Ndugu Michuzi.,

Nimesoma hoja ya huyu mdau aliyetoa maoni yake na mimi nimeguswa sana nitoe maoni yangu na pia ningeomba ufanye hii mada kuwa kubwa zaidi watanzania wengi wajue thamani ya uhai.

Nilisafiri na basi la Ngorika mwezi Januari, Michuzi kusema ukweli mabasi ya hii kampuni watu wengi wanaamini hua mmiliki wake ni kigogo wa jeshi la polisi., hili halihitaji ushahidi sana manake hii kampuni inajulikana kwa kuwa na mabasi yanayoendeshwa kwa rafu barabarani na kwa speed kubwa.

Nilikua naelekea Tanga kutokea Moshi na basi la ngorika na hili nilipanda tuu kutokana na kukosa basi jingine na usafiri ulikua wa shida siku hiyo. Kusema ukweli niliona kitu cha ajabu sana, basi lilipakia abiria wengi wa kusimama, wengi idadi karibia sawa na abiria waliokaa, polisi walisimamisha pale Mwanga na kujifanya kama hawajaona chochote cha ajabu ndani, mbaya zaidi dereva akaanza kukimbiza gari kwa mwendo wa ajabu kama speed 120 hivi au zaidi na njiani anakwepa mashimo kwa mbwembwe......... mimi mwenyewe nilikua nimekaa nyuma nikashangaa abiria waliokua mbele mbona hawamwambii dereva apunguze mwendo?..... nilianza kupiga kelele japo sikusikika sababu watu ni wengi na hakuna pa kukanyaga kwenda mbele, abiria waliokua kwenye basi wachache wakani-support lakini wengi hawakuona kama kuna tatizo, baadae nikahamua kupiga simu polisi lakini mawasiliano yakawa si mazuri, Nashukuru mungu tulipofika Hedaru polisi alisimamisha nikamwita polisi dirishani na kumwambia apande aingie ndani ajionee mwenyewe na kwa kumtisha polisi nikamwambia nimeshawasiliana na trafic makao makuu kwahiyo anatakiwa achukue hatua.

Michuzi story ni ndefu ila kwa kifupi watanzania tujaribu kuthamini maisha yetu, tuache kuishi kwa matumaini eti ajali ikitokea ni mipango ya Mungu. Huu ni uvivu wa mawazo na tusimsingizie Mungu, uwezo wa kuzuia ajali upo mikononi mwetu abiria, hua ajali zinapotokea ninaonaga waandishi wakiuliza majeruhi hospitalini kua chanzo cha ajali ni nini na hapa utamsikia abiria majeruhi akiwa analalamika dereva alikua anaendesha mwendo wa kasi. 

Naomba waandishi wote wa habari mnapowahoji majeruhi na kuwauliza hili swali pia muwaulize walichukua hatua gani walipoona dereva anaendesha kwa kasi?..... kwanini tunakubali kuweka roho zetu rehani kwa madereva wazembe kwa kisingizio tunataka kuwahi au kwa kumwonea huruma dereva?, pia kuna abiria unakuta wanamtetea dereva utadhani wana hisa kwenye hizo kampuni wanasahau kua UHAI HAUJI MARA MBILI na pia huruma zetu za kinafiki hazirudishi uzima ulemavu uliotokana na ajali ambayo tulikua na uwezo wa kuizuia.

Ningekua ninamamlaka ningefanya kifuatacho kupunguza ajali:

Ningehakikisha vituo vyote vya polisi njia kuu za mabasi kuelekea mikoani vinajulikana kwa abiria na nyuma ya tiketi za mabasi yote ya mikoani kunakua na majina ya hivi vituo na namba za simu za mkuu wa hicho kituo ili abiria waweze kuripoti mapema kabla ya ajali wanapoona dereva anaendesha kwa uzembe. Pia ningefanya hizi namba kuwa special na ziwe zinarekodiwa ili inapotokea ajali kwa kesi ambayo imesharipotiwa askari aliyekua zamu au mkuu wa hicho kituo awajibishwe.

Mdau,
Globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2012

    yaani wewe ulieandika post hii unaonekana umetoka nje ya nchi hii. unataka abiria wapige simu wapi? na hizo simu zirecordiwe? hiyo ni third world almost forth huyo abiria itabidi ahonge ili polisi afanye kazi yake. uzembe wote huo unaletwa na leseni zisizo na thamani unaweza kumiliki hiyo leseni kwa glasi ya bia hawaigi mifano kutoka nchi zingine. sector zote big selfish tutafika lini?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2012

    Mdau uliyetoa mada. Kuhusu mmiliki wa kampuni hii ya Ngorika, ni vyema ukafanya utafiti zaidi ili ujue nani wamiliki wake. Kifupi na kampuni hii inamilikiwa na familia ya marehemu (RIP)mzee Mberesero na si kigogo wa Polisi kama ulivyo dai. Kwa hilo hakuna asiye jua. Kuhusu mwendo kasi wa magari haya hilo sina ubishi nalo kwani mabasi yote hapa Tanzania mwendo kasi ndiyo kawaida yao. Kibaya zaidi ni kwamba hata abiria wanaosafiri hawajali kabisa. Na wakisika mtu analalamika wanamshangaa. Hao Polisi wa usalama barabarani ndio usiseme. Wanadiriki kuwaambia madereva "MBONA LEO UMECHELEWA VIPI"? Huu umekuwa ugonjwa na dawa yake ni kuweka hukumu ya kifo pale dereva anaposababisha ajali. Nadhani itasaidia kwa kiasi kikubwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2012

    wewe uliyeponda mtoa maada na kusema leseni ni gharama ya bia 1, wewe ndo wale abiria ambao wanaogopa kumwambia dereva apunguze mwendo lakin ajali ikitokea na yeye akibahatika kupata ajali bila kufa, akiulizwa na mwandishi chanzo cha ajali anasema uzembe wa dereva...kila kitu kinawezekana bwana kikiamuliwa na sio kukatishana tamaa...wewe n mzembe wa kufikiri nadhani na upeo wakoni mdogo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2012

    Nimefurahi kuona mdau anaendeleza swala la Usafiri. napenda nimpongeze. nimefurahi kusikia maoni ya anonymous 12:15 kwani yanawakilisha hisia za watu wengi kwasababu ni ukweli kuwa mabasi/biashara ni za vigogo au watu wanahusika na vigogo wenye pesa na SERIKALI NA SIASA YETU inakumbatia WENYE PESA. Kwa hiyo masikini askari akipeleka kesi hiyo mbele anaambiwa aiache. ni vigumu kutekeleza sheria. kwa misingi hiyo nashauri kuwa tuendelee kupiga makelele na tutakapokuwa wengi pasi tutaweza kuleta mabadiliko.

    aluta continua

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2012

    Kukalipia upuuzi huu wa madereva ni muhimu ni sehemu ya kuelimisha Umma utambue haki zao za kuishi hata kama serikali yenyewe haitilii maanani.Kwa kweli Nidhamu Bongo hakuna hasa kwa Watawala,sasa kama watawala hawana nidhamu hata waliochini yao hawatakuwa na nidhamu.Vifo vya kipuuzi vya barabarani havikuanza leo na hii kutokana na Rushwa kutawala.Kingine ilipo tokea ajali Wami ya aliyekuwa waziri Mkuu sokoine binafsi nilitarajia mwaka 1984 ijengwe hospitali kama kumbukumbu ikajengwa kambi ya vijana,hospitali katika njia kuu ni muhimu kwa huduma ya kwanza kwa majeruhi.Watawala jengeni vitu vitakavyo Okoa na Kunusuru maisha sio kambi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2012

    Mdau mleta mada,
    Kwakweli nakushukuru kwa ujasiri wako na upevu wako wa kimawazo.
    Yawezekana kweli (kama anony hapo juu alivyocoment) kurekodi simu na kuwajibisha mapolisi husika ikawa ngumu kufanyika. Lakini hii haizuii abiria kusimamia haki zao. Bado mteja ni mfalme (usipopanda hayo mabasi hawatapa biashara), abiria wakisimama kwa umoja na kumkanya dereva anaeendesha vibaya nina hakika tutaanza kuona mabadiliko bararani sio tu kwa mabasi ya safari ndefu bali hata madaladala.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 01, 2012

    Serikali nayo pia ni chanzo cha yote hayo. Kwa nini haishugulikii miundo mbinu ya reli. Watu wachgue njia bora ya usafiri. watu wanalazimika kupanda mabasi pasipo kutaka

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 01, 2012

    Huyo aliyeongelea Reli nampa tano.Kuna reli iko hapo kutoka Tanga hadi moshi imeanza kuota hata nyasi..Kwanini isitumike hii kwa treni za abiria za kisasa.Serikali please.Badala ya kujazana kwenye hizo ngorika reli hii ingesaidia sana sana.Tena kuanzia Dar hadi Moshi.Reli hii haitumiki sana/haitumiki kabisa?

    David V

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2012

    Haya matatizo hayawezi kuisha kama serikali hawawezi kutafuta mbinu ya kuzitatua.Na sijui kama kweli wapo siriasi kwakuwa hawa maaskari wadogo hawana nia ktk mioyo yao na kinachofanyika ni rushwa huku jamii inateketea.

    Wazo langu;
    1-Polisi wapewe vifaa vya kileo ili kuweza kuwakamata madereva wanaokiuka sheria.
    2Polisi waweke kitengo maalum na watoe namba za simu na ziwekwe waziwazi ili abiria wakiona hali isiokuwa ya kawaida wapige simu moja kwa moja na watoe namba ya gari na jina la gari ili ikifika ktk kituo cha mabasi lisimamishwe na kama anamakosa watozwe faini tena ya kukomesha yaani asirudie tena.
    3-Viwekwe vituo visiopungua 5 au 6 vya kurekodi muda kwa kila basi na kama amefika kabla ya muda aliopangiwa alipishwe faini isiyopungua 500,000.
    4-Na kama basi litasababisha au litafanya ajali kimakosa;
    a)Dereva kama yupo hai ashitakiwe na aende jela miaka isiyopungua 30 kulingana na kesi yenyewe hadi maisha kama ameua.
    b)Mwenye basi afungiwe leseni ya biashara kwa muda wa miaka 2 ili ajue kufuatilia madereva wake na utendaji wao wa kazi na ajue kutafuta madereva walio makini hasa umri pia unachangia matatizo kama dereva bado anaumri mdogo.
    5-Abiria nao wanatakiwa wawe na umoja ktk hili kama alivosema Mdau kwamba kajitokeza kukemea lakini anajikuta peke yake au wachache huku wengine utakuta wanakenua na kukuona kama fala.

    ReplyDelete
  10. MwamatandalaMay 01, 2012

    Mimi na wazo tofauti kidogo na wenzangu waliotangulia,nimeona Lusaka sheria zinafuatwa,Botswana vile vile zinafuatwa sijui kwa nini Tz hatuwezi?Wazo langu ni kuyatumia makampuni ya simu za mkononi kubuni mbinu za kupata taarifa za mwendo kasi kwa mabasi ya abiria kupitia ujumbe wanaopata toka kwa abiria.kwa hiyo abiria unapotaka kusafiri unatuma hiyo msg na kupata wastani wa mwendo kasi wa mabasi husika,hii itapunguza biashara kwa mabasi yanayoenda kasi.Jeshi letu limeshindwa kazi kwa hiyo wasafiri lazima tubuni njia zetu za kulinda usalama wetu.Ahsante

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2012

    Mdau aliyeleta suala la Reli ameleta hoja ya maana sana lakini tatizo ni Watawala wameliuwa Shirika la Reli makusudi ili mabasi yao yapate biashara.Na pia wameuwa Shirika lilokuwa limeajiri Watanzania wengi Nchini,leo hii Mikoa ya Tanga,Moshi na Arusha imeathirika.Kwa taarifa Kenya wanaazisha Bandari Lamu na Reli,ambayo itatoa ajira kwa watu wao wakati sisi Reli na Bandari tunazo Tanga kinachotakiwa ni kizifufua lakini Watawala wanacheza Ndobolo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...