Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Balozi Khamisi S. Kagasheki (katikati) akizungumza kwenye mkutano wa kuzindua Bodi ya ushauri na wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ulifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara ya Maliasili na utalii.kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bibi. Ester Mkwizu akipokea vitendea kazi kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi Khamisi S. Kagasheki (katikati) huku Naibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu akitazama kwa umakini.
Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika picha ya pamoja na badhi ya wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania imezinduliwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi Khamisi S. Kagasheki.Uteuzi wa Bodi hiyo ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) tangu tarehe 1 Desemba 2011 hadi 30 Novemba 2014.
Uteuzi wa wajumbe 7 wa bodi hiyo mpya ulianza rasmi Desemba mosi 2011 baada ya Waziri kutumia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali kuunda Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
Bodi hiyo itaongozwa na Bibi. Ester Mkwizu kama Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakala wa Huduma za Misitu ni kama ifuatavyo:-
1. Bibi. Esther Mkwizu – Mwenyekiti, kutoka Sekta Binafsi (Tanzania Private Sector Foundation), Dar es Salaam;
2. Bibi. Gladness Mkamba - wa Wizara ya Maliasili na Utalii;
3. Eng. Bonaventura T. Baya – wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC);
4. Bw. Sosthenes Sambua - wa Dar es Salaam;
5. Prof. Yonika Ngaga - wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro;
6. Dkt. Himid Majamba - wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Sheria; na
7. Bw. Rawson Yonazi – wa Dar es Salaam.
Uteuzi wa Bodi hiyo ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) tangu tarehe 1 Desemba 2011 hadi 30 Novemba 2014.


.jpg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...