NA MERY AYO,ARUSHA

Jumla ya watoto 1500 kutoka nchi saba za bara la afrika wamefanikiwa kupewa chanjo ya majaribio ya malaria ambapo lengo halisi ni kupunguza idadi ya vifo vya malaria

Kauli hiyo imetolewa Mjini Arusha na Dkt John peter Lusingu kutoka katika kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu kwa mkoa wa tanga(NIMR) mapema leo jijini hapa

Bw Peter alisema kuwa watoto hao walifanikiwa kupewa chanjo hiyo kwa maeneo tofautitofauti kwa bara la afrika kuanzia mwaka 2010 ambapo mpaka sasa hakuna madhara ya aina yoyote ile

‘tunasubiri shirika la afya ulimwenguni liweze kudhibitisha juu ya chanjo hii ya majaribio kwa watoto lakini kama itaenda vema basio itaweza kusaidia sana hasa kwa kujikinga dhidi ya malaria’aliongeza Bw peter
Akielezea hali ya gonjwa hilo hapa nchini alisema kuwa kasi yake imepungua kwa kiwango kikubwa sana lakini bado kuna mikoa mitano ambayo bado inaongoza huku kwa upande wa Tanzania visiwani kasi ya gonjwa hilo ikiwa ,ni ndogo sana.

Alitaja mikoa ambayo inaongoza kuwa ni pamoja na mikoa ya Kagera,Pwani,Lindi, kigoma na Tanga kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Pia alisema kuwa hata idadi ya vifo vinavyotokana na Malaria nayo imepungua sana kwa kuwa kwa miaka ya nyuma zaidi ya watu milioni moja walikuwa wanakufa kwa mwaka wakati kwa sasa wanaokufa ni watu watu kama laki sita sawa n ungufu wa asilimia 50.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...