Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkuu wa Jeshi la akiba nchini Brigedia Generali R.M Muhuza hayupo pichani katika ofisi yake leo alipomtembelea kujitambulisha na kueleza juu ya ujio wake Mkoani Rukwa ambapo ni kuona matayarisho ya kikosi cha mgambo cha Mkoa wa Rukwa ambacho kitashiriki kwenye zoezi la kijeshi litakalohusisha Vikosi vya JWTZ vilivyopo katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini (Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa, Lindi, Mtwara, Njombe na Katavi) ifikapo tarehe 15 Septemba 2012. Zoezi hilo la kijeshi litaandaliwa na Brigedi ya 401 KV iliyopo Songea Mkoani Ruvuma. Jumla ya Wanamgambo 60 kutoka Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kushiki zoezi hilo litakalojumuisha vikundi toka Kamandi zingine za Ndege za Kivita, Wahandisi, Mizinga na Vifaru.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Jeshi la akiba nchini Brigedia Generali R.M Muhuza, Msaidizi wake Kanali A.Y Amasi na Katibu wake Meja A.R Gumbo kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Dar es Salaam wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa walipomtembelea Ofisini kwake leo.
Miongoni mwa mambo aliyosisitiza Mkuu huyo wa Mkoa ni uboreshwaji wa sekta muhimu nchini kama sekta ya ulinzi ili kuepusha uvunjifu wa amani iliyodumu nchini kwa muda mrefu. Alisema Jeshi la Wananchi lina jukumu kubwa la kuhakikisha amani inakuwepo nchini na sio kutokana na hatari zinazoweza kutoka nje bali kwa hatari zinazoweza kusababishwa na wananchi wenyewe.
Mazungumzo yakiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akifafanua jambo (Picha na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa RUKWA)
MR MISUPU PLEASE AMENDI JINA NI BRIG GE RAPHAEL MUGOYA MUHUGA
ReplyDeleteBY CARLOS MUHUGA
Kwa uhalifu na uhatarihsaji wa amani ufanywao na wana Chadema Arusha:
ReplyDeleteMkuu wa Mkoa wa Arusha nae angefanya zoezi la kuwakaribisha Maafisa wa Jeshi kama alivyofanya Eng. Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa!