MAREHEMU SELEMAN ANDREA NKINGWA
1954 - 27/4/2011
LEO UMETIMIZA MWAKA MMOJA TOKA ULIPOTUAGA UNAKWENDA KIKAZI NZEGA HALAFU UKARUDI UKIWA KWENYE JENEZA. HATUNA CHA KUSEMA ILA TUMEBAKI KUMSHUKURU MUNGU TUU KWANI AMEPENDEZEWA NAWE ZAIDI YETU.
BABA, TUNAKUKUMBUKA KWA MENGI LAKINI KUBWA KULIKO YOTE NI JINSI ULIVYOPIGANIA ELIMU YETU AMBAYO IMETUFIKISHA HAPA TULIPO.PIA ULIAMINI KUWA BILA SALA NA UPENDO WA MUNGU, HATUWEZI KUFIKA POPOTE. TUPO KAMA ULIVYOTUACHA. TUNAENDELEA KUKUENZI KWA HAYO INGAWAJE BADO MAJARIBU NI MENGI.
UNAKUMBUKWA SANA NA MKEO MPENZI SUBYEKI, WANAO RACHEL, RAPHAEL, RAYMOND,RENATHA, RICHARD, NA RAINFRED, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.
TUTAKOSA FADHILA PIA KAMA HATUTAKUMBUKA VIKUNDI VIFUATAVYO AMBAVYO VILITUSAIDIA SANA WAKATI WA MSIBA WAKO:
WANAPAROKIA YA MT. JOSEPH MUKASA – NYAKATO, HASA JUMUIA YA MT. PAULO KWA HUDUMA ZOTE ZA KIROHO UONGOZI NA WAFANYAKAZI WA BENKI KUU TAWI LA MWANZA KWA USHIRIKI WAO UONGOZI WA KAMPUNI YA CASTIAN KWA MSAADA WAO WA HALI NA MALI KIKUNDI CHA KINAMAMA CHA TUMAINI NYAKATO MAJIRANI NA NDUGU HASA SHEMEJI YANGU METUSELA ANDREA NKINGA NA MAGDALENA DIALLO.
MISA YA KUMUOMBEA ITAFANYIKA JUMAPILI YA TAREHE 29/4/2012 HUKO NYAKATO,KARIBUNI SANA.
RAHA YA MILELE UMPE EEE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE,APUMZIKE KWA AMANI
-AMINA!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...