Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania sasa wanaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha katika matumizi ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaposafiri katika nchi tisa za Afrika ambapo Vodacom na wabia wake kibiashara wanatoa huduma.

Nchi hizo na mitandao ya makampuni ya simu katika mabano ni Afrika Kusini (Vodacom), Msumbiji (Vodacom),Lesotho (Vodacom), DRC Congo(Vodacom), Ghana(Vodafone), Kenya (Safaricom), Rwanda (MTN), Uganda (MTN), Uganda (UTL) na Burundi (UCOM).

Kupitia mitandao ya mawasiliano ya makampuni hayo mteja wa Vodacom Tanzania sasa anaweza kupokea simu BURE, kupokea BURE ujumbe mfupi wa maneno - SMS, kupiga simu na kutumia huduma za Intaneti kwa gharama nafuu anapokuwa safarini katika nchi hizo.

Akizungumzia huduma hiyo mpya ya Africa Roaming, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza amesema “Tunajua kwamba watu wanapenda kuwa katika mawasiliano wakati wote bila kujali kama yupo nyumbani Tanzania ama mapumzikoni Afrika Kusini, au katika safari ya kikazi nchini Ghana, bila kuwa na hofu ya gharama za kuunganishwa kimawasiliano safarini - roaming.”

“Tunachokizundua leo ni suluhisho kuwapa wateja wetu utulivu wa mawazo wanaposafiri” Gharama ya matumizi ya Intaneti kwa mteja anapokuwa safarini ni za juu kwa mitandao mingi ya ya simu, leo tunajivunia kuja na gharama nafuu za matumizi ya Intaneti pamoja na za simu na za ujumbe mfupi wa maneno – SMS pindi mteja anapokuwa safarini katika moja ya nchi zilizo katika huduma hii ya African Family.” Aliongeza Bw. Meza

“Huduma hii pamoja na nyenginezo nyingi ambazo Vodacom Tanzania imezizindua hapo kabla zote ni katika kutimiza ahadi yetu ya kubakia kuwa mtandao bora zaidi wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi hapa nchini. Wateja wetu watarajie mengi mazuri zaidi kutoka kwetu katika wiki na hata miezi ijayo.” Amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza

Kwa maelezo zaidi kuhusu Africa Roaming mteja wa Vodacom Tanzania anaweza kutembelea www.vodacom.co.tz/africaroamingill

Wateja wa Vodacom wa malipo ya baada na wa malipo ya kabla wote wanaweza kupokea simu BURE, kupiga na kuperuzi katika Intaneti kwa gharama nafuu wanapokuwa safarini katika nchi ambazo mitandao yake ya mawasiliano imejumuishwa katika huduma hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Help us to connect MTN Swaziland. it is one of the notorious network in Africa as it makes our life difficult whila in Swaliland.

    ReplyDelete
  2. Mimi nafurahi kwa hili maana hivi majuzi nilikuwa Mombasa just next to Tanzania lakini Vodacom ilikuwa haifanyi kazi kabisa. Ukijaribu kupiga, Safaricom walikuwa wanatuma ujumbe unaosema kuwa wameshindwa kuchaji..Afrika bado tuna changamoto ya kuimarisha miundo mbinu ya mawasiliano. Thnx Vodacom if this is an active services.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...