Habari Mkuu,

Naomba msaada wa kunitangazia tangazo hili, jana nikiwa Mjini Dar es salaam...nimepoteza pochi yangu yenye vitambulisho vyangu mbalimbali vya hapa Tanzania na vya Italy, zikiwemo leseni zote mbili. Naomba sana yoyote aliyeokota tuwasiliane kwa namba hii; 0767-191275.
Kwa yoyote aliyeokota nitatoa zawadi kwake, naomba sana.

Salamu sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. muschi b.c.April 20, 2012

    Baba pole sana, si unakumbuka mambo ya bongo land! Huwa wallet haiwekwaji mfuko wa nyuma! kurudishiwa bwana si rahisi wewe jiuendee tu polisi upate RB number uanze process ya documents nyingine mtu wangu.

    ReplyDelete
  2. sasa picha yako ya nini?

    ReplyDelete
  3. ingalikuwa pochi imepotelea zanzibar ungaliletewa hadi kwako,lakini dar... mmh sahau yakhe.

    ReplyDelete
  4. umepotezea maeneo gani? sema utajiwe maalwatan wa maeneo ukaonane nao

    ReplyDelete
  5. Nchi yetu itatuchukua a very long time kuwafikia wenzetu huku. Mimi nilipoteza wallet yangu hapa London mwaka jana (2011), ambayo pia kama mdau Chibiriti, ilikuwa na doc zangu karibu zote - NI card, driving licence, credit cards, etc. Nikaenda kutoa taarifa polisi instantly. Polisi walichukua namba yangu ya simu hafu wakarekodi hilo tukio limetokea wapi na muda gani approximately. Baada ya siku mbili tu nikapigiwa simu na polisi niende kituoni nikachukue Wallet yangu, kwamba imepatikana huko Oxford! Kumbe mtu kaiokota kwenye tube (underground train), yeye alikuwa akienda zake Oxford - nje kabisa ya jiji la London, so hakuweza kuireport mpaka mwisho wa safari yake. Basi nilienda nikachukua vitu vyangu vyote vikiwa intact!

    Contrast with Bongo, I have my doubts kama ningeipata wallet yangu. Namwonea huruma mdau wa Italy, jamani ndugu zangu, najua baadhi humu mtanibeza na kunitukana, lakini ninajua jinsi Chibiriti anavyohangaija sasa hivi cos I've been there, kwa aliyeiokota, pls msaidieni mmrudishie vitu vyake.

    Mdau
    Buckinghamshire

    ReplyDelete
  6. Pole sana ndugu.

    Utapata documents mpya baada ya kuripoti polisi.

    Lakini iwe funzo. Ukiwa mtembezi duniani kote, documents acha nyumbani. Nikija Bongo, vitambulisho, leseni ya gari N.k naacha nyuma. Nakuja na pasi tu na pesa. Nikipoteza pochi, napoteza pesa tu, hamna kitu chochote muhimu katika pochi. Hio leseni yako ya Italy itakusaidia nini Tanzania?

    ReplyDelete
  7. Habari wadau?mdau hapa juu unauliza sasa picha yake ya nini?jibu lake ni ilituweze kumjua huyu jamaa anaishi Itali.

    ReplyDelete
  8. Chibiriti..imepotea au umechomolewa?Kama umedondosha hata bongo watu wakiikokota wanapeleka polisi,tatizo la polisi wetu nao ukienda kuripoti nimeokota blah.. balah.. blah wanaanza tena kukusumbua wewe uliyepeleka na maswali kibao..ndio maana wakati mwingine raia wengi wanaogopa kupeleka vitu walivyoviokota polisi.Kama hiyo pochi umechomolewa hapo tena sahau mkuu manake wakikuta hakuna 'dola' wanatupilia mbali majalalani.

    David V

    ReplyDelete
  9. nawe chibiriti amaaa wasiwasi wanini kwani hiyo ni passport vituhivyo vyote ulivyopoteza una weza kuvipata vingine utakapo rudi italy na kama nipesa huna nenda ubalozi wa italy watakusaidia sasa pressure yanini minahisi pesa zimeisha sasa unataka kumtosa mtasha huyo ajue mmeibiwa chibiriti bwana acha mbwembwe chukua mchuma geuza.maisha ya bongo sio ya kwenda na mtasha, asubuhi mwenzio anataka conflakes au full breackfast,lunch bado sio mchezo hiyo conflakes tu bei zake mnazijua. pole chibiriti.

    ReplyDelete
  10. waweza kupata, wewe nenda eneo ambalo umepotezea hizyo wallet kama unapakumbuka, ongea na mateja, wenyewe wanajuana, wanaweza wakakupatia wenyewe au wakaipeleka kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa then watakupatia......

    ReplyDelete
  11. Bongo porojo nyingi. Mdau anatafuta documents zake, sasa kwa nini ajadiliwe yeye mwenyewe??? Kama hauna msaada wowote, kaa kimya. Siyo unapayuka tu bila mpangilio

    ReplyDelete
  12. nimegundua kuwa baada ya msiba ya kanumba, watoaji maoni walipungua kwa kiasi kikubwa sana. naona sasa wadau wanaanza kuchangia mada. Du, poleni sana. naona mme anza ku -recover from that shock!

    ReplyDelete
  13. Kuna watu wanapenda kuliharibu jina na sifa ya nchi kwa kutoa mifano isiyofanana na hali halisi ya mambo ilivyo.
    Huyo mdau wa Buckinghamshire aliyerudishiwa vitu vyake anataka kutuambia kuwa hakuna walioibiwa au kupoteza katika eneo analokaa na wakashindwa kurudishiwa?
    Kurudisha mali au vitu ulivyookota hakuna uhusiano na kuishi Tanzania.Kunategemeana na tabia na hali ya yule aliyeokota.MSITAKE KUTUDANGANYA TUJIONE SISI WATANZANIA NI MBUZI NA HAO WENGINE NI SMART!!!
    Mimi niliwahi kuokota pochi hapa NY na ndani mlikuwa na pesa na vitambulisho,nilichofanya nilichukua pesa zote (NILIKUWA NA SHIDA)na pochi nililitupilia mbali.
    Kuna rafiki yangu yupo Australia Yeye alipookota pochi alikumba vijisenti alivyovikuta na akampigia simu the owner aende sehemu aliyolitupa pochi.
    Kiufupi inategemeana na kila mtu alivyo.MSILETE UNAFIKI WENU WA KUHARIBU JINA LA NCHI YETU ETI TU KWA SABABU POCHI HALIKURUDISHWA!!!
    Halafu kwa kumalizia tu je haiwezekani kuwa huyu Chibiriti alitaka tu washkaji duniani wajue kama na yeye katua Bongo? Au alitaka awaoneshe wengine kuwa na sisi Bongo tuna uwanja wa mpira wakisasa?

    ReplyDelete
  14. Michu, naomba usiiweka kapuni hii, niweke mbele za haki ,nione wenzangu wanasema je ?? Ndugu Chibiriti kapoteza pochi yake, na hakukosea kuomba msaada ndani ya blogi yetu tukufu, sasa hawa wanaoponda bongo na wanajihakikishia kwamba Chibiriti asahau hiyo pochi kuipata, bora eti angelipotezea UK au America eti angeipata !!! Jamani huu uzembe wa mawazo nawaombeni mkome, bongo kuna watu wema wengi tu huenda kushinda hata huko mliko, Je ?? tuseme kwa mfano pochi imepatikana !!! mtasema kwamba Bongo imekuwa kama London ?? acheni zenu dharau,mnahangaika sana huko, kwanza kwa kuipata hiyo pesa ya kodi na kula yenu ya sanduwich au hotdog kwenye vigali vya barabarani-lakini mnavyoandika ,utafikiri nyie wote huko ni akina Obama. sikilizeni mlioko huko, kizuri sana mnachojifunza huko ni ile adabu na speed za kufanya kazi,maana Myahudi hakulipi bila ya wewe kumzalishia mara 3 yake, sisi huku hiyo adabu na speed za kazi za namna hiyo kwa kweli hatuna,sisi ni kutunga ugonjwa au kufiwa ndo zetu huku,sababu kubwa ya kuwa na tabia za namna hii Bongo hakuna pressure ya maisha,zamani kutoa contena bandarini ilikuwa inachukua mwezi-hadi Kikwete akapiga kelele,siku hizi kuna kauafadhari kidogo, anyway sitaki niende nje ya mada , Chibiriti ataipata pochi yake nina imani hiyo na Mungu aihitimize imani yangu na nyie huko msikimbilie kuwa mahakimu bila ya kwenda shule kuzijua sheria, na kingine Chibiriti kaja na dola zake 300, kakuta Bar zimejaa watu mpaka saa 10 za usubuhi-kitu ambacho Italy hakuna !!! alitegemea kujua bei ya nyumba za kienyeji chache zilizobakia Kariakoo akaambiwa bei ni Million 600 nyumba ya miti. Hana hamu. Zebedayo wa Zebedayo,mna Nasa (Mwanza-Tanzania.

    ReplyDelete
  15. HATA TANZANIA INAWEZEKANA KURUDISHA, TATIZI WANAOPOTEZA WENGI VITU WAKIENDA KU-REPORT POLISI WANATAJA NA VITU VINGINE AMBAVYO HAVIPO MFANO MTU ANASEMA NIMEPOTEZA VITU VYANGU PAMOJA NA FEDHA NA LAKI SABA (UNAKUTA MTU AKIOKOTA HAWEZI KULETA.

    ReplyDelete
  16. Ohhh Chibiriti Pole Mdau mwenzetu!

    Sitoi hukumu au kujenga dhana isipokuwa mara nyingi kwetu Wakonongo akufanyiae Ubaya ni mtu aliye karibu na wewe!

    Wanajua kuwa umetokea Italy na wanaamini inawezekana ukawa una chochote mfukoni hata kama huko unabeba Mabox!,

    Kwa namna hizi:

    1.Wanaamini wanaweza kupata chochote ndani kama mabaki ya EUROS au vitu vya Thamani.

    2.Kama unavyoona Wadau wanasema (Kila kitu Bongo ni gharama, kujisaidia, kuoga ,kukaa Mjini benchi la mpiga kiwi viatu,hata kuelekezwa mahali sasa ni gharama!) hata ukienda Polisi utatakiwa utoe kitu kidogo, na vile vile ukipoteza na kurudishiwa inatakiwa utoe kitu na hivyo utakuwa umewawezesha watu angalua kwa mlo mmoja na ulevi kidogo.

    Hivyo usihofu hiyo ni karibu Tanzania kutoka kwa jamaa zako wa karibu!

    ReplyDelete
  17. Pole Mdau Chibiriti!

    Tatizo mnapokaa Majuu mnakuwa mabahili wa Msaada kwa ndugu waliopigika huku nyumbani matokeo yake mnalizwa na hao hao ndugu zenu wa karibu wakiamini wanapata chochote humo.

    Ile tu kuwa umetokea Italy kila mtu atajua pochi lako litakuwa limenona hata kama wewe kule unaishi kwa Mafao ya Msaada wa Jamii !

    Sasa ni nani anaeweza kutarajia kuwa atapata kitu kwenye pochi lako kama sio jamaa zako wamechora hapo?

    ReplyDelete
  18. mdau wa oxford safi sana lakini ukiiokota pochi na kuipeleka polisi si ajabu ukawekwa ndani.......!!!!!??????^

    ReplyDelete
  19. pole sana chibiriti,hiyo imekula kwako kwani walio okota hiyo wallet wala hawaijui hii blog,hawajui internet,hawasomi magazeti,wala hawaangalii TVcoz wanalala vibarazani.nxt tym ol crucial doc shud b left home....!

    ReplyDelete
  20. sasa picha ya nini? ushamba wa kabila lako maana kila kitu huwa lazima mtumie kwa show-off.msiba,harusi,hata kupoteza vitu mweh! haya utaipata muda si mrefu ila sema umepotezea maeneo gani.yani kama dar ni magomeni kariakoo au sinza au kawe.sema exactly achana na show off za Italy nyuma ya kiwanja sijui.

    ReplyDelete
  21. Ile tu kukaa Italia imekuponza!,,,endapo ungekuwa umekuja Dar unatokea Kaliuwa-Tabora au Chalinze halafu ukasahau hata kama furushi lenye vumbi jekundu kibao hata liwe na Mamilioni ya Shilingi hakuna mtu angehangaika nalo ungelikuta!

    Sasa iwe mtu ametoka Majuu hata kama Pochi ina makadi na makaratasi nani asiizingatie?

    ReplyDelete
  22. Watu walivyoona umekuja na Demu wako huyo Mzungu wako pembeni hapo,,,ohhh wakaona ngoja wakupige Pancha kidogo ili usimalizie hela zote Hotelini!

    ReplyDelete
  23. Angalia sasa Bwana mkubwa Chiberiti wewe unakuja Bongo badala ya kukaa na sisi nyumbani kwetu ulikokulia Manzese unakaa na Demu wako Mzungu Hotelini?

    Ahhh si ndio wanandugu wakakuchorea mchoro upigwe kwanza!

    ReplyDelete
  24. POLE BWANA KAKA!

    Inaonyesha Ndugu Chiberiti unaleta Ujanja wako wa Italia na Ubahili wa Majuu wakati unajua wandugu Masela Vijana wa Maskani ya karibu yako wanaishi maisha Mabovu tu !

    Ulitakiwa angalau uwacheki kwa 500/= au 1,000/= kwa kila mmoja wasingekufanyia !

    Wala Vijana wa Maskani hawahitaji Mamilioni au Malaki ya Shilingi zako ni ile tu kuwawezesha kwa kununua 'Kete' za 'sigara zao' au 'Vichwiii' vya Mastimu ili walewe!

    ReplyDelete
  25. Pole na Matatizo !

    Bosi wa Italy tatizo unakuwa 'spana' sana kutoa mgawo kwa Masela Maskani wakati watu wameuwawa wamekufa kabisa wapo kaburini na Maisha vibaya kabisa,,,wamezeeka kwa shida za maisha ya Bongo unakuta mtu ana umri wa miaka 19 anakuwa kama Mzee wa miaka 91 hivi, unatoa hata mia mbili mia mbili watu wanaunga unga wanapata hata Glasi za Maziwa kupunguza moshi wa sumu vifuani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...