Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma,SSP Kihenya wa Kihenya akionyesha moja ya silaha zilizosalimishwa na Mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyankwi kilichopo katika Kata ya Busunzu Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma alietambulika kwa jina la Tora Muhoza (42).

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyankwi kilichopo katika Kata ya Busunzu Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Bw. Tora Muhoza(42), amesalimisha silaha moja ya kivita aina ya SMG ikiwa na sirasi mbili kwenye magazine yake.

Silaha hiyo yenye namba BA 178645 ilisalimishwa kwa Mtendaji wa Kata ya Busunzu na baadaye kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya wa Kihenya, amesema kuwa kusalimishwa kwa silaha hiyo kunatokana na msako mkali unaoendeshwa na Jeshi hilo baada ya muda uliotolewa na serikali wa kusalimisha silaha kumalizika.

Kamanda Kihenya amesema kuwa pamoja na kumalizika kwa muda huo, lakini Jeshi la Polisi limeacha kumchukulia hatua mwananchi huyo kutokana na kuamua kujitokeza hadharani kwa hiari kuisalimisha silaha hiyo kwa mtendaji wa kakta hiyo.

Katika kuhakikisha kuwa hali ya amani na utulivu inaendelea kudumu mkoani Kigoma, Jeshi la Polisi limeendelea kufanya operesheni ya kupambana na vitendo mbalimbali vya kihalifu vikiwemo vya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Kamanda Kihenya amesema kuwa hiyo ni silaha ya tatu kusalishwa mkoani humo katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Amesema pamoja na kusalishwa kwa silaha hizo aina ya SMG pamoja na risasi kadhaa, Polisi pia imewakamata
watuhumiwa 11 waakiwemo wa makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu.

Jeshi la Polisi mkoani humo limeendelea kutoa wito kwa wananchi mkoani humo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi mara wanapobaini kuwepo kwa makundi ya wahalifu ama mhalifu mmoja mmoja ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kaka michuzi,waambie vjana wanaochapisha hizi habari wawe wanazisoma poleX2 japo mara mbili kabla ya kuzirusha hewani..makosa madogo madogo yanaongezeka kaka

    ReplyDelete
  2. Ahsante kwa kusalimisha silaha,

    Ni vizuri tukawa na Mfumo wa kutoa Ruzuku kwa watakao kubali kubadilika kimaisha kwa ridhaa yao wenyewe ili kuongeza ari na uwezo wa kujitambua.

    Mfano:
    1.Ruzuku kwa watakao acha Uhalifu,
    2.Ruzuku kwa watakao acha Wizi na Uhalifu,
    3.Ruzuku kwa watakao kubali kurudi Vijijini,
    4.Ruzuku kwa watakao lima mazao yalioelekezwa kwa kipaumbele.
    5.Ruzuku kwa watakao kubali kazi za wito ,n.k

    Hao waliosalimisha silaha ni vema wakafikiriwa kwa uwezeshaji ili waweze kujimudu kimaisha baada ya kuachana na kazi ya Ujambazi !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...