Flaviana Matata akikabidhi msaada wa maboya 500 kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Elias Makori kulia ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba, anayeshuhudia ni Meneja Masoko na Biashara wa Shirika la usafirishaji wa majini mkoani Mwanza la Marine Service,Kapten Obadia Nkongoki. Igoma jijini Mwanza.
flaviana na wageni wakiweka mashada kwenye makaburi ya waliofariki kwenye ajali hiyo Igoma Mwanza.
Waombolezaji wengine waliofiwa na ndugu zao wakiombea marehemu wa ajali hiyo.
Flaviana Matata akishindwa kujizuia na kuangua kilio wakati wa ibaada ya kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba alipotembelea baadhi ya makaburi ya watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo yaliyopi Igoma jijini Mwanza, katika ajali hiyo Flaviana alimpoteza pia mama yake mzazi.
Flaviana akionesha moja ya maboya yenye nembo ya foundation yake aliyokabidhi katika kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya MV Bukoba ikiwa ni kampeni yake ya kupunguza ajari za majini hapa nchini.
Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kuokolea maisha ya watu katika vyombo vya usafiri wa maji ambavyo vimelengwa maalum kwa Ziwa Victoria jijini Mwanza.
Msaada wa vifaa hivyo umeelekezwa katika shirika la kiserikali la usafiri wa maji jijini Mwanza lijulikanalo kama Marine Service Co. Ltd.
Flaviana Matata ametoa jumla ya vifaa hivyo 500 (vyombo vya kuokolea maisha ndani ya maji) ikiwa ni kumbukumbu ya ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba mnamo May 21 mwaka 1996 ambapo pia alimpoteza mama yake mzazi katika ajali hiyo iliyouwa watu takribani 1,000.
Sababu mojawapo kubwa iliyofanya watu kupoteza maisha yao siku ya tukio hilo ilikuwa upungufu na ukosefu wa vifaa vya kuokolea majini kama maboya (Live Vest).
‘Naamini kwamba, watu waliofariki katika ajali ya meli ya Mv Bukoba wengi walipoteza uhai wao kwa sababu walikosa vifaa vya kujikwamua ndani ya maji, hivyo ndo maana nimeamua leo katika kumbukumbu ya
kuzama kwa meli ya Mv Bukoba nije kutoa msaada wa vifaa hivi 500’ alieleza Flaviana Matata.
Vilevile akaongeza kuwa ni vyema vyombo vya majini vikawa na utaratibu wa kutoa elimu na maelekezo jinsi ya kutumia maboya endapo kutatokea tatizo kabla ya kuanza kwa safari kama wafanyavyo katika usafiri wa anga.







Positive energy...try to make the better world...God bless Flaviana...God bless Tanzania
ReplyDeleteMungu akubariki sana binti!
ReplyDeleteJamani na sisi watanzania ni hovyo sana huyo Flavia mbonza vazi laki halijaendana na tukio alilokuwa analifanya?
ReplyDeleteacha wenge wewe,kha!
DeleteWell done Flaviana. Asanta sana kwa msaada wako kwa taifa. Na sasa wapokeaji sio vifaa hivyo vikatumzwe store, ni kwa ajili ya matumiza, na viwe available na tayari kwa matumizi in case of accident, sio vionekane ila vikiwa vimefungiwa somethere.
ReplyDeleteOne again big up Flaviana. Mungu akubariki na akuzidishie.
Keep up the Good Work!
ReplyDeleteHongera na Pole sana Flaviana, Natamani ningeweza kupata nafasi ya kuifanyia nchi yangu jambo kama hilo Mungu akuongezee sana na sana
ReplyDeleteHuyo aliyetoa hoja ya vazi la Flaviana ana lake. Hapo watu hawakuenda kuangalia amevaa nini ina anafanya nini.
ReplyDeleteWell done Flaviana!
ReplyDeleteHongera sana Flaviana na Mungu akubriki ila tu mwanetu kivazi na tukio kidogo halijakaa vizuri hasa ukizingatia utamaduni wetu wa kitanzania.
ReplyDeleteSasa we mdau hapo juu ulitaka binti avaaje?
ReplyDeleteHongera Flaviaa, we ni mfano wa kuigwa
Hongera sana Flavi. Anon wa Mon May 21, 08:32:00, muhimu hapo alichoenda kukifanya Flavi na sio kivazi. Watu kama wewe ndio msiokua na shukran.
ReplyDeleteYaani unayesema vazi halijaendana, sijui utaamka lini kwenye huo usingizi mzito uliopo, kazi unayo..
ReplyDeleteAnonymous wa hapo juu
ReplyDeleteUlitaka avae vipi? tusaidie na sisi tusiojua ili tujue tusiendelee kuwa ovyo Watanzania! unapocritise toa na alternatives
Mungu akubariki dada. Hakika umeonyesha moyo wa Imani..Mdau hapo juu vazi lake halina tija kwenye hili. Umetugusa Watanzania.
ReplyDelete