Fikiri, matumizi nyumbani: chakula, umeme, gesi, maji, soda/juisi za wageni. Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu. Matibabu hospitalini, pesa ya walinzi kwa mwezi, sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya; Zaka ya kanisani na misikitini, Kupanda Mbegu/ Sadaka, Shukurani ya Neno, Tozo za Flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzit...upa hapo hapo), Madalali wa nyumba/viwanja, Pango la nyumba, Fremu ya biashara/ofisi, Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers]; Mafuta ya gari Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa); Tozo za kuegesha magari, Makato ya Mikopo, Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf. 


Rambirambi ya mfiwa mtaani kwetu, Harusi ya ndugu yako wa ukoo na zawadi, Sendoff ya mtoto wa mdogo wake rafiki yako na zawadi, Kumuaga mfanyakazi mwenzetu na zawadi, Michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara; Michango ya besdei party na zawadi; Ndugu wa kule kijijini, Mshahara wa Hausigeli na hausiboi; Bodaboda, teksi na bajaj; Duka la dawa, Tuisheni ya mtoto, Kuchangia wahanga wa mabomu na mafuriko. 


Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa, Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu. Chakula cha mbwa, Machango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa, Kuchangia Uinjilisti Masasi, outing ya kitimoto, Ujenzi wa Nyumba Mabwepande, Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa). Na kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi. Maji ya Traffik, Chai ya Nesi na Daktari, Kahawa ya Hakimu, Karani na PP. 


Vishoka waunganisha maji na umeme; Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa. Hivi hali inakuwaje? Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba, kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni. umeme uliopanda bei, gesi iliyopanda bei, maji yaliyoadimika, bado contingency mana huu usafiri unaotembelea ball joint, bush, feni belt havijaf - hapo bado service. Bado msosi wa mchana kazini esp kama maofisi yetu mama ntilie wanakaribiana bei za restaurants, bado mchango wa kitchen pati na sare, baby shower. Na hapo bado hujatoa watoto outing jumapili n.k 
Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above 19%. Ndipo unapoimba "Mwokozi nitoe roho niepuke na hili balaaa" 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. baba maisha ni magumu kupita maelezo na serikali haijali na wala kufanya lolote kupunguza,cha kufanya ni kukwepa baadhi ya michango isiyo ya lazima.la sivo utakuta unaishia kula tu bila ya kufanya lolote la maana.

    ReplyDelete
  2. duh hayo yooote ulosema ni kweli> MUNGU NDO MTOAJI RIZKI KWA KILA MTU

    ReplyDelete
  3. Yaani wewe ni noma umesahau tu condom na guest na kuhong nyumba ndogo

    ReplyDelete
  4. Umefika mbali sana mwisho wa cku cc watanzania wote nahubutu kusema cc ni wezi cause vyanzo vyetu vya vipato sio rasmi.

    ReplyDelete
  5. .....Duh its a miracle tunaishi.. Glory Be To God...!

    ReplyDelete
  6. SULUHISHO LA KUIMUDU HALI HALISI:

    Ili kukabiliana na wimbi zito la Maisha ni muhimu kuishi 'economic life' /maisha ya kiuchumi zaidi.

    Pana kitu AVAILABLE RESOURCES,(AGAINST)-Choice, Preference and opportunity costs with sacrifice costs./....Pana KILICHOPO YAANI UWEZO AU NGUVU ILIYOPO (DHIDI YA)-Chaguo,Kipaumbele uwezekano wa kupata, na kujitoa mhanga.

    Panga vitu kwa Vipaumbele ukianzia na vyenye umuhimu zaidi na kushuka chini, kwa kwa kanuni za kiuchumi daima ni vile huwezi timiza kila kitu ktk maisha yako.

    MFANO:
    1-Chakula
    2-Mavazi
    3-Pango la nyumba, bili za umeme,maji na makazi
    4-Shughuli/Kazini/Fremu/internet kwa kazi
    5-Matibabu/Hospitali
    6-Elimu kwa watoto shuleni
    7-Misiba/MAMBO YA IMANI YA DINI
    8-Harusi,
    9-Bar/ Pub na Ulevi..washikaji
    10-Juisi /soda za wageni
    11-Mizinga vijiweni, Ma dogo njiani
    12-Vipaimara na komunio
    13-Mlinzi nyumbani
    14-Vishoka,
    15-Rushwa
    16-Waosha vioo ktk foleni
    17-Bodaboda
    18-Uzinduzi wa Kwaya
    19-Mama Ntilie mchana/restaurant
    N.K

    Kanuni kuu ya Maisha ya kichumi ni 'Uwezekano kwa kilichopo na kujibana kadiri iwezekanovyo' hasa kwa Bajeti.

    Sasa kwa msingi huo utatumia kanuni hapo juu utachagua vipaumbele kuanzia juu mfano kama unamudu 12 vya juu achana navyo kuanzia 13-19, au ukimudu 7 vya kuanzia juu achana na 8-19

    ReplyDelete
  7. Jamani kweli kuna watu wanaupeo wa kufikiri hivi vitu sijawahi kuvifikiri hata siku moja pamoja na kwamba niko nje ya nchi ila badoo jinamizi hilo nakumbana nalo yaani linanifuata hukuhuku kama vile niko bongo mpaka sometimes nawaza sijui nibadili namba ya simu ili niwapotezee wahusika?!. Na kwakuongezea tu kwasie tulio nje ya nchi ni KODI TUNAZOPIGWA KILA KONA TUNAYOENDA,KUOMBWAOMBWA MSAADA WA KUNUNUA SIMU TENA ZA BEI MBAYA NA WANANDUGU AU MARAFIKI,PERFUME, LAPTOP, IPAD, PLAYSTATION,PSP, IPHONE, NGUO, VIATU MARA NITAFUTIE GARI NITAKURUDISHIA HELA YAKO POLEPOLE YAANI SIO SIRI INAFIKA SEHEMU UNASEMA SIJUI NIJINYONGE NIEPUKE HILI BALAA!Na huwa najiuliza WATANZANIA TUMEKUWA WAVIVU WA KUFIKIRI, KWELI KUNA VITU HAVINA UMUHIMU KABISA KWANINI TUSIACHANE NAVYO KUKATA COST? HATA MWINGEREZA ANAKWAMBIA SPENDING CUTS NA HIYO NI KUTOKA SERIKALINI UTARATIBU HUO UPO MPAKA MAJUMBANI .NDUGU JAMAA NA MARAFIKI TUTIE MOYO KWA KUTUSHAURI VITU VYA MAANA NA SIO KUTULILIA SHIDA MNATUCHANGANYA JAMANI LOO!

    ReplyDelete
  8. Sasa ndugu, Mwokozi akiitwaa hiyo roho yako nahiyo timu yako nani unamwachia?
    Mwokozi hataitoa roho yako cha moto utakipata hahahaha

    ReplyDelete
  9. Kwa ujumla maisha bora kwa kila mtanzania yamekwama, Hiyo bajeti ni ya wachache wenyenazo.Mtanzania wa kawaida ni kama mfungwa ndani ya nchi yake.

    ReplyDelete
  10. Nashukuru sana ndugu yangu hapo umegusa kila pembe ya maisha hapa duniani na ni ukweli mtupu usiopingika. Je tufanye nini ili kukabiliana na hiyo hali ngumu ya maisha? kwangu mimi sifikirii kwamba kifo ndiyo solution.

    ReplyDelete
  11. Du! nimesoma hii taarifa naona mambo kibao nachanganyikiwa tu kufika hapo mwisha loh! Lakini wapo wanaoyaweza kuyatimiza hayo yote uliyoyataja, kwani watu husema vidole havilingani.

    ReplyDelete
  12. haya ni matokeo ya UONGO-zi Bora na SI(h)ASA Bora tulizonazo Bongo!
    lakini Ankel kale kachama ketu kaleee kanasema mambo ni swali na tumefanikiwa sana!!

    yaani mpaka tulipofika hapa Mungu anatupenda sana!

    ReplyDelete
  13. I feel your pain!!!!

    ReplyDelete
  14. na usipo fuata staili ya maisha hayo, kuna social pressure.

    aidha kata matumizi mpaka vibaki vitu 5 tuu au kila ukisali ongezea uletewe mtoa roho pia baada ya sala.

    ReplyDelete
  15. Kuna mkurugenzi mmoja , alipofika hapa toka Ulaya, alihitaji kujua matumizi ya mfanyakzi, kwani aliona mshahara wanaolippwa hautoshi,....
    Alipewa yale ya wastani tu,akashangaa na kujiuliza,
    'Mbona huyu mfanyaakzi yupo hapa kuanzia asubuhi mpaka jioni, ...anapatia wapi pesa za ziada kuziba hili pengo,maana mshahara anaopata hautoshi kabisa, hata nusu ya gharama ..?' akauliza.
    'Hivyo hivyo, tumezoea haya maisha....'akasema meneja utawala.
    'Hapana, vinginevyo kuna hali ya inayoenndeela hapa, ...lazima kutakuwa na wizi..'akasema na akaitisha ukaguzi wa mahesabu, na ulipofanywa hakukuonekana wizi wowote..

    'Oh, kwa mataji huu, Wafanyakazi wengi ni wezi, lakini sijui wapi wanaiba...'akasema.

    ReplyDelete
  16. Hayo ni matumizi. Je kuna yaliyolizima? Marehemu Baba yangu aliweza kumiliki nyumba na usafiri wake ulikuwa wa baiskeli. Chakula chetu kilikuwa kina vyakula muhimu kwa binadamu. Tulikuwa tunafuga kuku wa kienyeji kwa hivyo siku za iddi na akija mgeni nakamata mmoja na kuchinja. Samaki tunanunua siku za bamvua. Nguo zetu tunashonewa na fundi cherehani. Viatu tunapata mwaka mara moja. Nilikuwa muda mwingi natembea miguu chini hado form II. Dawa yangu ya meno ilikuwa mkaa. Tulikuwa pia na heka tatu tukilima wiki-end kwa vyakula kama ndizi na mihogo. Pia tulikuwa tunamiliki ng'ombe watano ambao hupata maziwa na pia huchinjwa wakati wa harusi na sherehe.

    ReplyDelete
  17. inaonekana kulikuwa na mpango wa kuwapunguza chadema bungeni.

    Plan A washambuliwe kwa mapanga.

    Plan B Mahakama iwamalize.

    Hii itakuwa ni Plan B

    ReplyDelete
  18. na hapo ukute mshahara wenyewe laki mbili! Kwa staili hiyo wizi hauishi makazini!!

    ReplyDelete
  19. na hapo ukute mshahara wenyewe laki mbili! Kwa staili hiyo wizi hauishi makazini!!

    ReplyDelete
  20. Mbona umesahau mengi, mfano nunua mkaa lazima uwepo maana umeme hauna uhakika au gesi kuchemshia maharagwe inasumbua, watumie wazee chochote, watoto hawaja vaa, michango ya shule, nunua madaftari na kalamu, toa hela ya watoto ya kunywa maji mchana kila siku shuleni, toa michango ya ulinzi shirikishi, nunua sabuni za kufulia na kuogea, nunua incect killer/mosquito spray,nunua vyakula nyumbani, changia mchango wa chama cha ukoo, zawadi kwa mfanya kazi mwenzako kajaliwa mtoto, nunua luku, recharge dtsv/startimes,replace bulb energy saver imeungua, shuleni watoto wana study tour/graduation, nunua kitasa cha geti kimegoma kufunga,n.k, n.k, n.k.

    Mshahara ndio ule ule, hmna annual incremen, hamna annual promotion kazi nikupigana uswahili tu. mwajiri anakuwa na sababu kibao. Taifa letu lina vyanzo vingi vya mapato lakini tatizo halija jipanga vizuri. Wafanya biashara hawalipi kodi ni wachache wanalipa ipasavyo, wachache wanalipa asilimia kidogo tu ya kinacho takiwa. Ni aibu kubwa kusikia serilkali haina hela hata ya kuwalipa wafanya kazi mishahara yao. Mkapa alikusanya hela nyingi sana maana serikali yake ilikuwa imejipanga angalau vizuri kukusanya kodi na mabadiliko yakaonekana na inflation ikawa managed. Kuna haja ya kufuatilia ukusanyaji kodi na kupata mapato zaidi.

    ReplyDelete
  21. Chadema ni chama Makini sana. Nimefurahiswa na uamuzi wa kumweka WILBROAD SLAA kama Mgombea mpya wa jimbo la Arusha

    ReplyDelete
  22. Fanya kazi kama hutakufa siku za karibuni na uombe as if una dakika chache za kuishi

    ReplyDelete
  23. Hapa Makala inahusu Hali ya Maisha sio CHADEMA,,,NA KWA TAARIFA YENU JIMBO LA ARUSHA MJINI LINARUDI C.C.M MTAKE MSITAKE!

    HATA KAMA WATAKAA WATATU KWA MPIGO WAKISIMAMA KAMA MMOJA 1.Freeman Mbowe ,2.Zitto Kabwe,3.Dr.Wilbroad Slaa JIMBO LAZIMA LIENDE C.C.M!

    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!

    ReplyDelete
  24. Watanzania tunawaza matumizi tu, badala ya kufikiria upande muhimu kabisa wa kutafuta vyanzo vipya vya mapato. Tujikite zaidi kwenye kutengeza mapato then matumizi yatajiweka sawa yenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...