Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam asubuhi hii.
  Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba asubuhi hii kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.akifuatiwa na Mkewe,Pamoja na Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete (mwenye nguo nyeupe kulia).
 Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba asubuhi hii kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba asubuhi hii kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.
 Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akitoa heshima za mwisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. R.I.P Steven Kanumba

    ReplyDelete
  2. May God rest his soul in Peace.....AMEN

    ReplyDelete
  3. Michuzi pole sana,ila tunakuomba sana tujue historia ya maremu Kanumba.

    ReplyDelete
  4. Asante sana ankali michuzi tupo nawe moja kwa moja.

    ReplyDelete
  5. Kwa nini umeruhusu, ee mungu mwenyezi, yatusononeshee moyoni, kwa nini umeruhusu.Ona haya machozi, tazama tunavyoliiia, twajiuliza sana aa bwana ni kwa nini unaruhusu.
    Twayakumbuka, maaatendo yako, mema yasiyoelezeka , hatutakusahau, twakukukumbuka ulivyoishi vizuri, kwa muda ulikuwa nasi, hatutakusahau.....oooh kanumba

    ReplyDelete
  6. Was this a State funeral? Where everything is paid for by govt? We need to know, I think there are more needy people who would also like some help but they are just ignored. Our priorities - big mazishi, $$$$ siyo tatizo!!!

    ReplyDelete
  7. Dah! unbelivable kwa kweli msiba wa kijana wetu huyu umetuacha midomo wazi kweli kabisa kazi ya Mungu haina makosa ila kama kuna mkono wa mtu basi umeumiza watanzania wengi sana. Mungu ilaze roho ya kanumba mahali pema peponi amina.

    ReplyDelete
  8. Hapo safi sana , yaani mtenda mema hulipwa mema, yaani watu wameacha shughuli zao na kwenda kumzika Kanumba,kwa sababu alikuwa mtu wa watu,tutamkumbuka sana kwa utu wake,na sisi tuliobaki ,tujiangalie kwenye vioo-matendo yetu yako vipi ?? viburi,jeuri na kutukana watu,hatutapata heshima kama hii aliyoipata Kanumba, angalia Jeneza lake lilivyotulia -kama la Whitney Huston, yaani kwa kweli ,Kanumba kaondoka kwa kishindo.Ngwana Magese.

    ReplyDelete
  9. Michuzi you have the best blog ever we get to see the whole event katika muda muafaka sio kusubiri.......thanks RIP Kanumba

    ReplyDelete
  10. duuuh kweli kila nafsi itaonja mauti pumzika kwa amani kanumba tulikupenda sana lakini mungu alikupenda zaidi,this is unbelivable

    ReplyDelete
  11. Kaka Michuzi naomba weka youtube ya wimbo wake kuna sehemu kasema siku akifa hata adui zake watebeba jeneza na ujumbe mwingi wa maana

    ReplyDelete
  12. kweli kanumba umetutoka!Ok nakubali umetutangulia,Lala mahala pema peponi, Amin

    ReplyDelete
  13. INNA LILLAHI WAINNA ILEYHI LAJU'UN!
    YAANI JAMANI HUYU KIJANA KANIUMA MIMI,,NDIO KAZI YA MUNGU LAKINI EEE!INAUMA SANA SANA,,SIKU ZOTE WATU WEMA NDO HUONDOKA GHAFLA!,,UMATI WA WATU NDO UNAONYESHA KUWA ALIKUWA MWEMA SANA,,SI WA MATUSI WALA MARINGO,,SIKU ZOTE MTU AKISHAFARIKI HUWA WANATAJA MEMA YAKE LAKINI HUYU KANUMBA,,ALIKUWA HATAJWI KWA MABAYA YOYOTE KATIKA UHAI WAKE,,NA KWA NINI UMTAJE UBAYA WAKATI MASIKINI YA MUNGU ALIKUWA NI MTU WA KAWAIDA,UKILINGANISHA NA UMRI WAKE NA USTAR WAKE,,ALIKUWA HANA MAKUU,,NIMEUMIA SANA SIJUI MAMA YAKE MUHAYA MWENZANGU ANAFEEL VIPI,,MAANA ALIVYOKUWA AKILIA KWA KIHAYA IMENIUMA MNO,,SIKUJUWA STEVE KANUMBA ALIKUWA MWANATU..
    KAZIKWA KAMA RAIS,!!!
    ALIKUWA MTU WA WATU!!

    AHLAM,,,LONDON

    ReplyDelete
  14. Kanumba RIP. Tulikupenda sana lakini mungu kakupenda zaidi.Wote hiyo ndiyo njia yetu.

    Kanindo-Arusha.

    ReplyDelete
  15. haijapata kutokea tangu Baba wa Taifa alipofariki,kwa kweli Kanumba kagusa miyo yetu. Ametuachia somo watanzania tupendane. Mungu amurehemu. Kwaheri Kanumba.

    ReplyDelete
  16. Makaburi ya watu wengine yameharibiwa na umati wa watu waliokuwa huko Kinondoni cemetery leo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...