MGAMBO SHOOTING YAPUNGUZWA KASI FDL

Fainali ya 9- Bora ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwania tiketi za kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao imeendelea kushika kasi leo (Aprili 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro kwa Mgambo Shooting ya Tanga kuvutwa shati.

Mgambo Shooting ambayo hadi kabla ya mechi za leo (Aprili 15 mwaka huu) ilikuwa ikiongoza kwa pointi 11 imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Polisi Tabora ambayo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika ilikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Mabao ya Polisi Tabora yalifungwa dakika ya tano na Ernest Nkandi kwa shuti kali lililomshinda kipa Kulwa Manzi. Keneth Masumbuko aliifungia Polisi Tabora bao la pili dakika ya 40.

Mgambo Shooting inayofundishwa na beki wa zamani wa Taifa Stars, Joseph Lazaro ilikianza kipindi cha pili kwa nguvu na kufanikiwa kupata bao dakika ya 58 lililofungwa kwa shuti kali nje ya eneo la hatari na Salum Kipaga.

Dakika saba kabla ya filimbi ya mwisho, Juma Mwinyimvua aliipatia Mgambo Shooting bao la kusawazisha akimalizia pasi ya Fully Maganga kutoka wingi ya kushoto.

Fainali hiyo inashirikisha timu tisa ambapo tatu za kwanza zitafuzu kucheza VPL msimu ujao. Timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo ni Rhino Rangers ya Tabora, Trans Camp ya Dar es Salaam, Mbeya City, Tanzania Prisons ya Mbeya na Mlale JKT ya Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Poulsen anaenda kuangalia michuano hii au anapiga soga na 'watoto' wa Daresalaam??.Kuna timu inaweza isipannde daraja lakini ikawa na wachezaji wazuri vile vile(Mchezaji mmoja mmoja)..Pia Washambuliaji/wafungaji wanaweza kupatikana kwenye ligi hii yenye timu ndogo hizi...siyo lazima SMB, YNG na AZM.Hakuna anayezungumzia timu ya Taifa(Taifa stars).......Hiki ndicho kipindi ambacho kocha Poulsen alitakiwa kuwa anazunguka nchi nzima..Viwango vya FIFA tunazidi kuporomoka..ni yeye5Poulsen) wa kulaumiwa hakuna mwingine na hatutaki tena siasa hapo..Wakati wa Maximo tulikuwa "Heroes"(Washindi?) sasa tumekuwa "Zeroes"(Sifuri/Sufuri?)

    David V

    ReplyDelete
  2. Mbona matokeo ya Toto africa vs yanga hujatoa? Wadau tunataka kujua. Au Yanga imefungwa? Maana wewe nasikia ni mnazi mkubwa wa Yanga.

    ReplyDelete
  3. Jamani hii nembo ya TFF inatakiwa ifanyiwe ukarabati. Yaani imekaa vibaya mno na kuifanya TFF kuonekana soooo cheappp....Please someone do something to improve this nembo...!!

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza acha uongo, Maximo ndiyo hovyo kabisa, alituharibia soka letu,wakati wake hata unbingwa wa
    afrika Mashariki hatukuwahi kuuchukua!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...