Rais mpya wa Shirikishio la Riadha Tanzania ( RT), Antony Mtaka ambaye ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro ( aliyesimama ) akitoa hotuba yake ya shukrani kwa wajumbe wa Shirikisho hilo, Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ( wapili kutoka kushoto) kwa kumchangua kwa kura za kishindo pamoja na safu yake ya uongozi mpya baada ya kushinda mpinzani wake Kanali Mstaafu Juma Ikangaa , uchaguzi huo ulifanyika juzi (Mei 20) Mjini Morogoro.
Rais mpya wa Shirikishio la Riadha Tanzania ( RT), Antony Mtaka ambaye ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro ( aliyeshika ua) akipongezwa na baadhi ya wajumbe waliochaguliwa wa Shirikisho hilo juzi ( Mei 20) wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Mjini Morogoro ( aliyekaa kulia) ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) Dioniz Malinzi.
Rais mpya wa Shirikishio la Riadha Tanzania ( RT), Antony Mtaka ambaye ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro akipongezana na aliyekuwa mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo, Kanali mstaafu Juma Ikangaa ( wenye suti ) baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu na washindi wa nafasi mbalimbali kupatikana , uchaguzi huo ulifanyika juzi ( Mei 20) Mjini Morogoro.
Kanali Mstaafu Juma Ikangaa ( wa kwanza kulia) akifuatilia matangazo ya matokeao ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania ( RT) uliofanyika Mei 20, mwaka huu mjini Morogoro, Ikangaa aligombea nafasi ya Rais wa RT na kushindwa dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka .
KATIBU MKUU WA RT, SULEIMAN NYAMBUI NA TABASAMU LA USHINDI.

( Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2012

    Ndio maana tanzania hatuendelei kwenye michezo,badala ya kuchagua watu wanaojua nini kinahitajika ile tuwe na wanamichezo wa kimataifa kuwa viongozi,tunachagua alimradi tu..sasa huyu mtaka ni nani kwenye riadha?nani anamjua?amewahi kushiriki nini kutuletea sifa Tz kwenye riadha?anajua wapi pa kuanzia kuwatafutia wanariadha wetu wafadhili na mameneja wa kimataifa kama nchi zingine wafanyavyo?khaaaa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2012

    Mdau hapo juu acha hizo, kwahiyo kwa kuwa wewe biafsi humfahamu mteuliwa ndio kigezo kwamba riadha haitaendelea!!? Ina maana maeneo yote ambapo walioteuliwa wanafanya vizuri wewe unawafahamu??!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2012

    Hivi jamani kiongozi wa riadha lazima awe mtu anayejulikana? mi nadhani uwezo wa mtu kuongoza cha muhimu hapa ni management na si ukimbiaji? wewe unayehoji kuwa huyu ni nani ulitaka achaguliwe nani kama watu hawajitokezi kugombea nafasi? halafu nikuulize waliouwa riadha Tanzania ni kina nani? yaelekea hujafanya tafiti vizuri riadha yetu imefika hapo ilipo gonjwa na hao wanariadha ndiyo wamefikisha hapo japo wakati wao wakishinda uongozi haukuwa na wanariadha sasa lipi bora wakimbiaji wanafanya RT kuwa mradi wao au watawala ambao mwisho wa siku wanaongoza vema. shime watanzania tujitokeze kugombea nafasi mbalimbali hata katika vyama vingine kama netboli na kuacha kulalamika

    Deliwe

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2012

    HAPA FITINA TUPU !

    Hakuna nini wala nini, huyo Juma Ikangaa ni mtu kwa kweli ingebidi hata Uchaguzi wenyewe usifanyike ila yeye apewe nafasi hiyo moja kwa moja !

    Jamaa anastahili kwa sababu anazo rekodi (hata kama nchini hazipo huko nje kwa wanaojua zipo) ameshiriki mashindano mengi sana na ametutoa sana kimasomaso Watanzania!

    Sielewi huyo Mpinzani wake ktk Uchaguzi Ndg. Mtaka zaidi ya huo U-DC wake (tena alioupata mwezi huu) sina uhakika kama ana lolote ameshatuletea nchini !

    *****NAOMBA NUULIZE*****
    JUMA IKANGAA NAZO REKODI ALISHATULETEA MEDALI NA SIFA KIBAO.

    JE MHE.MTAKA ALISHAWAHI KUKIMBIA RIADHA WAPI?, ALISHAWAHI KUPATA REKODI YEYOTE (IPO WAPI REKODI YAKE?) WALA HAJAWAHI KUTULETEA MEDALI TANZANIA?

    Huyo DC anachotaka hapo sio kuleta maendeleo ya Riadha bali ni kujihakikishia mafao ya ziada zaidi ya Mshahara wake.

    KAMA MDAU MTOA MAONI WA KWANZA HAPO JUU ANAVYOSEMA NA MIMI NATOA MSISITIZO YA KUWA *****TUACHE FITINA***** NA TUCHAGUE VIONGOZI WETU KWA UWEZO NA VIGEZO ILI TUENDELEE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...