Baadhi ya wachezaji wa timu ya soka ya Tanzania All stars inayoundwa na wachezaji nyota wa zamani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazoezi jana jioni Leaders Club jijini Dar es salaam wakijiandaa kwa safari ya Mombasa leo ambapo watakwenda kucheza na Kenya All stars. Aliyechuchumaa mbele ni kiongozi wa msafara Kitwana Manara Popat ambapo kulia kwake ni Mohamed Hussein 'Mmachinga' na kushoto kwake ni Mohamed Mkweche, Omar Gumbo, Nyuma  ni pamoja na Mohamed Hussein 'Keegan), James Washokera, David Mwakalebela, Hamisi Soda,  Dotto Mokili na wengineo. Wakiwa Mombasa watacheza na Kenya All Stars ya akina Odhiambo Gor, Joe Kadenge, Mahmoud Abbas 'Kenya One, Allan Thigo na wengineo. Hii ni moja ya shughuli za Tanzania All Stars Foundation, taasisi iliyoundwa kushughulikia wacheza soka wa zamani ambapo huwasaidia kuwaweka pamoja na kutoa huduma za kiafya na kijamii.

 All Stars toka shoto Nyanda toka Zanzibar, mbele ni Mohamed Hussein Mmachinga, James Washokera na Mohamed Mkweche. Nyuma ni Mohamed Hussein 'Keegan' na David Mwakalebela
 Nyuma kulia kaongezeka Bakari Malima 'Jembe Ulaya'
Kikao cha All stars

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ok! wana bima lakini?! isijewekwa msaada tutani hapa ohhoooooo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...