Wiki iliyopita nilikuwa kwenye ofisi ya Jumuiya yetu nikiongea na baadhi ya vijana waliowasili hivi karibuni kutokea “UBATANI”(Hili ndilo jina tulitumialo badala ya “UTURUKI”kama vile litumikavyo jina “UMANGANI” badala ya “UGIRIKI” )
Ilijionesha wazi katika mazungumzo yetu kuwa picha waliyokuwa wakiidhania ilikuwa ni tofauti mno na hali halisi waliyokumbana nayo.Baadhi yao wamekuja na seaman book wakitegemea wangepata kazi ya melini mara tu watapofika!!!
“Niliambiwa nikifika Umangani kuna meli kibao zinatafuta mabaharia na mshahara ni buku!!!Lakini tangu nimefika hapa nimegundua kuwa zilikuwa ni kamba tu za washkaji maana hata huko bandarini si rahisi kukaribia”Alisema mmoja wa vijana hao kwa unyonge na uchungu.
Mwingine aliongezea akikuna kichwa “Nimelazimika kuomba msaada kwa washkaji zangu waliopo UK ili nitafute mchongo wa kuchomoka maana hali nilivyoiona sivyo nilivyoambiwa na hadi sasa washkaji wenyewe wananipa story tu”
“Mimi rumba nililishtukia tangu pale tulipokuwa tunabinjuka toka ubatani baadae tukakamatwa na kuwekwa kambini,Walipotuachia tuje Athens nikampigia simu mama anitafutie tiketi ya kurudi!!!!Alisema kijana aliyekiri kuwa hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kusafiri nje ya nchi.
Nimelazimika kuielezea mifano hai hiyo nikiwa sina lengo la kufichua siri za jandoni,bali niweze kupata nafasi ya kutoa picha kwa wale wanaopanga kufuata njia hizo hizo bila ya kuwa na picha kamili ya hali halisi itayowakabili ambao wengi wao hawana ule ubavu wa kukabili mazingira kama walivyoyakabili wasafiri wa zamani ambao walivumilia mengi magumu zaidi ya haya.
Namalizia kwa taarifa ifuatayo:
Serikali ya hapa imepitisha bungeni hivi karibuni sheria ya kuanzisha kambi za kuwahifadhi wageni wanaoingia nchini kinyume cha sheria. Kuanzia sasa wageni wakibinjuka hawatakuwa wanaachiwa waende Athens, badala yake watahifadhiwa (WATAFUNGWA) katika kambi hizo hadi pale utapopatikana uwezekano wa kuwarudisha makwao.
Tunawaomba vijana wote wataofikiria kupitia njia hizi walijue hili, ili wasije wakawatia presha wazazi wao pindi watapokuwa wamefungwa na hatimae kurudishwa.
Niliyoyasema si vitisho bali ni wajibu wetu kuwajuza ndugu zetu wa nyumbani wasioijua hali halisi ya huku na baada ya hapa wao wana haki ya kuamua kuja au kutokuja. .
Kwa kuhakiki maelezo niliyoyatoa kuhusu kambi za kuwafungia wageni wanaweza kuingia google kabla hawajaamua kuja.TAARIFA YA MWISHO NI KUWA WAMEPELEKWA WAGENI 56 KATIKA KAMBI MPYA ILIYOPO KIJIJI CHA AMYGDALEAS.ITAYOKUSANYA WAGENI 1,200.
Ahsanteni
KAYU LIGOPORA
KATIBU MKUU JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI
Hii inaonyesha wazi Katibu huna uelewa na WaTZ wahangaikaji katika nchi mbali mbali. WaTz wamekuwa wakienda Greece kwa miaka mingi iliyopita kabla mambo ya kujiripua hajaanza na uingiaji ulikuwa ni huo huo wa kubinjuka na kihalali kwa wale wenye pesa za kutosha. Inaonyesha wewe Katibu uliingia Greece kwa viza ya mwanafunzi na ukabaki. Hujui lolote lile linalohusu uhangaikaji katika nchi za watu. Hivi sasa kuishi katika nchi za Ulaya ni rahisi sana kama utajiripua na baadae kuzaa mtoto. Ombi langu kwa WaTZ waliofika nchi za nje wasijifanye viongozi wakati wao walifika huko kama mwanafunzi au afisa ubalozi. Acha majungu.
ReplyDeletesi mrudi tu, kwani lazima mkae huko? EU yote sasa hawataki wageni kazi hamna.
ReplyDeleteAHSANTE KIONGOZI KATIBU WA JUMUIYA KAYU LIGOPORA!
ReplyDeleteLa muhimu umefafanua ktk taarifa yako juu ya hali halisi, pia kwa mtazamo wangu kulingana na nilivyoisoma hii taarifa na kufuatilia mabadiliko ya matukio yanayojiri Duniani, kama anavyosema Mdau mtoa maoni wa pili EU (Umoja wa Ulaya) na Dunia nzima kazi ni tatizo kutokana na kuporomoka kwa hali ya Uchumi Duniani.
Tatizo jingine ni kuwa Vijana wengi wanazo taarifa za hali ilivyokuwa wakati huo wa neema miaka kibao tu iliyopita kitambo, wakati hali hiyo imebadilika imebaki ni hadithi na Historia za zamani za kale.
Kitu kingine, Vijana wengi hasa wanaopenda Usafiri hukurupuka tu, kupenda kusafiri kwa kutegemea bahati na kubabaisha tu,
Wengi wao hata wengine waliopo nje hawafuatilii masuiala ya Kimataifa, na ndio maana wanakuwa na rekodi iliyopitwa na wakati kama hao vijana wanavyosema kuhusu kupata kazi Ugiriki mara tu waingiapo, kitu ambacho kwa sasa hakuna!
WAKAE WAKITAMBUA KUWA DUNIA HAIGANDI INAENDA NA MABADILIKO, KISIASA,KIFEDHA,KIUCHUMI, KIDIPLOMASIA NA KIJAMII KILA DAKIKA.
Mtoa comment,unachokisema kuna ukweli wake lakini pia inategemeana na nchi,Kuna jamaa mmoja sitaki kumtaja jina ana watoto wawili Norway lakini huu ni mwaka wa 17 bila bila na hawezi kwenda popote.Ulipuaji pia sasa hivi mgumu,ujilipue upate unachokitaka na case nyingi sasa hivi ni miezi 6.Usipopata unachokitaka baada ya hapo mambo ni magumu.Tusidanganyane kua kuishi EU ni rahisi sana kuliko wakati wowote.Ukitaka kujua fuatilia campaign za urais France,Belgium ichaguzi mwezi wa 10 fuatilia pia.On top of that family reunion inazidi kua ngumu pia,jamaa wanakaza kamba kila kukicha.Hatuwezi kukataza anayetaka kujaribu lakini ajaribu akiwa anajua hali halisi,siyo mtu anachukua 10M au anauza kiwanja chake anajua akija mambo yanamnyookea mara moja.
ReplyDeleteNa wewe nawe nani kakuambia Greece iko EU!! Elewa kwanza dunia invyokwenda kabla ya kuchangia.
ReplyDeleteTaarifa iliyotolewa na katibu ni nzuri na inafaa kupongezwa maana inamsaidia anayetaka kuja huko afikirie mara mbili mbili kama aende ama asiende. Mdau anayeponda taarifa hii nadhani ana matatizo yake binafsi, aonewe huruma na apuuzwe tu!
ReplyDeleteacha roho ya kwanini ndugu yangu utakufa mdomo wazi-Mdau muddy shaweji-Italy
ReplyDeletelakini hii news ililetwa zamani na vijana ikakanusha vibaya vibaa kwenye maface book tukaambiwa matona nahadija kopa tunajirusha sasa leo imekuaje tena jumuiya kutamka hivi au Mkuki ni Kwa ngurue tu?
ReplyDeleteMsema kweli
anonyymous wa pili unasema hivyo kwasababu baba yako fisadi ambao ndio wanaotufanya tukae huku.
ReplyDeletemimi sina lakusema hapa ila nacheka huyo aliemkosowa mwenzake kuhusu GREECE si EU ....haya atwambie ni wapi, au ndio tuseme iko karibu na uganda
ReplyDeletemaana nimesikia tanzania inataka kujiunga na KENYA,UGANDA, NA GREECE nayo imo
Tatizo ni hili:
ReplyDeleteWatanzania huwa tunaendesha mambo kufuatia 'mazoea' kuwa huwa tunafanya hivi na vile au 'kusikia' niliambiwa kuwa hivi na hivi:
Mifano:
1.Wasafiri wengi nje hasa vijana wanasafiri wakiwa na taarifa za miaka ya nyuma (ILIVYOKUWA miaka ya 1980's na 1990's huko nyuma kutoka kwa watu walioona miaka hiyo kitambo walipokuwa huko Majuu) taarifa ambazo kwa sasa zimepitwa kabisa na wakati.
2.Wengi hawafuatilii habari za Kitaifa na hasa Kimataifa. (Kama inavyoonekana taarifa anazotoa Katibu Kayu Ligopora kutoka kwa vijana walioingia zinaonyesha Vijana walionana na watu waliofika Ugiriki miaka hiyo kitambo huko nyuma)
MAMBO YAMEHARIBIKA KWA VILE IMEFIKIA SASA MZUNGU AMEANGUKA KIUCHUMI PAMOJA NA UJANJA WAKE WA KUENDESHA MAMBO KA MPANGILIO,,,MAJI YAMEZIDI UNGA!
wengi wenu mlolalamika na kuonyesha hali ya kukata tamaa na kulilia kurudi nyumbani inaonyesha wazi kuwa hamna spirit ya kusafiri mnaiga tu kuja maisha ya viwanjani maisha sio lelemama kila mtu ana bahati yake katika maisha ya kutafuta
ReplyDelete