Mtoto Farid Rashid akiwa na baba yake anbaye anaomba msaada kumpunguzia mateso ayapatayo


Mtoto  Farid Rashid mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 8 anasumbuliwa na tatizo la kuziba kwa mirija  inayosafirisha haja ndogo( mkojo) kati ya Figo na Kibofu cha mkojo.
Baba Mzazi (Rashid Said)  wa mtoto huyo anawaomba msaada wadau mbalimbali ili aweze kumpeleka mtoto Farid nchini India kwa matibabu zaidi.

“Mwanangu anajisaidia kwa maumivu makali, sema kweli ni mateso makubwa kwa mtoto, naomba mnisaidie mwanangu apate matibabu” hayo ni maneno ya baba mzazi wa Farid (Rashid Said).

Akizungumza na Msimamizi wa Mtandao wa habari wa  MO BLOG Bi. Johari Kachwamba Ndugu Rashid Said amesema amemzungusha kwa matibabu mtoto Farid katika hospital mbalimbali za hapa nchini bila mafanikio ikiwa ni pamoja na kulazwa zaidi ya miezi mitatu(3) katika hospitali ya taifa ya Muhibili.

Katika juhudi za wazazi wa Farid kutafuta misada, wamefanikiwa kupata tiketi moja (1) ya ndege, dola 1,500 pamoja na Shilingi Milioni moja (1) lakini bado haitoshi.
Hata hivyo tayari wamefanikiwa kupata hati za kusafiria (Passport) na VISA ya nchini India ambayo inakoma (expire) 19-06-2012.

 Hivyo anaomba msaada wa kupata tiketi nyingine pamoja na gharama za matibabu.

Nambari ya simu ya baba mzazi ni +255655-000556 
au wasiliana na MO BLOG 
kupitia nambari 0714-940992.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. si aende wizara ya afya wanapeleka wananchi wa kawaida india watamsaidia...aulize wizarani apewe utaratibu..

    ReplyDelete
  2. Jamani Wandugu suala la dharura kama kuumwa kuuguliwa halina taarifa na linaweza kumfika yeyote yule huku akiwa ktk hali yeyote ile,,,tutoe Msaada kama uwezekano upo na sio kutoa maneno ya kebehi, Ustaarabu hauna Chuo cha Mafunzo, tujaribu kuwa na Ubinaadamu !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...