Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo lililoanza leo Aprili 18, kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipofika kufungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza leo Aprili 18, 2012 kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya Viongozi wa Dini, baada ya kuzindua rasmi Kongamano la Dini la waislam na Wakristo, katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Simon Shayo, wakati alipotembelea katika Banda la Chuo Kikuu cha DUCE cha jijini Dar es Salaam, alipofika kuzindua maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na Utafiti yaliyoanza leo Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kushoto ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo hicho, Abdul Njaid.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Ardhi, Prof. Mangisen Kaseva, wakati alipotembelea katika Banda la Chuo hicho baada ya kuzindua maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na Utafiti yaliyoanza leo Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kulia ni Ofisa Utawala wa Chuo hicho, Rosemary Bundara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa TCU, baada ya kufungua rasmi maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo, Aprili 18, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...