Mwanafunzi Mwenjuma M. Magalu aliyechaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wilayani Handeni akimuonesha mwandishi fomu ya kuitwa shulen
Mwenjuma M. Magalu (kulia) akiwa na Bibi yake nyumbani kwao Kijiji cha Msasa, wilayani Handen
Na Joachim Mushi, Handeni
LICHA ya Serikali kuliarifu Bunge la Tanzania kuwa wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba mwaka 2011 kutoka mikoa 12 tayari wamejiunga na kidato cha kwanza, imebainika bado kuna wanafunzi wameshindwa kujiunga na shule kutokana na kipato duni cha familia zao.
Mwenjuma M. Magalu aliyechaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wilayani Handeni ni miongoni mwa wanafunzi walioshindwa kujiunga na sekondari kutokana na mama yake kushindwa kumgharamia mahitaji ya shule.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni kijijini Msasa, wilayani Handeni, katika utafiti uliofanyika kwa ushirikiano na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), mama wa mtoto huyo Hadija Magalu aliyetelekezwa na mumewe kwa muda mrefu alisema ameshindwa kumsomesha mwanaye kutokana na kipato duni alichonacho.
Magalu alisema alipata taarifa za kufaulu kwa mwanae tangu Desemba 12, 2011 na kuanza kujikusanya taratibu lakini hadi muda wa kwenda shule ulipofika (Januari 9, 2012) alikuwa hajakamilisha baadhi ya vifaa vinavyohitajika shuleni vikiwemo fedha ya ada na michango mingine.
“Naweza kukuonesha hata baadhi ya vitu ambayo nilikuwa tayari nimenunua kama sare, kwanja na mahitaji mengine madogo madogo…aliyenikwamisha na kunivunja moyo ni babayake (baba wa mtoto), ambaye awali niliwasiliana naye kupitia kwa ndugu zake na kuahidi angenisaidia ada lakini hakufanya hivyo hadi muda wa kwenda shule ulipofika,” alisema Magalu.
Mume wa Magalu (jina tunalo) ametelekeza familia yake (watoto wanne) pamoja na mkewe kwa zaidi ya miaka minne sasa kwa kisingizio kwamba amekwenda nje ya Wilaya ya Handeni kutafuta maisha, huku mkewe akibaki akiangaikia familia hiyo.
“Tumekuwa tukisikia tu kwamba ameonekana kijiji fulani lakini ukifuatilia humpati, na mara nyingi anapowasiliana na ndugu zake ndio wanatupa taarifa zake…nami niliwasiliana naye mara ya mwisho nikimpata taarifa za mtoto kufaulu lakini hakutekeleza ahadi yoyote juu ya kunisaidia ada ya mtoto.
Michango iliyomkwamisha mwanafunzi Mwenjuma Magalu kujiunga na kidato cha kwanza ni ada ya sh. 20,000, fedha ya taaluma sh. 10,000, fedha ya madawati 15,000, fedha ya sweta sh.10,000, kitambulisho sh. 5,000, ulinzi sh. 5,000, tahadhari 5,000 pamoja na fedha kwa ajili ya nembo ya shule sh. 2,000.
Akihutubia Mkutano wa Saba wa Bunge la Tanzania lililomalizika hivi karibuni, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kutoka mikoa 12 ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mara, Morogoro, Mwanza, Lindi, Kilimanjaro, Pwani, Ruvuma na Tanga, wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba wamefanikiwa kujiunga na Kidato cha Kwanza.
Hata hivyo mwanafunzi Magalu kwa sasa anafanya vibarua kwa moja ya kampuni za Kichina zinazofanya ujenzi wa barabara inayopita Kijiji cha Msasa, kwa madai anatafuta fedha za ada na endapo akikamilisha atahakikisha anaendelea na elimu ya sekondari hapo baadae.
Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuzungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni, Hassan Mwachibuzi alisema ofisi yake haina taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na shule, hivyo kumshauri mwandishi amueleze mtoto huyo kufika ofisi za halmashauri ili aweze kujieleza na ikiwezekana kusaidiwa.
“Kama huyo mtoto yupo mwelekeze aje pale ofisini kuna wataalamu wa utambuzi watamuhoji na kuangalia namna ya kumsaidia…sisi hatuna taarifa hizo na huenda wahusika wanatuficha,” alisema kiongozi huyo.
*Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com) kwa kushirikiana na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA)
Katiba inasema ni haki ya kila Mtanzania kupata elimu lakini katiba haijaweka utaratibu unaoeleweka kwamba ni kwa vipi hiyo haki mtanzania ataipata. Kwa hiyo katiba haina kipengele cha mtu kuishtaki serikali kwa kutompatia mwananchi haki hiyo.
ReplyDeleteTubadilishe katiba ili iweke wazi kwamba haki ya elimu ni nani anapaswa kuitoa ili miaka ijayo kijana kama huyu aweze kuifungulia mashtaka mamlaka inayohusika kumpatia haki hiyo.
Inasikitisha! pengine akipata elimu ni Magufuli wa baadae, tunatakiwa tukipata matatizo kama haya, tuyaweke wazi kwa kila mtu tusione aibu wala kuwa mashujaa wa kutaka kuyatatua mwenyewe wakati uwezo huna
ReplyDeleteafadhali mambo kama haya yaletwe hadharani na ikiwezekana thehabari iwakusanye watoto wengi wa namna hiyo na kuelekea bungeni woote ili kujua hizo posho zao wanazokalia kila siku si msaada wowote kwa jamii. Akiwemo mmbunge aliyepigiwa kura na wazazi wa huyu kijana. Aibu kubwa saana sana kwa jamii maana hizo pesa ni nyingi kwa familia ilihali ni chache sana kwa viongozi wetu wanaosomesha watoto wao nje ya nchi na wao wenyewe kutibiwa nje ya nchi. Serikali iwajibishwe hasa maana viongozi wamelala na taifa la kesho linateketea.
ReplyDeleteWatu wanapenda kutumia umaskini kuchangisha michango. Hivi kwanini mama yake huyo mtoto haonekani kwenye picha? Aende ofisi husika, anapaswa asikataliwe kujiunga na shule hata kama hana ada.
ReplyDeleteWewe mwandishi ulimuuliza kama alienda shule akafukuzwa?
Ni aibu kubwa sana leo hii Tanzania mtoto anashindwa kujiunga na sekondari kwa ajili ya mahitaji yasiyozidi Tshs.100,000.00. Mzazi hana uwezo lakini je hapo kijijini hakuna watu walioenda shule kuweza kumshauri huyo mama aanzie wapi ili aweze kusaidiwa mwanae asome. Hapa ndio utaona blabla za viongozi wetu. Yaani serikali ya kijiji haina taarifa au uwezo wa kushauri njia gani itumike ili mtoto apate haki yake hiyo ya msingi....na ktk karne hii tunasema tuna uongozi wa vijiji!! Na walimu wa shule yake ya msingi je? Hawakuona umuhimu wa kutoa ushauri kwa mtoto waliyemfundisha kwa miaka saba na akafuata mafundisho yao na kufaulu ili njia gani afuate ili apate haki yake ya msingi kabisa....ama kweli elimu zetu hizi....Tubadilike!!
ReplyDeleteThis is a very sad story wakati mafisadi yanakula nchi na wananchi don't even have a cent to send kids to school. Where is that MP who had $1m in a foreign account? Shame on leaders, this should not be happening at all!!! How long wananchi wataendelea ku-suffer huku viongozi wetu wanaishi kifahari beyond their means.
ReplyDeleteMhariri naomba Kama ningepata mawasiliano na wazazi wa huyu mtoto ili mi na familia yangu tuweze kumsaidia aweze kuendelea na masomo.email yang ni adushariff@ hotmail.com.
ReplyDeleteShukran.
mh. kigoda mpiga kura wako huyo tafadhali naomba umsaidie
ReplyDeleteAcheni Jamani. Inatakiwa familia iseme inangapi na imepungukiwa na ngapi. Kila kitu serikali - kula yako, kuvaa, hata pahala pa kujisaidia na kuzoa taka ulizomwaga wewe mwenyewe serikali!!!
ReplyDeleteHakuna serikali ya namna hiyo duniani.
Watu wafanye kazi waache midomo.
Watu hawalipi kodi kila mtu anataka msamaha wa kodi, serikali itatoa wapi pesaaaaaa.
Watanzania jitihada inahitajika sana,
ReplyDeleteTuangalie tunalewa sana ktk Mabaa na Pubs huku tukifanya anasa za ajabu ambazo gharama yake ni kubwa kuliko ada anayotakiwa mtoto huyu ili aweze kuendelea na Masomo.
Tujitahidi kutuma michango kwa mambo kama haya.
Hapa ili kuwa na vitendo bila kuchelewa tunahitaji Namba ya M-Pesa ili watu wachange haraka iwezekanavyo!
Mbona serikali inayo pesa za kununua magari mazito kama land cruser n.k?Lakini pesa za kuwasomeshea wanafunzi hakuna!Si maajabu hayo?
ReplyDeleteNaona watu mnaongea irrelevant na shida. Michuzi wekeni bank info tumchangie.
ReplyDeleteadulshariff rahman akujaliye kila la kheri na baraka tele hapa duniani na kesho akhera wewe pamoja na family yako kwa kumsaidia huyu na mwinginewe Allah ma amin.
ReplyDeletetunahitaji mtu mwenye moyo kama wako na si kutoa comment tu katika blog hii shukran sana
mdau new york
michu nakusalimia bro