Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh Muhammad Reza Rahimi Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh Muhammad Reza Rahimi Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi. Katikati yao ni mkalimani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh Muhammad Reza Rahimi Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012 Mjumbe maalumu kutoka serikali ya Burundi, Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo. Kati ni Balozi wa Burundi nchini Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012 na Mjumbe maalumu kutoka serikali ya Burundi, Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo. Kushoto ni Balozi wa Burundi nchini Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012 kutoka serikali ya Burundi alioletewa na Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma ujumbe alioupokea Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012 toka kwa Mjumbe maalumu kutoka serikali ya Burundi, Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo. shoto ni Balozi wa Burundi nchini Tanzania.PICHA NA IKULU.



SERIKALI ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kufuta riba yote, ya kiasi cha dola za Marekani Milioni 146, ya deni ambalo Iran imekuwa inaidai Tanzania tokea mwaka 1986 kutokana na ununuzi wa mafuta.
Aidha, Serikali hiyo imesema kuwa imekubali pendekezo la Tanzania la kulipa deni la msingi kwa njia za kubadilisha bidhaa na kwa makampuni ya Iran kukaribishwa kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.
Uamuzi huo wa Serikali ya Iran umetangazwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mheshimiwa Mohammad Reza Rahimi wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo, Jumatano, Mei 30, 2012.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, viongozi hao wawili wamezungumzia masuala mbali mbali yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Iran likiwemo deni ambalo Iran imekuwa inaidai Tanzania  tokea mwaka 1986 kutokana na ununuzi wa mafuta.

Kuhusu deni hilo, Mheshimiwa Rahimi amemwambia Rais Kikwete: “Kwa amri ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, napenda kukujulisha na kutangaza kuwa kuanzia leo Iran imefuta riba yote iliyokuwa imezalishwa kutokana na deni hili.”
Ameongeza: “Iran pia inapenda kukujulisha Mheshimiwa Rais kuwa iko tayari kuangalia njia mbali mbali za kulipwa deni la msingi ikiwa ni pamoja na nchi zetu mbili kubadilishana bidhaa na makampuni ya Iran kupewa nafasi ya kuwekeza katika uchumi wa Tanzania katika maeneo mbali mbali na hasa kwenye kilimo na afya ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vya madawa.”
Mheshimiwa Rahimi yuko katika ziara ya siku tatu kutembelea Tanzania kwa mwaliko wa Makamu wa Rais, Mheshimiwa Mohamed Gharib Bilal. Wakati wa ziara yake, kiongozi huyo wa Iran amefanya mazungumzo na viongozi Wakuu wa Tanzania na amefungua ama kuanzisha miradi inayogharimiwa na Iran.
Wakati huo huo, Rais Kikwete leo amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Mjumbe Maalum wa Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi. Mara baada ya kupokea ujumbe huo, Rais Kikwete amefanya mazungumzo na Mjumbe huyo, Mheshimiwa Martin Nivyabandi ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Tarafa (Serikali za Mitaa) wa Burundi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2012

    safi sana tunataka iwe hivi hivi rais wa iran njoo siyo wa vatican

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...