JINA LA KITABU: MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA: TULIKOTOKA, TULIPO NA TUNAKOKWENDA
 
MWANDISHI: JOHN MTWALE KASEMBO
Ni mzaliwa wa Mkoa wa Mwanza. Ni mwezeshaji na mtoa mada wa mambo ya uongozi, dini, vijana, falsafa, ujasiriamali na amali za maisha. Ni mhitimu wa masomo ya falsafa na dini katika Chuo cha Mtakatifu Augustino Peramiho ambacho ni Chuo Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Urbaniana, Roma. Tena yeye ni mtafiti wa maendeleo ya Tanzania.

Yaliyomo
Kutabaruku................................................................................................. 7
Shukrani..................................................................................................... 11
Dibaji.......................................................................................................... 15
Utangulizi................................................................................................... 17
Vifupisho................................................................................................... 23
Sehemu ya Kwanza
TANZANIA TULIKOTOKA
1. UKOLONI TANZANIA BARA........................................................... 27
2. HARAKATI ZA UKOMBOZI............................................................. 39
3. UHURU................................................................................................ 47
4. MAISHA BAADA YA UHURU......................................................... 57
Sehemu ya Pili
TANZANIA TULIPO
5. JUBILEI YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA....... 69
6. JUBILEI NI KUANGALIA TUNU ZETU KAMA WATANZANIA. 78
7. JUBILEI NA CHANGAMOTO ZETU................................................ 86
Sehemu ya Tatu
TANZANIA TUNAKOKWENDA
8. JUBILEI NI KUANZA UPYA............................................................. 107
9. KANUNI YA TIBA MCHEPUO KWA MAENDELEO
YA TAIFA LETU..................................................................................... 133
TATHMINI NA MOTISHA..................................................................... 145
HITIMISHO.............................................................................................. 159
REJEA....................................................................................................... 169

MUHTASARI:
Ndugu Watanzania wenzangu, nimendika kitabu hiki kwa malengo matatu. Kwanza kitabu hiki kinalenga kupanua mawazo na mtazamo wetu Watanzania kuhusu dhana ya Jubilei ambayo sisi tunafanya kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru wetu yaani kujua kuwa nini tunatakiwa tufanye. Uelewa huu utakuwa wa msingi kwa kizazi kitakachofanya Jubilei ya miaka 75 au miaka 100 ijayo ya taifa letu. Tena, lengo la pili la kuandika kitabu hiki ni kutoa uelewa ambao utakuwa ni chagizo la mabadiliko, ukombozi na maendeleo kwa watu tulioamua kutafakari na kutenda kadiri ya ukweli kwa manufaa ya taifa letu katika kizazi hiki na kijacho wakati huu tunapofanya Jubilei ya miaka 50 ya uhuru wetu. Na zaidi, lengo langu la mwisho la kuandika kitabu hiki ni kuchukua wajibu kama Mtanzania wa kushirikisha mawazo yangu kwa  Watanzania wenzangu ili kuyatafuta maendeleo ya kweli ya taifa letu na zaidi sana ni kutoa mchango wangu katika sherehe hizi za taifa letu.

Kitabu hiki kimegawanyika katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza ni Tanzania - tulikotoka ambayo inaongelea masuala ya ukoloni, harakati za ukombozi, uhuru na maisha baada ya uhuru. Sehemu ya pili inaongelea Tanzania – tulipo inayozungumzia hali yetu leo kiuchumi, kisiasa na kijamii nikijadili changamoto zetu kama taifa na tunu zetu tulizonazo tangu uhuru mpaka sasa kama Watanzania na maana na umuhimu wa sherehe zetu za Jubilei ya miaka 50. Hatimaye, sehemu ya tatu, inazungumzia Tanzania – tunakokwenda (mwanzo mpya) ikijadili wapi tunakokwenda kama taifa yaani kuwa na mwanzo mpya na kuingalia kanuni ya tiba mchepuo kama nyenzo ya kutufikisha huko.  Kama yule mshairi na mtunzi wa vitabu wa Uingereza Robert Louis Stevenson alivyopata kusema kwamba, “Usipime siku yako kwa yale uliyovuna bali pima kwa yale uliyopanda.” Malengo hayo ndiyo yamenifanya nipande mbegu ya kitabu hiki kwa kuitakia mema nchi yangu kwa miaka 50 mingine.

Mwisho natabaruku kitabu hiki ni kwa heshima ya taifa langu Tanzania linalofanya Jubilei ya miaka 50 ya uhuru wake na kwa namna ya pekee Mama yangu mpendwa Christina Shija, baba yangu mpendwa marehemu Gabriel Kasembo, marehemu babu yangu Chifu Yohana Kilangabhana Kasembo, marehemu bibi yangu Agatha Mija Michael, Hayati Askofu Mkuu Anthony Mayala, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Watanzania wote ninaochangia nao utaifa na nia njema ya kuitakia mema nchi yetu.
 KWA KUAGIZA NAKALA YA KITABU HIKI KIZURI WASILIANA NA:
JOHN MTWALE KASEMBO
P.O BOX 22, PERAMIHO.
SIMU: 0755 417 074 / 0712 120 775
BARUA PEPE: jmkasembo@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MIAKA 50 YA UHURU:

    Tulipotoka katika kitabu chako umeeleza vizuri sana , tulipo ndio hasa umepatia ila tunapokwenda mkae mkijua kama MSIPOJIREKEBISHA CHAMA TAWALA MTAANGUKA NA KUZAMA KABURINI KABISAAAA !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...