Wanafunzi wa Wanasoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) walipowasili katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Milembe iliyopo Dodoma kwaajili ya Kuwatembelea na Kukabidhi misaada yenye thamani ya Jumla ya Shiling aki tano na nusu.
Home
Unlabelled
WANAFUNZI WA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOMSSO) WATEMBELEA HOSPITALI YA WAGONJWA WA AKILI YA MILEMBE NA KUKABIDHI MSAADA WENYE THAMANI YA SHILINGI LAKI TANO NA NUSU LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Bongo raha sana, natamani ningesoma chuo nyumbani na kujuana na wenzangu tunaosoma kozi moja na kurahisisha usomaji na uelewa. hizi tabia za hawa jamaa kuchagua masomo unakuta darasa zima kozi tofauti wala mda wa kufahamiana na wenzako huna, kila darasa unaloingia sura tofauti ya itakapofika muhula mwingine unakutana na watu tofauti tena.. acha tuwe na upendo na ushikamano hata kama bado tu nchi masikini
ReplyDeletekumbe hili swala la kujipangia ratiba huku nchi za wageni linatugusa wengi
ReplyDeleteWewe mchangiaji wa kwanza uko sahihi. Lakini ni kwa degree programs kama hii ya hawa walioenda kutoa zawadi na nyingine za 'arts'. Lakini kwa programs za sayansi, elimu ya bongo iko nyuma hatua 1 000 000 000 000 000, kulinganisha na elimu ya vyuo bora duniani. Kwa hiyo kwa sayansi ukisoma bongo utafurahia kuchat na marafiki, na baada ya miaka yako unapewa cheti bila kuwa na ujuzi.
ReplyDeleteMimi nina experience na hili, kuna wanafunzi wa Ph.D toka engineering UDSM walikuja Sweden kwa ajili ya kufanya course ili kuwaongezea uelewa wa topic zao za research. Course zenyewe zilikuwa za masters. Kwa hiyo walifundishwa pamoja na wanafunzi wa masters, lakini hakuna aliyefaulu hata course moja kati ya tatu walizochukuwa (walipata chini ya alama 15 kwa 48). Sasa hao kwa sasa ni madaktari (Ph.D holders). Ikiwa uwezo wao uko chini ya level ya masters kwa hapa Sweden, unategemea watampa ujuzi gani mwanafunzi wa kitanzania??