Abiria 35 na wafanyakazi wane wa ndege ya shirika la Ndege Tanzania (ATC) wamenusurika katika ajali ya ndege (pichani juu) iliyotokea asubuhi ya leo majira ya saa 4.15 katika uwanja wa ndege wa Kigoma.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya Kihenya  amesema aina ya ndege ni  Dash  8 Q 300  air tannia flight No. TC 119 iliyokuwa na abiria thelathinin na tano na staff wanne

Alisema ndege hiyo ilikuwa inatoka Kigoma kwenda Dar es salaam kupitia Tabora kabla ya kupata ajali baada ya kuteleza  na kuangukia ubavu wa kulia kutokana na  tope jingi lililokuwepo katika njia ya kurukia ya uwanja huo.

Abiria na wafanyakazi wote waliokuwamo waliweza kutoka katika ndege salama muda mchache baada ya jaribio lake la kupaa angani liliposhindikana.

Baadhi ya abiria waliohojiwa baada ya ajali wamewasifia sana rubani Emmanuel Mshana na msaidizi wake Mbwali Masesa kwa kujitahidi kuidhibiti kiuweledi ndege hiyo na kuokoa maisha ya watu.

Uchunguzi wa awali unaonesha bawa la kulia pamoja na injini ya propela ya upande huo vimeharibika vibaya.


Mmoja wa abiria walionusurika akiongea na wanahabari
Kaimu Kamnda wa Polisi mkoa wa Kigoma  SSP Kihenya Kihenya (kulia) akiwa eneo la tukiio na maafisa wengine.
Picha na Pardon Mbwate wa Jeshi la Polisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Laa haula wala kuwwata! Mwenyezi Mungu ni mkubwa.

    Poleni sana kwa matatizo na hongereni sana kwa kusalimika na ajali ya ndege.

    ReplyDelete
  2. poleni sana mlionusurika katika ajali hiyo na pia msisahau kumwomba na kumnshukuru MUNGU siku zote.

    swali langu ni je hao marubani pamoja na wahusika wengine wote hawakuona kua hali ya uwanja sio nzuri kwa ndege kupaa au kutua??

    mnaposema ajali imesababishwa na kuteleza kwa ndege kutokana na tope jingi katika njia ya kupaa inaonesha basi kulikua na uzembe to underestimate the situatuion before taking off.

    tuwe waangalifu zaidi

    ReplyDelete
  3. Poleni sana, lazima mumshukuru Mungu. M/Mungu akupeni maisha marefu na yenye amani na furaha.

    ReplyDelete
  4. Mi nafikiri Tanzania tusiruhusiwe kumiliki ndege hadi tutakapokuwa tayari vya kutosha. Nyie wazungu, msituuzie ndege, sisi bado wajima...eti matope uwanja wa ndege!

    ReplyDelete
  5. Kama hiyo ndege itakuwa haifai kutengenezwa, gharama ya kuweka lami ni nafuu kuliko hiyo ndege

    ReplyDelete
  6. NA HATUNA NDEGE NYINGINE....ILIKUWA HII TU

    DAVID V

    ReplyDelete
  7. Yaani hata Lori la kusafisha lami Airport Hakuna?

    Lakini Malori ya kurusha maji ya kuwasha yapo kila kona!

    ReplyDelete
  8. Ngombe wa masikini hazai akiza.............

    ReplyDelete
  9. Tumshukuru Mungu kwa kuwaepusha na sintofahau. Masikini Tanzania!!! Ama kweli ng'ombe wa masikini hazai.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...