Mara kadhaa sasa nimekuwa nikiliona tukio hili la magari kupita kwenye taa hizi zilizopo kwenye makutano ya Barabara ya Kawawa na Kinondoni Manyanya Jijini Dar bila ya utaratibu maalumu uliopo kwa taa hizi kama tunavyotakiwa kufuata.ambapo ikitokea umesimama kwa kufuata sheria za usalama barabarani kufuatana na kuwaka kwa taa nyekundu halafu nyuma yako kuna gari nyingine,utasikia unapigiwa honi kana kwamba umesimama kimakosa au wakati mwingine unaona gari iliyo nyuma yako inakupota na kuondoka zake kana kwamba hazioni taa hizi.sasa leo uzalendo umenishinda na kuamua kulileta kwenu wadau ili tufahamishane zaidi,hivi ni kwamba hizi taa hazionekani au inakuwaje??
Home
Unlabelled
HIVI NI KWAMBA TAA HIZI ZA KUONGOZEA MAGARI HAZIONEKANI??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
kaka / dada unapigia mbuzi "guitar". madereva wengi wa bongo hawajui maana ya matumizi ya taa za barabarani. kwa wachache wakiona nyekundu wanakubali kusimama coz kuna askari kwa mbele au basi tu magari ya upande ulioruhusiwa yameshaanza safari. lakini hakuna gari hata iwake nyekundu kali kiasi gani ndio kwanza wanapitiliza... hasa madaladala.... pole..... na hizo taa za kinondoni ndio mbaya zaidi.. kuwa makini usidhani madereva wote wana busara kama wewe....
ReplyDeleteHata Mimi. yamenikuta, mume wangu alisimama daladala nyuma ikapiga honi akakidai hasijii, mbona daladala alisogeza gari hadi kugonga gari la mume wangukwa nyuma, hapo. wakafikishana Oysterbay police kuandikishana, yskaishia hapo. mzee. wangu alichoka kufuatilia. _
ReplyDeleteAsante mdau..Hata mimi imeshanitokea sana hii.Bora hata hiyo..kuna barabara zingine Mfano pale sijui Maktaba,kama unatoka Akiba unaingia Posta(Barabara ya Bibi Titi,Sofia House)..Zikiruhusiwa gari za kwenda posta tu,wewe unayeelekea Mwenge unastahili kusimama hata kama hakuna barabara inayokatisha Mbele yako kwenda upande Mwingine.Utasikia honi kibao nyuma eti kwa sababu hakuna gari zinazovuka kwenda upande mwingine(Kuingia Maktaba)
ReplyDeleteKwa nini huruhusiwi kupita hata kama hakuna barabara ya Magari inayokatisha upande mwingine??Kwa sababu wakati gari zinazoingia Posta zimeruhusiwa kunakuwa na Watembea kwa miguu wanaotakiwa kuvuka barabara zote mbili za Bibi TITI na hapa ndipo madereva wengi wanasahau au wanafanya makusudi.Binafsi nilikuwa sielewi hadi nilipodakwa siku moja na Askari wa barabarani na kunieleza.Nilikubaliana naye hapo hapo na kumshukuru.
David V
Hii ndio kinondoni Kiria kwa manyanya huu ni mwaka wa 7 hizo taa twazijulia ikiwaka taa nyekundu ya chini wee ndo kata uelekee town upo? au wapo wahusika........
ReplyDeletewatanzania tuna tatizo la kutojali taratibu au sheria zinazopaswa kutii bila shuruti hasa kwa vile hata leseni zenyewe zinapatikana bila kufuata taratibu na ukipatwa na kosa unaweza kuhonga kwa vyombo husika na kuendelea na shughuli zako.
ReplyDeleteDalili tosha kuwa nini kilichomo ndani ya vichwa vya watanzania....haya ndio maalezi toka chama tawala kwa miaka 50.......sidhani hata tukiwabadili waondoke madarakani tutabadili chochote katika kufikiri kwa mtanzania......taratibu tunaelekea Nigeria....ambako hata ubadili mfumo wa uongozi nchi imeeisha kaa tenge....MUNGU ISAIDIE NCHI YANGU.....
ReplyDeletemimi naona siyo tatizo la DEREVA,tatizo ni mamlaka zinazosimamia sheria zimelala halafu serikali inasema haina pesa wakati mitaji kama hii iko wazi wazi.mamlaka imeoza,hakuna anayejali,wako kusimamia siasa badala ya sheria.vipi kama hivi kwa nchi za wenzetu unaogopa kufanya kwa sababu unaogopa faini na kuimamishwa leseni.
ReplyDeleteKawawa na kinondoni hapo. Huwa hazionekani kabisa! katika taa ambazo madereva hawazifuati hizo ni moja wapo.
ReplyDeleteNashukuru kwamba wapo watu wanaojali kama wewe. Inafaa yeyote asiyefuata utaratibu huu wa taa atozwe malipo ya adhabu bila hiari. Shida kubwa ni kwamba askari wetu hawangojei sehemu kama hiyo. Tatizo kama hilo lipo pia makutano ya bara bara ya Chuo Kikuu na Sam Nujoma, karibu ya Ubungo.
ReplyDeleteHuko nje ya Tanzania, askari hungojea watu wasioheshimu taa sehemu kama hizo. Mara anapotokea mhalifu, hakuna hadithi bali adhabu ya kutotii taa. Kazi kwenu askari.
yale yale, uharaka na uzembewa madereva wa bongo, taa zinaonekana vizuri kabisa, mi nishakoswakoswa hapo napaogopa kama ukoma!
ReplyDeleteBongoland, nikirudi sijui kama ntaweza endesha gari though nimeendesha gari Dar tangia na miaka 15, na nimeendesha for 5yrs,nikaondoka. nw nipo nchi ya watu kwa obama, nimeshia zoea kufata sheria miaka 4now...nawasiwasi nikirudi bongo nitagongwa sana na madereva wazembe ambao hawafati sheria za barabarani. huku fanya hivyo utaona tu camera ina flash and unatumia faini yako ktk mail...ukifanya ndo tabia unafungiwa leseni na u cnt drive without a licence utaenda jela
ReplyDeleteTanzania nchi yangu miaka 50 ya uhuru bila utawala wa sheria.Sheria zipo ila hakuna enforcement ya KUWAJIBIKA, ila sheria zipo za rushwa.
ReplyDeleteNenda pia kona ya Shekilango na Morogoro rodi taa za kuelekea Ubungo. Kweli ya mambo ya bongo ni upepo tu; "YOTE YATAPITA NA MAISHA KUENDELEA"
ReplyDeleteMimi nafikiri zile za maktaba ziliwekwa muda mrefu, na kama ni kurekebishwa basi nazo zinahusika. Kwa sababu zenyewe hazitofautiani sana na zile za mbele yake (BP/Serena - zamani Movenpick), kwa sababu nazo zikiruhusu za kwenda Ohio, basi wale wa moja kwa moja nao wanapita ingawa upande wa kwao zitakuwa nyekundu. Jaribu kuangalia hata akiwepo askari kuongoza magari, naye ataruhusu za kuingia posta mpya/Ohio, kwa pamoja na zile za moja kwa moja - yaani kuelekea taa za BP/Serena na Mwenge.
ReplyDeleteIla kwa hizo za Kinondoni, kwa kweli ni madereva wachache sana wanaona nyekundu, wakati mwingi naona inaonekana ni kijani tu, which kweli ni hatari.
Sasa nyie woote mliocomment kumbe ndio hamjui vizuri sheria za barabarani,hususan hizo taa.Nitawaelimisha.Hapa dar set up ya taa ipo katika scenarios mbili;kwanza ni pale kwenye set up kama ya msalaba,yaani,kuna njia nne zinakutana(mfano tazara,mwenge,ubungo,st peters(tofautisha na namanga),akina nk,nk)Hizi utekelezaji wake uko straight maana ikiwaka nyekundu,ujue upande mwingine imeruhusu,hata gari isipokuja,bado inabidi usubiri maana taa si zako.Hii ni rahisi.Scenario ya pili ni taa ambazo zipo kwenye njia tatu .mfano hapo junction ya Ohio,junction ya maktaba,Palm beach, Namanga nk.Mfumo wa taa hizi unatambua njia tatu tuu rasmi.ndio maana hapo junction ya bibi titi na Ohio hakuna hakuna taa inayoongoza magari yanayotoka hapo BP kituo cha mafuta,au pale palm Beach hakuna kabisa njia rasmi upande ule wa kushoto (ukitizama kaskazini.msingi hapa ni kwamba katika taa hizi zinazotambua njia kuu tatu,hakuna kabisa lay out ya ule upande ambao hauna barbara rasmi.Sasa hii ina impact gani?nichukue mfano wa pale namanga ukitokea mjini.Taa ya kijani ya mshale inapowaka ili kuruhusu wale waendao namanga kukunja kuelekea huko,wewe unayeenda Moroco inabidi unyooke,hata kama taa ni nyekundu,maana hakuna logic ya kusimama,kwani mfumo wa taa hauna layout ya mtu anayetoka moroco kukunja pale namnanga ili sijui aende wapi! kwa hiyo kutakuwa hakuna collision kwa mtu anayetoka mjini akipita muda huo. kwa mfumo huu wa taaa za kwenye junction ya njia tatu,ni sahihi kupita kwenye taa nyekundu kwa mazingira hayo niliyoyataja.Ila sasa watu wanakosea sana pale mataa ya st. peters.Wanadhani pale kuna mfumo wa njia tatu,kumbe sio.Pale kuna njia rasmi nne!Mlimani city pale njia ya kwenda sinza makaburini pale ni mfumo wa njia nne,japo ile njia ya nne imeelekezwa porini kwa makusudi maalum(kuna plan ya majengo kule porini siku za usoni).Nadhani hint hii niliyowapa itakusaidieni kuchambua zaidi ukweli huu.Asante kwa kuelewa.
ReplyDeleteWewe anony wa 3.26 ndio yaleyale niunayosema, imehusu nini serikali. Hivi Mama ako nyumbani amekulea kwa heshima, ni lazima akufuate kila mahala ili ajue kuwa unatekeleza malezi yake. Serikali gani inasimamia roho za watu barabarani, ni akili za vijana wa siku hizi wasiotaka au kutokujua kufuata sheria. Hiyo serikali yako itakayoingia ikaanza kusimama barabara kuhakikisha hupigi honi nyuma ya gari la mwenzio wakati taa imewaka nyekundu itakuwa kama Mama wa kambo viboko kama hujakosha vyombo vizuri.
ReplyDelete