Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Chiku Gallawa akifungua rasmi Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mjini Tanga jana. Mkutano huo ulijumuisha wanachama wapatao 270 ikiwa ni pamoja na viongozi wa Serikali na Siasa wa mkoa huo, waajiri, watoa huduma za afya na wanachama wa Mifuko ya NHIF na CHF.
Mh. Chiku Gallawa akikabidhi msaada wa mashuka 770 yenye thamana ya Sh. 7.7 Milioni ambayo yametolewa na NHIF kwa hospitali na vituo vya afya vya Mkoa wa Tanga na wilaya zake. Tukio hilo lilifanyika mjini Tanga wakati wa mkutano wa wadau wa Mifuko hiyo kwa mkoa huo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Hamis Mdee akikabidhi kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga moja ya Mashuka 150 ambayo yametolewa kwa Hospitali ya Bombo katika kuadhimisha miaka 10 ya Mfuko huo.
Hospitali ya Bombo mjini Tanga wametenga sehemu maalum ya kuwahudumia wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Suala hili limefanyika ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanachama wa mfuko huo.

Wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wa Mkoa wa Tanga jana ambao ulijumuisha wadau wapatao 270, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa alisema wanafurahi kwa taarifa kwamba Tanga ni ya kwanza Tanzania kwa kusajili asilimia 52 ya wananchi wake katika Mifuko wa Afya ya Jamii. 

Hata hivyo alionyesha kutokuridhishwa na asilimia hiyo na kutoa rai ya kuongeza kasi na kuingiza katika mpango mkakati wa utekelezaji wa shughuli za mkoa kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015 wananchi wote wa Tanga wawe wamejiunga na mifiko ya bima ya afya ya CHF, NHIF na TIKA.

Aidha, Mhe. Gallawaalibainisha kuwa Siku Kuu ya Mei Mosi imepangwa kufanyika kitaifa mkoani Tanga, aliwataka viongozi kuitumia nafasi hiyo kikamilifu katika kuwahimiza wananchi kujiunga na Bima ya Afya

Nae Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Hamisi Mdee wakati akitoa maneno ya utangulizi, aliwahimiza watoa huduma na halmashauri za Mkoa wa Tanga kuitumia fursa ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo inayotolewa na NHIF ili kujiepusha na swala la ubovu wa miundombinu na ukosefu wa vifaa tiba katika vituo vya afya.

Wakati akitoa taarifa ya huduma za NHIF katika hospitali ya Bombo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo amesema wamefungua kitengo rasmi cha kuwahudumia wanachama wa NHIF ili kuhakikisha huduma bora za matibabu kwa wanachama hao. Kutengo hicho kitatoa huduma ya kuwaona madaktari, vipimo pamoja na dawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...