
Uendelezo wa Mwanadamu aliyezaliwa na Mwanamke na kuumbwa kwa udongo, hutegemea sana pumzi na uhai kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ingawa Mwanadamu huwekwa katika kundi la wanyama, lakini huesabiwa kama mnyama mwenye akili kuliko wote. Ila kuna baadhi ya mambo kwake huwa ni giza......watu wengi tulishawahi kujiuliza sana; kwanini hatuijui kesho wakati tuna Kalenda majumbani mwetu? au tulishawahi kuwaza ni kwanini hatuijui kesho yetu? na mara nyingine ulishawahi kujiuliza pindi utakapo lala huelekea wapi? Hakuna ambaye ana jibu sahihi......hasa swali zito kwetu ni kuwa si kulala tu! ila mara nyingine huwa tunajiuliza kwanini tunakufa? na tunakwenda wapi baada ya kufa? na kipi kitakacho sababisha kifo chetu? Ingawa ni matamanio ya kila Mwanadamu, kutamani kufahamu hata tarehe, muda na wakati ambao Israeli atakuja kukatisha maisha yetu!
Daima tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote na kwa uhai anaotujalia......maana hatujui lini tutaitwa kwake. Kwakweli kifo cha Steven Kanumba kimetusikitisha sana, pole sana kwa wanandugu na jamaa wote.....ni majonzi makubwa kwetu sote, ila hatuna budi kumwombea ili Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani....Amina!
-BARAKA wa CHIBIRITI


Asante kwa pole na wewe pia ila Chibiriti unavituko, Hiyo ndo kadi?
ReplyDelete