpira club ya yanga ni mbumbumbu kabisa wa sheria zinazoongoza mpira wetu----Hivi kuna mtu hakuona alichokifanya Nadir Haroub kwa refa yule--kuna mtu hakuona utovu mkubwa wa nidhamu aliounyesha huyu kijana au hatuoni eti kwasababu anachezea yanga!!! kuna mtu hajui ni adhabu gani mchezaji anastahili akimsukuma refa, tuwe wakweli jamani vijana wetu wamekosa kabisa maadili ya mpira. Haruna alipewa kadi nyekundu lakini siku iliyofuata aliomba msamaha---ni kwasababu ni professional footballer. Wanayanga wanashindwa kujua kuwa violent contact adhabu yake ni 3 matches ban---hilo hawajui kabisa ndiyo maana wameshikilia jambo moja tu---Haroub hakumpiga mwamuzi--hakumpiga mwamuzi---hakumpiga mwamuzi lakini hawasemi alimsukuma mwamuzi, na reaction aliyonyesha baada ya kupewa yellow card kama si umahili na nguvu ya ziada angeenda kumdhulu yule mwamuzi.
Kulikuwa na akina Mwape, Kiiza, na Haruna Mwenyewe--je walimfanya mwamuzi---walikuwa watazamaji tu kwasababu waligundua kuwa ni kitendo cha aibu.
Naomba niseme wazi kuwa nilikuwa namheshimu sana tena sana Bwana Maulid Kitenge lakini leo ninapata wasiwasi na uwezo wake wa kuchambua na kusema ukweli juu ya football---anachokifanya ni kutaka kutuonyesha kuwa anapenda Yanga na siyo mpenzi wa football---tukio la kwanza kabisa lilinifanya niaenze kuuliza juu ya uwezo wake wa ku analyse mpira ni siku ile Tanzania wamecheza na Mozambique---alimpinga sana mwalim kutumia mshambuliaji mmoja lakini sikumsikia akitoa makosa mengi yaliyofanywa na mshambuliaji Bocco ambaye kama angetulia angefunga hata magoli manne--4 clear goals. hilo Kitenge hakuona kwasababu hata kabla alikuwa anatofuatiana na mwalimu.
Nakushauri Kitenge uige vijana wenzako kama akina Shaffi Dauda ambao analysis zao zimekuwa zakujenga na kuinua mpira wetu---acha kuongea kishabiki--hutusaidii---kama tunataka kujenga mpira wa kushindana tuache ushabiki.
Tuache TFF ifanye kazi yake bila kuingiliwa na watu wasiojua sheria za mpira.
Simba enzi za akina Dalali walipoteza points Sita



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. napenda kushukuru kwa comment za hiyo makala,lakini mwandishi hakufuatilia kiundani ni nini tatizo katika hili sakata,mpira haukumiwi kupitia vyombo vya habari wal comment za shafii dauda,cannavaro amechezeshwa mechi na coast kwa sababu ripoti ya mwamuzi imemruhusu acheze..kwani mchezaji anapopewa kadi njekundu na hakausika kwenye fujo basi kwenye ripoti ya kamisaa wa mchezo lazima ionyeshe hivyo
    swali..aliyeandika makala hii alifuatilia ripoti ya kamisaa wa mchezo?
    mpira sio siasa ya ktumia vyombo vya habari kutimiza matwaka ya kina fulani.

    ReplyDelete
  2. Mdau mbona unazungu tu huna point...je Nadiri alimpiga refa au? hiyo video clip uliyoweka haionyeshi kuwa Nadiri alimpiga refa, bali mchezaji mwingine. Mimi nadhani argument yako ni very weak...sababu huna supportive argument yeyote kuwa huyo mchezaji unayesema...hiyo clip haionyeshi kuwa kampiga refa, bali wenzake wana mzuia asimfikie refa....

    Sisi wengine tunafuatilia soccer la nyumbani kwenye blog and magazeti, naona ndio sababu timu yetu ya Taifa haifiki mbali...

    ReplyDelete
  3. Mkuu uliyetoa hoja weka ushabiki pembeni,kwanza cannavaro hakupewa kadi ya njano,pili hakumsukuma refa,kama amehukumiwa kwa kitendo ambacho hatujui alikuwa anataka kufanya nn sawa,alafu ukweli unabaki palepale refa mamlaka yake ni red card baada ya mechi report inapelekwa kamati ya ligi na huko ndio wanaweza angalia adhabu stahili japo kuwa hawana mamlaka,je utajisikiaje kesho ukisikia yanga wameshinda rufaa yao,jiulize why mwenyekiti wa azzam aliyetangaza kujiudhuru alirudi ghafla kuendesha kikao bila kutangaza uamuzi wa kusitisha kujiudhuru,lipi alilofanya shaffih katika maendeleo ya soka la bongo?

    ReplyDelete
  4. Anon wote wa hapo juu ninyi ndiyo mnaua nidhamu katika soka. Kwa kweli refa lazima alindwe kama Naddir kampiga au mchezaji mwingine ni dhahiri hiyo haijalishi. Kwanza ilitakiwa wachezaji wote waliomzonga refa kwa kumsukuma kupata adhabu sawa na aliyempiga refa.

    Ndiyo maana hatuna mchezaji hata mmoja anayecheza katika ligi za dunia ya kwanza. Tena katika nchi nyingine ilitakiwa wanapigwa ban ya kucheza mpira kabisa wakacheze mpira wa mchangani. Mpira ni burudani si vita, unapocheza lazima uwe na nidhamu kama unaona unaonewa unapeleka malalamiko kunako husika.

    Big up mwandishi wa makala hii.

    ReplyDelete
  5. Ngumi yenyewe ya ki uchovu uchovu, you can see the man is not a natural fighter, ile ngumi koko una iblock na kumdunda knock out punch easily, lakini refa alikuwa mstaarabu, kumpiga au lumbugudhi refa mambo ya kizamani hayo, kwa wakazi wa Chang`ombe/keko enzi na magutu na mbwa mwitu- Avenja.

    ReplyDelete
  6. Aibu Tupu. Tanzania ovyooo. Hamna nidhamu

    ReplyDelete
  7. Nyie wote wehu, mpira si ngumi, inabidi wachezaji waliohusika wafungiwe maisha. Ndio maana hatufiki popote kwa akili mbovu ka hizi.

    ReplyDelete
  8. Refa kabamizwa, Yanga hawataki nyodo zisizo na msingi. Aluta Kontinyua!

    ReplyDelete
  9. Wadau, hoja ni kwamba canavaro alipewa kadi nyekundu na mwamuzi aliandika ktk ripoti kwamba ni kosa la kupigana, hata kama mwamuzi alikosea hakuna kamati iliyokaa na kusema canavaro hana kosa kwa hiyo alitakiwa atumikie adhabu ya kukosa mechi tatu kwa mujibu wa ripoti ya mwamuzi hata kama alikosea. Na kamati ya Tibaigana iliweka wazi kwamba haiingilii maamuzi ya mwamuzi. Hiyo ndio sheria ya mpira, mambo mengine yote ni kuleta siasa na ushabiki ktk mpira.

    ReplyDelete
  10. mi nina swali kwa hao waungwana hapo juu waliodai kwamba cannavaro hana kosa?swali red card aliyopewa anastahiki kutocheza mechi ngapi?na ile ya coastal ilikuwa mechi yake ya ngapi ?

    ReplyDelete
  11. Habari Ankal!

    Kuna vitu ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya soka nchi hii, kuna viandishi uchwara ambavyo havina ethics za uandishi wa habari, ukijaribu kuangalia clip ya makosa yanayosadikikia kufanywa na wachezaji wa Yanga utagundua kwamba Nadir Haroub hakumpiga refa wa mchezo husika, aliyempiga refa alikuwa ni stefano mwasika hilo halina ubishi, lakini baada ya mwamuzi wa kati kuongea na mwamuzi msaidizi na nadhani ni misunderstanding/misinformation yeye mwamuzi wa kati akaamua kumpa kadi nyekundu 'straigh red card' kwa Nadir Haroub 'canavaro'. Lakini uthibitisho wa clip unaonyesha kabisa kuwa Canavaro hakumpiga mwamuzi ila baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ambayo kwake anaiona siyo halali ndipo alipo react intentionally kutaka kumpiga mwamuzi, swali la kujiuliza je tulifanya uchunguzi na kugundua tatizo la mwamuzi huyu pia, na si kufungia wachezaji tu, Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ni Mwenyekiti wa Klabu ya Azam F.C. nadhani hapa kuna conflict of interest, na pia tusiwe washabiki wa ukosefu wa adabu mchezoni kama walivyofanya wachezaji wa Yanga, lakini pia kunahitajika kufanyike uchunguzi wa hali ya juu wa busara na hekima za waamuzi wetu kwani inaonekana kuna mushkeli katika maamuzi mengi ya kiwanjani, ukiangalia ile clip utagundua kuwa yule mwamuzi alikuwa na ajenda ya siri, kumtoa Haruna Niyonzima na Nadir Haroub ndicho kilikuwa kipaumbele cha kuumaliza ule mchezo, Said Mohammed - Mwenyekiti wa Azam F. C. anajua karata zao wanazicheza vipi! tutafika!!!!

    Mashaka, H. A.
    shark_ham@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  12. naungana na wadau mliomkosoa mtoa mada, ameonesha unazi zaidi badala ya kuchambua pointi, huna tofauti na Nyange Kaburu ambaye anakurupuka kutoa maamuzi ya kuionea yanga ili kuifavor timu yake simba hilo ndio tatizo, soma ripoti ya kamisaa, na maamuzi ya kamati ya nidhamu badala ya kukurupuka mmeanza kuweweseka kwa kutokuwa na uhakika wa kupata ubingwa chezeni mpira badala ya kusubiri ushindi wa mezani

    ReplyDelete
  13. Na Mafisango alipomsukuma refa mechi ya Simba na Orijoro JKT naye afungiwe na Simba Kunyanganywa point?

    ReplyDelete
  14. Kwani huo ulikuwa mpira wa miguu 'football match', au masumbwi 'boxing'? Nimeangalia hizi 'clips' lakini sijapata JIBU.

    ReplyDelete
  15. Media zinachangia kwa kiasi kikubwa sana maendeleo ya soka ndani ya nchi,sasa wewe ukisema hajaona mchango wa akina shafii dauda ktk soka bovu la nchi yetu ntakushangaa sana na nakukuona haujui na haufuatilii kabisa mambo ya mpira!Swali kwako kama si media kuwepo wale wakijijini wangepata vp taarifa za michezo?Tusicomment vitu kiushabiki tunatakiwa kuangalia kweli uko wapi,kama alizuiwa na wenzake lengo lake lilikuwa ni nini na asingezuiliwa nini kingetokea?Haroub adhabu anastaili tena 100% ili wengine wajifunze,mpira ni mpira na ngumi ni ngumi na ndio maana kuna vyama vinavyohusika na hizo categories!

    ReplyDelete
  16. Hivi muandishi wa hii tamthilia ana bifu na Maulid Kitenge au? Anapatkana ITV/Radio One, humu si mwake acha umbea.
    Enhe..Yanga iletewe usharouharo halafu itulie,chapa hao waamuzi vimeo siku nyingine wafanye kazi yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...