Inakuwaje unatuacha masaa machache kabla ya pasaka....,
hata hukusubiri nitoke nje ya nchi huku nirudi nyumbani tuagane mdogo wangu heh!
Kipindi fulani ulitukanwa na kusimamngwa sana huku ukiongezewa na vicheko vya kejeli kukusononesha mdogo wangu wakati ukiwa hai...,
leo hii umepumzika kimya wala hurudishii neno, ni lipi uliondoka nalo mdogo wangu, la furaha au sononeko.....??!!
Baba na Mama uliwaaga kwa amani, vipi wasanii wenzako, mashabiki wa wa kazi yako, vipi ndugu na jamaa na marafiki...
heh Kanumba, mbona ndio kwanza ulianza kusimama imara ktk sanaa na maisha kwa ujumla...!
Hainiingii akilini kama hauko nasi, ila hatuwezi kupingana na maamuzi ya Mwenyezi Mungu.
Mola akulaze mahali pema peponi, Amina.
Poleni sana wote tulioguswa na msiba huu, ila ni wakati wa kusherehekea mazuri mengi aliyoyafanya hapa duniani na kama lipo alilowakosea,
mumsamehee natumai naye atafanya vivyo hivyo,
Mola ndio Muumba wa vyote!
Frank Mtao
Australia


yaani roho inaniuma sana kwa kijana huyu! hatuna jinsi ni mapenzi ya mungu, mwenyewe mola amempenda zaidi, wahenga walisema "ivumayo haidumu", R.I.P. S.C.Kanumba.
ReplyDeletewe frank toa pole tuu, usiannze kushika watu ubaya. original comedy walivyom-komedy kanumba alipoenda bigbrother sio kwamba walikuwa hawampendi. sidhani kama watu comedy wanafanya comedy kwa ajili ya chuki??!
ReplyDelete