Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata Amekuja nchini akitokea nchini Marekani ambako ndiko yaliko makazi yake kwa sasa mahsusi kwa ya ajili ya kugawa msaada wa VIFAA VYA KUOKOLEA MAISHA MAJINI (life vest) ikiwa ni miaka 16 tangu meli ya MV BUKOBA izame ambapo mama yake mzazi alifariki kwenye ajali hiyo.anatarajia kugawa msaada wa vifaa hivyo Jumatatu ya 21 May jijini mwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2012

    Mfano wa kuigwa, hongera Dada!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Flaviana, kweli wewe ni mtu wa 'MIADI' (A LADY OF YOUR WORD). Mwenyeez Mungu azidi kukujaaliya moyo huo huo wa kujali, kutowa na kutimiza AHADI zako. Nakumbuka ulilisema na kuliahidi hilo bayana kwenye kile kipindi cha 'Mkasi' kinachoongozwa na Salama Jabir. Hakika umeweza kulitekeleza na kulitimiza suala hilo, hongera sana! Mwenyeez Mungu amlaze pema peponi marehem MAMA yako mzazi, pamoja na wote waliopoteza maisha yao katika ajali ile ya M.V. BUKOBA. Naamini kitendo ulichokifanya kinadhihirisha wazi UPENDO na pia KUMUENZI marehem MAMA yako. Hakika, umeweza kuonyesha na kuzingatia suala zima la 'healthy and safety' khususan katika vyombo hivyo vya baharin. Umeonyesha moyo wa UZALENDO na UPONDO kwa NCHI yako na RAIA wake kwa jumla. Mungu akubariki katika kila jambo ulifanyalo na akujaalie salama, amani na maisha marefu. Ubarikiwe sana Flaviana.

    Na wewe Salama Jabir, uliahidi kuchangia juu ya hilo huku 'ukisherehesha' kwamba, hata weye kwenu bila 'kuvuka' bado hujajifa. Haya basi zingatia...ahadi ni deni.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2012

    Well done sissy!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2012

    Asante dada, Mungu akubariki na moyo wako kwa kufanya jambo la maana kama hili, nasi tuko nawe na nitakuunga mkono kwa kujitolea kwenye foundation yako. Ni mfao mzuri kwetu wote kuiga ili tuokoe maisha yetu wote. Hongera saana dada.

    ReplyDelete
  5. hongera flavian, pole kwa kupotelewa na mama. MUNGU AKUJALI ZAIDI UKUMBUKE NYUMBNANI

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2012

    Asante sana kutoa ni moyo mwenyezi mungu akuzidishie mengine mengi na amlaze mama yetu mpendwa mahali pema peponi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...