Rais Dkt. Jakaya Kikwete akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi na Waziri wa Sheria na Katiba Mama Celina Kombani.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakitoka chumba cha mikutano Ikulu baada ya Rais kutangaza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakimsubiri Rais Kikwete kuja kutangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo Ikulu jijini dar es salaam.
Rais Kikwete akitoa ufafanuzi kuhusu Tume ya mabadiliko ya Katiba aliyoitangaza, akisisitiza kwamba tarehe ya kuanza kazi itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadae kuapishwa. Ila kisheria tume inatakiwa iwe imekamiliosha kazi ndani ya miezi 18.


TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
(Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,
Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7)
______________________________


UONGOZI WA JUU

1.
Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA  
-  Mwenyekiti
2.
Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino
RAMADHANI
-  Makamu Mwenyekiti


WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - BARA

1.
Prof. Mwesiga L. BAREGU 

2.
Nd. Riziki Shahari  MNGWALI 

3.
Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI

4.
Nd. Richard Shadrack LYIMO

5.
Nd. John J. NKOLO

6.
Alhaj Said EL- MAAMRY

7.
Nd. Jesca Sydney MKUCHU

8.
Prof. Palamagamba J. KABUDI

9.
Nd. Humphrey POLEPOLE

10.
Nd. Yahya MSULWA

11.
Nd. Esther P. MKWIZU

12.
Nd. Maria Malingumu KASHONDA

13.
Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)

14.
Nd. Mwantumu Jasmine MALALE

15.
Nd. Joseph  BUTIKU



WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - ZANZIBAR

1.
Dkt. Salim Ahmed SALIM

2.
Nd. Fatma Said ALI

3.
Nd. Omar Sheha MUSSA

4.
Mhe. Raya Suleiman HAMAD

5.
Nd. Awadh Ali SAID

6.
Nd. Ussi Khamis HAJI

7.
Nd. Salma MAOULIDI

8.
Nd. Nassor Khamis MOHAMMED

9.
Nd. Simai Mohamed SAID

10.
Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA

11.
Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN

12.
Nd. Suleiman Omar ALI

13.
Nd. Salama Kombo AHMED

14.
Nd. Abubakar Mohammed ALI

15.
Nd. Ally Abdullah Ally SALEH



UONGOZI WA SEKRETARIETI

1.
Nd. Assaa Ahmad RASHID
-  Katibu
2.
Nd. Casmir Sumba  KYUKI
-  Naibu Katibu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Leo ni Ijumaa Kuu siyo siku ya Kazi

    ReplyDelete
  2. Serikali KUU (IKULU),Hospitali zote, Idara ya Usalama na Polisi hazina LIKIZO WALA SIKUKUU !

    ReplyDelete
  3. kikwete (my president)umefanya kama inavyotakiwa lakini tukiangalia umri wa hao wakuu wa hiyo tume mbona umekwenda sana huoni kama hicho kitakua ni kikwazo hebu angalia wanatutengeneze katiba au wanatuachia usia tafadhali mkuu wangu hebu penyeza vijana kwa wingi

    ReplyDelete
  4. Umesahau, ndege na meli mabasi na daladala zote zinatembea au na wao waende kulala sikukuu. Nyumbani mama lazima apike chakula, petrol station zifungwe na zenyewe na umeme uzimwe, Tanesco wasifanye kazi na nyumba yako ikiungua fire wasifike maana ni sikukuu. Nakwambia ukumbi una wajinga kuliko werevu.

    ReplyDelete
  5. watu hawa ni wengi sana hakuna na haja ya kuwa na timu ya wanzibari na watanzania bara kwanini tusiunde timu ya watanzania tuangalie katiba yetu namuunga mkono aliosema wazee amejazaa wazee watupu yaani jamani hakuna watu wengine tanzania hii wenye zaidi ya hawa ambao tumewasikia tangu tukiwa vidudu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...