Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa Marehemu Rais Wa Malawi Bingu wa Mutharika, Bi Calista Mutharika wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwa marehemu Ndata,Wilayni Thyolo, nje ya jiji la Blantyre, Malawi leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Malawi, marehemu Profesa Bingu wa Mutharika,wakati wa mazishi yaliyofanyika shambani kwa marehemu Ndata,wilayni Thyolo leo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Malawi marehemu Prof.Bingu wa Mutharika, kijijini Ndata,wilyani Thyolo, nje ya jiji la Blantyre, nchini Malawi leo. Pembeni yake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Malawi Marehemu Prof.Bingu wa Mutharika wakti wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake Ndata,Wilaya ya Thyolo, nje ya jiji la Blantyre, leo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais mpya wa Malawi Bibi.Joyce Banda wakati wa mazishi wa Rais wa zamani wa Malawi Marehemu Prof.Bingu wa Mutharika kijijini kwake Ndata, wilayni Thyolo, nje ya Jiji la Blantyire leo asubuhi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu
Ninaomba msaada kwa mtu yeyote anayefahamu lugha maarufu ya watu wa Malawi...ni kuhusu hili neno Ngwazi. Marehemu Banda alikuwa anaitwa Ngwazi Dr. Kamuzu Banda na marehemu Bingu naye anaitwa Ngwazi Professor Bingu wa Mutharika. Je, hii Ngwazi ina maana kama Ndugu...au namna gani? Naomba msaada.
ReplyDeleteThe title Ngwazi means "chief of chiefs" (more literally, "great lion", or, some would say, "conqueror") in Chicheŵa.
ReplyDeleteMama Mutharika atanyakuliwa na nani? Hakuna raisi single? Kama mke wa Samora alivyonyakuliwa na Raisi Mandela. Pole nyingi kwa Madame Mutharika na waMalawi wote. Upumzike kwa amani Raisi Mutharika.
ReplyDelete'Inawezekana' Mama Mutharika akanyakuliwa na Gen. SERETSE KHAMA Raisi wa BOTSWANA yeye ndio yupo single kwa Maraisi wa Kanda yetu hii kwa sasa.
ReplyDelete