Mhe. Mathias Chikawe(Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) ameshiriki katika majadiliano ya mada mbalimbali wakati akihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Mpango wa uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi –Open Government Partnership.
Mhe Chikawe akichangia majadiliano kuhusu uzoefu uliopatikana katika utoaji wa huduma kwa Umma. Mhe. Chikawe alieleza historia ya utoaji wa huduma kwa umma nchini Tanzania. Pia alieleza changamoto mbalimbali ambazo Serikali Inazipata katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zenye ubora na kwa wakati. Pamoja na mambo mengine Mhe. Chikawe alisisitiza umuhimu wa kupitia na kuhuisha Mikataba ya Huduma kwa Wateja ili kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii. Katika majadiliano hayo Nchi za Kenya, Denmark na Estonia nazo zilitoa uzoefu wao.
Wadau kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia majadiliano kuhusu uzoefu uliopatikana katika utoaji wa huduma kwa umma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...