![]() |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI |
Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa ni kauli yake ya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai kwa jazba sana kuwa hukumu ya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.
Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala Ikulu imeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu ama kuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.
Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa hukumu ama kuelekeza namna ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala mamlaka hayo.
Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa Mahakama ambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili mwingine katika maamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazima atambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu.
Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya, kwamba Bwana Lema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni la kisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo mahakamani.
Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu mwingine wa kumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo, ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu. Tunaomba wananchi wampuuze. Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hana mtu wa kumlaumu bali ajilaumu mwenyewe.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012
bw mkurugenzi Ikulu wala usingepoteza muda kumjibu huyu.. mngemwacha tu abwabwaje tufungue kesi mpya..si yeye bingwa wa matusi?? ajaribu tena aone kilichomng'a kanga manyoya..hii nchi ya utawala wa sheria bana!
ReplyDeleteLakini, kusema ukweli bila upendeleo, kampeni za siasa za Tanzania huwa ni za matusi na kejeli, basi useme tu huyu kimemwangukia vibaya, mimi ni mwanasiasa vilevile, na nimeshuhudia vyama vya upinzani vinakejeli na kutukana chama tawala, pia c.c.m. haijakaa chini nayo inatukana na kukejeli wapinzani tena kwa namana ya pekee kabisa, kama unataka ushahidi nina tape kadhaa za kampeni za siasa za tanzania, kwahiyo hakuna aliye safi hapa wote mambo ni hayo hayo. ilakusema eti huyu hakimu amehukumu "under influence" hiyo sina hakika, ingawa nakili kuwa uwezekano upo tena mkubwa tu kwamba mheshimiwa Jaji anaweza kuwa ameshawishiwa kutoa hukumu ya namna hii, inaweza kuwa siyo na Mh. Rais au anayefanana naye, lakini ikawa ni C.C.M, Kwakuwa wanakitaka kiti kile siyo siri.
ReplyDeleteMwisho napenda kusema kwamba C.C.M Hawawezi kupata kiti kile, kwasababu "wame-mess-up" sana katika jimbo lile, hata kama siyo Mr. Godbless Lema atapatikana mwingine wa upinzani, anayepinga anyooshe kidole.
Malalamiko ya Godbless Lema hayana kichwa wala miguu:
ReplyDeleteHakuna sababu yeyote Raisi kuhangaika na Jimbo la Arusha Mjini wakati ,Mhe. Raisi anatawala nchi nzima ikiwemo hiyo hiyo Arusha Mjini.
inonyesha Lema na wenziwe wakiingia ikuklu wataamrisha polisi nani akamatwe (bila kosa), nani ashindwe mahakamani (bila haki), nani afanyiwe opresheni hospitali (hata kama haumwi) nani auliwe kwa kunyongwa (hata kama hana kosa) nani afukuzwe nchi, nani atiwe kizuwizini, n.k., kwa sababu wanaamini RAISI ANA NGUVU NA HAKI YA KUFANYA CHOCHOTE, WAMEKOSEA.
ReplyDeletechungeni saana hawa CDM na wapinzani.
kauli zao na mienendo yao inaonyesha si wasomi, ni form 6, ukiacha zitto.
hawa CDM hawako makini kwa kauli hiyo, kwani hawakuangalia inawaumiza kiasi gani kwanza. Kama yale ya Igunga ya mtandao wa DC.
Kamwe JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA haiwezi ruhusu kutawaliwa na 'Genge' lenye Msimamo na mwenendo uliojaa ,JAZBA,GHADHABU,CHUKI,DHARAU, MAKUNDI, PUPA NA KUTOFUATA TARATIBU!
ReplyDeleteMWIZI AU KICHAA HAKABIDHIWI RUNGU!
Hawa jamaa hatuwezi kuwapa IKULU !
ni pre-planned,nahudhuria the same case ya uchaguzi singida,Tundu lissu pia hali yake mbaya, he gona drop out believe me,nchi haiendelei ina litigation za kung'oa ubunge kila siku
ReplyDeleteHii ianatuonyesha kwa kiasi gani Mr.Godbless Lema amekosa hekima na busara,kama hakuridhika na maamuzi ya mahakama akate rufaa,kauli zake za hovyo hovyo ndo zimemfanya kuvululiwa ubunge.open your mind mr.lema.
ReplyDeletebila jazba ubunge hupati!!!!tutajuaje uko serious? hahahaha!!
ReplyDeleteJamani mnashangaa kitu gani kwa aliyekuwa mheshimiwa kutamka hivyo? toka awali ameonyesha kuwa busara kwake ni haba na wakati wa mwenendo wa kesi tuliona jinsi shule yake ilivyotia shaka. tukifuatilia kwa sana unaweza kukuta shule yake kachakachua.
ReplyDeleteYaani leo ndio mnamjua Lema? It was just a matter of time before his true colours come our, hata hivyo hazijajionyesha zote... he is not a leader material... twalijua hilo ingawa sio mwanasiasa mie. huwezi kumweka level moja na Mnyika, Zitto, January etc..
ReplyDeleteIkulu..mngejinyamazia tu mkaendelea na shughuli zenu za maana zaidi... msibishane na....
ReplyDeleteaaaaaaaaaaache ujinga mr lema ,chadema kwa huyu jamaaa anawapotezea sana,toa kwenye chama
ReplyDelete