Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya waombolezaji wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba Sinza Vatican jijini Dar es salaam leo kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisaini kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa  mwigizaji  mahiri nchini, marehemu Steven  Kanumba, nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es salaam. 
 Waziri Mkuu,Mizengo  Pinda  akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Rehema Nchimbi  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Aprili 9,2012 kuhudhuria kikao cha Bunge  kinachotarajiwa kuanza 
kesho asubuhi. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwa maelezo ya mdogo wake Kanumba inawezekana kabisa kifo cha Steve kingeepukika kutokana na yafuatayo:- kama kumngekuwa na mtu aliyekuwa trained kutoa huduma ya kwanza Steve angefanyiwa CPR na ingeweza kuokoa maisha yake. La pili urasimu uliopo Tanzania kwamba mtu anapoumia au umizwa mpaka aende polisi kupewa PF3 hii ni processes ndefu sana na itaendelea kusababisha vifo vya wengi kwani inabidi kubadilishwa na mtu akimbizwe kwanza hospitalini kupata huduma kisha mambo ya polisi ndo yafuatie. Maoni kwa wale wote wanaojiona ni watu wenye vipaji wakati wote itabidi muwe na team ya madaktari wa huduma ya kwanza popote pale mnapoenda, itabidi muingie gharama za kuwalipa. Pawepo na walinzi wa mwili(body guards) wakati wote hata mkiwa majumbani kwenu na sehemu zote za starehe, hii itapunguza kushambuliana na itaongeza usalama zaidi kwa wana vipaji wa Tanzania(celebreties) Kwa kuzingatia maoni yangu tutaokoa maisha ya waliowengi kwani wamezungukwa na maadui wa kila aina na kuna mashambulizi yanayoendelea kwa wenye kwa wenye ya kimwili na kiroho. Mwenyezi Mungu ampumzishe kijana wetu katika pumziko la milele Amen!

    ReplyDelete
  2. Kanuni ni ileile baada ya Mafanikio ya kimaisha kinachofuata ni Uadui licha ya kuwa matokeo katika maisha yetu mengi yake ni mipango ya Mungu !

    ReplyDelete
  3. Hawa clouds waache unafiki, wakati kanumba alipoenda kwenye jumba la big brother redio yao ilimchafua sana kanumba kwamba hajui kingereza leo hii ndio wa mbelembele

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...