Habari za Kazi Ankal,
 tafadhali twakuomba Tusaidie kupost hii kero ya umeme inayotukabili sie waTanzania wa Mbezi MaramaMawili.

Tuna wasilishakero hii hapa kwenu muweze kutupa mwongozo.sie wakazi wa Mbezi Maramba mawili tuna shida sana na umeme.tumeshaangaika sana kufatilia umeme tanesco ila wanatuhangusha sana.Wanzoni mwa mwaka 2008 tulienda kuomba umeme tukaambiwa mradi hauwezi kuja kwa sababu wakazi ni wachache, hapo tulikuwa wakazi zaidi ya 200.tukakubali mwakwaa 2010 tukaandika barua tena ya kuomba mradi tukanzungushwaa kweli kweli tukapewa kiswahili tu.


2011/2012 tukakusanyika tena na kamati yetu ya umeme tukafatilia Tanesco tukaambiwa tufatilie tanesco kituo cha Mbezi mwisho.Tumefatilia kweli hapo mwisho wa siku hatukupata jibu linaloeleweka.tukadanganywa kwamba nguzo zipo ila hawana transforme.

Sasa tupo wakazi zaidi ya 1500 tunaoishi Maramba mawilli stand ya basi mwisho.Umeme umeishia hapo Kifuru bjia ya kwenda Kinyerezi jirani kabisa na maramba mawili umbali wa 1KM na ukitokea mvezi umeme umeishia hapo msikitini umbali kidogo sana hata 1 Km haifiki.

Tumeenda Tanesco kuwaomba tujivutie hata huwo wa jirani zetu Kifulu au msikitini hapo lakini tunakataliwa na Tanesco wanatwambia umeme mdogo hautoshelezi.Tusubilie wa mradi ambao tumeombea toka mwaka 2008 adi leo hii 2012 hawajatuletea uwo mradi.

Maisha yamekuwa magumu sana kwa kukosa nishati ya umeme.matukio ya ujambazi yameongezeka kwa sababu ya Giza.Ukifika saa2 kupita njiani kuelekea Kinyerezi hatuwezi tunaogopa majambazi wanatumia mwanya wa Giza kufanya uhalifu.MBunge wetu John Mnyika taarifa tumeshakupatia ila hukuweza kuja hata kutusikiliza.Diwani wetu hata hatukufahamu sasa sie wananchi nani wa kutusaidi.
Mwenyekiti serikali za mtaa nae kazi imemshinda anakesi kila siku na wananchi wapenda maendeleo hatuna pa kukimbilie tumetengwa na serikali yetu. Miaka 50 ya uhuru lakini sie tupo gizani hadi leo hii.

Tunaomba wahusika wa Tanesco watusaidi kutufikishia huduma hii ya umeme tafadhali. 

Wakazi wa Maramba Mawili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni sana kwa adha mnayoipata. Nawashauri mumwandikie Mkuu wa Tanesco au tuma ujumbe kwenye E-mail yake: william.mhando@tanesco.co.tz;

    Kila la heri. Ichube

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...