Mtangazaji mkongwe Sekione Kitojo wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (DW) akiwa na wachezaji wa timu ya daraja la kwanza nchini Ujerumani , Bundesliga, FC Augsburg, Juu akiwa na Koo kutoka Korea ya kusini na chini akiwa Marcel Ndjeng mwenye asili ya Cameroon na ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Cameroon, alipotembelea hivi karibuni mjini Augsburg kwa vekesheni. Kitojo anakumbukwa na wengi kama mmoja wa watangazaji hodari wa mpira enzi za Radio Tanzania Dar es salaam, enzi za kina Charles Hilary, Salim Mbonde, Ahmed Jongo na wengineo.
Picha na mdau Malumbo Salim jr.
Picha na mdau Malumbo Salim jr.
Sekione Kitojo namkumbuka sana kwenye mpira enzi wa Radio TZ. Picha ya kwanza ametokea kijana mno hadi nilidhani ni mtoto wake.
ReplyDeleteNi kweli..Sekione Kitojo enzi za RTD ulikuwa unatangaza mpira vizuri sana..sauti yako ilikuwa bomba mkuu.Nilikuwa bado mdogo,nilidhani umeshakuwa mzee..bado unadai!!
ReplyDeleteDavid V
Angekuwa Tz angeshachoka na maisha, lakini Ulaya bado ni kijana.
ReplyDeleteHapa Tz angeishia na pombe kwa wiiiingi (oh samahani wadau!) ukizingatia kwamba chakula chenyewe michosho basi ungemkuta yuko hoi.