BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba yao katika kusherekea Sikukuu ya Pasaka ambapo wamesema kuwa wataanza kutoa burudani ndani ya Wipes Bar Mivinjeni Kurasini, siku ya Ijumaa watakuwa Leanders Club Kinondoni, Jumamosi watakuwa TCC Club Chang’ombe, Pasaka watakuwa Kata ya 14 Temeke na Jumatatu ya Pasaka watakuwa sambamba na FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’.

Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini kinachoendelea ndani ya bendi yao.

Alisema kuwa hata hivyo tayari wamejipanga vizuri katika suala zima la kuwapa burudani mashabiki wao katika kusherekea sikukuu hii ya Pasaka.

“Msondo ipo kamili katika kutoa burudan na ndiyo maana imeamua kutoa ratiba, hivyo tunaamini mashabiki wetu watakuja kwenye matamasha yetu kwani bila wao sisi hatuwezi kusimama na kuimba,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa wanahitaji mashabiki wao kjitokeza kwa wingi ili waone nini wanachowapa katika siku hizo zote kwani sikukuu ya pasaka ni muhimu kusherekea na msondo ngoma bendi hiyo inayotamba na
vibao vyake vipya vya Suluhu wa Shabani Dede na Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu pia watapiga nyimbo zao zote zilizotamba kipindi cha nyuma alisema Super D.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii ratiba ya WIPES haijakaa vizuri, hapana tofauti sana na PENTAGON wanapopiga wale jamaa zetu wanaoelekea kupotea katika anga hili la muziki wa dansi asilia. Tuwe makini kwenye kuchagua kumbi za kupiga kasehemu kale ni kadogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...