Baba Mtakatifu Papa John Paul II akiwapungia maelfu ya Watanzania waliofurika katika viwanja vya Jwangani jijini Dar es salaam alikoendesha misa maalum ya ziara yake hiyo Oktoba 1990
Baba Mtakatifu Papa John Paul II akimlisha mkate Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
Baba Mtakatifu Papa John Paul II akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba
Baba Mtakatifu Papa John Paul II akiwasili Jangwani
Baba Mtakatifu Papa John Paul II na ujumbe wake wa Vatican katika mazungumzo rasmi na serikali ya Tanzania chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi
Baba Mtakatifu Papa John Paul II akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
Rais Ali Hassan Mwinyi akimsindikiza Baba Mtakatifu Papa John Paul II baada ya kuhutubia Jangwani
Baba Mtakatifu Papa John Paul II akimpa zawadi Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania Mhashama Kardinali Rugambwa
Baba Mtakatifu Papa John Paul II na mwenyeji wake
Mhashama Kardinali Rugambwa.
--------------
KUTOKANA NA MAOMBI YA WENGI, SIKU ZA JUMAPILI GLOBU YA JAMII ITAKUWA IKIKULETEA MATUKIO MBALIMBALI YA KIHISTORIA YA NCHI YETU KUTOKA MAKTABA ZETU KAMA HIVI.
MDAU MWENYE AINA YOYOTE YA TASWIRA ZA KUMBUKUMBU
ANAZOTAKA KUSHEA NA WADAU USISITE KUTUTUMIA KUPITIA
ANAZOTAKA KUSHEA NA WADAU USISITE KUTUTUMIA KUPITIA
issamichuzi@gmail.com
picha hizi zinatukumbusha watanzania tulikotoka. Tulikuwa na uvumilivu wa imani zetu kwa kiwango cha juu sana. Kitu ambacho kimepungua sana siku hizi. Angalia Raisi Mwinyi na imani yake tofauti how he was so happy with this Pope..kwa kweli..ni vema tukauendeleza huu utamaduni wa kupendana na kuvumiliana.Tuache ubinafsi na kudharau imani za wenzetu. We can make our demands and claims without demonizing each other.
ReplyDeleteLoh...kumbukumbu nzuri sana..inahuzunisha sehemu fulani fulani lakini ndiyo hali halisi..
ReplyDeleteDavid V
Asante sana Michuzi. Niko interested na ubadilikaji wa utamaduni wa mavazi hasa katika tasnia ya siasa. Nilikuwa nikijiuliza bila jibu ni lini suti ya kwa Mama Malkia ilirejea lini kama vazi rasmi la dola. Hii ni data nzuri kabisa kwamba hadi mwaka 1990 katika hafla rasmi kama hii rais alikuwa bado anavaa suti ya kaunda.
ReplyDeleteHello Mdau michuzi,
ReplyDeleteAsante sana kwa ukumbusho huu mzuri sana, na Pongezi kwa wazo zuri.Keep it up ,We depend on you!
Maelfu walitoka mbali kwenda Jangwani kumwona na kumsika Pope. Hata waislamu walijazana Jangwani kupata baraka ya Pope! Kumbukumbu nzuri sana! Asante Michuzi!
ReplyDeletesafi sana umetukumbusha mbali endelea na moyo huohuo michuzi juuuuuu
ReplyDeleteMichuzi Asante sana kwa ukumbusho huu mzuri na muhimu.
ReplyDeleteBabu kubwa kaka issa.nilikuwa sijaona ziara baba mtakatifu john paulo wakati yupo bongo.asante sana
ReplyDeleteMdau hongera kwa kutuletea kumbukumbu hizi muhimu
ReplyDeletejamani ici yule kwenye picha ya Tano kulia mwanzoni sio spika bunge wetu mama Annie Makinda,naomba jibu wadau wenye data kamili.
ReplyDeleteMdau-Mtafiti wa mambo.
Aliyeleta utamaduni wa suti ya malkia katika ofisi za serikali alikuwa Mkapa baada ya kuchukua nchi 1995. Alianza kuvaa suti ofisini na maafisa wengine wote wakaanza kuvaa suti.
ReplyDeleteNguo zote za malkia, muafirka lake lubega, inayobadilika ni mitindindo, hata sasa mtu akitaka kuvaa kaunda hakatazwi, lubega hakatazwi utashi wa mtu binafsi, Nyerere hakufepologr ionsaryd
ReplyDeletemzuia mtu kuvaa anvyotaka, yeye kaenda china kavutiwa na choinlai kavaa, kavutiwa na kaunda suiti kavaa, watu wamemgeza sasa hoja iko wapi? Eeh wanadamu nyie hamna kheri!
Nilikuwepo hapo jangwani enzi hizo tyulikuwa hatuna hata uwezo wa kujenga majukwaa ya maana na matokeo yake tunajenga majukwaa ya mbao na kuezeka kwa makuti
ReplyDeletetumetoka mbali sana na mpaka hapa tulipofikia tumshukuru mungu.
Wengine wameona makuti sio ya maana wakati bado yanatumika kama urembo wa asili
ReplyDeleteSesophy
Nakumbuka hii ziara nilikuwa shule ya msingi darasa la sita. Nilikwenda kumsikiliza pope. Watu walikuwa Nyomi.
ReplyDeleteTanzania ya leo sio Tanzania ya enzi hizo maana kipindi hicho bado wazee wetu walikuwa wanasikilizana, vijana wanaheshimiana, dini na dhehebu vinakunywa pamoja. Leo yako wapi? inafurahisha ukikumbuka nyuma, lakini imauma sana ikitafakari leo. Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDelete