LICHA ya baraza la wazee wa klabu ya Yanga kumtaka mwenyekiti wao Lloyd Nchunga (pichani) ajiuzulu, mwenyekiti huyo amesema ataendelea na majukumu yake kama mwenyekiti halali wa Yanga. Jana, baraza la wazee wa Yanga kupitia kwa katibu wake Ibrahim Akilimali lilitoa siku sita kwa Nchunga na wajumbe wa kamati ya Utendaji Yanga kuachia ngazi kinyume na hapo watashusha mvua ya masika.

 Wazee hao pia walidai kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na uongozi wa Nchunga kushindwa kuongoza na hivyo kuisababishia klabu matatizo mbalimbali, hivyo hata kikao cha wazee alichokiitisha Mei 20 kinashangaza kwa kuwa aliwakana na kusema katiba ya Yanga haina wazee, hivyo wao wameona siku hiyo iwe ni kwa ajili ya mkutano mkuu wa wanachama wote, huku akiwaomba wanachama kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia Nchunga akijiuzulu.

Nchunga amesema  kwamba anashangazwa na shinikizo hilo la kumtaka kujiuzulu wakati anaongoza klabu hiyo kwa mujibu wa katiba ambayo ndiyo ilimuweka madarakani.

 Alisema yeye kama mwenyekiti alikutana na wajumbe wa kamati yake ya utendaji na kujadili matatizo yote wanayodai wanachama hao na ndiyo maana alitoa majibu kupitia kwenye vyombo mbalkimbali vya habari. Baadhi ya masuala aliyoeleza Nchunga ni pamoja tarehe ya kikao baina yake na wazee wa klabu hiyo,

mkutano mkuu wea wanachama, mchakato wa usajili pamoja na kutafuta kocha mpya kutoka nchi mbalimbali duniani. “mimi sifanyi mambo kwa shinikizo, nafuata katiba ya Yanga inasema nini, hivyo tarehe 20 Mei nimepanga kukutana na wazee, na mkutano mkuu wa wanachama ni Julai 15, kama kuna mengine nje na niliyoamua na viongozi wa kamati ya utendaji sina mamlaka nayo,”alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2012

    Nchunga usiyumbishwe na hao Wazee..Stand on your feet mate.

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2012

    Nyie watu wa Yanga mlimchagua wa nini siku ile pale PTA.Ndo matunda ya kuendekeza fedha za muda badala ya kuweka watu wa mpira

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2012

    Nchunga, mimi nilidhani kwamba ukiwa kama mwanasheria ulitebobea utatunza hadhi ya taaluma yako kwa kujiuzulu. Nakushauri kama ilivyosema ripoti ya mheshimiwa Mwakyembe, "angalia uzito wa jambo ukizingatia hadhi na heshima yako, kisha utoe maamuzi ya busara". Niheshima kujiuzulu kuliko kusubiri utolewe kwa nguvu. Jua kwamba kutolewa kwa nguvu inawezekana pia

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2012

    Kama namuona Davis Mosha huko aliko, Nchunga ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2012

    Nchunga, wenye Yanga yao hawakutaki, sasa wewe unachong'ang'ania ni nini??!! Si uondoke tu!!??

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2012

    Mzee Nchunga Yanga ilikuwepo toka babu yako yuko kijijini bado, umeshindwa majukumu hivyo wewe na wenzio wanaokuunga mkono kutokana na njaa zao mpumzike kabla hatujaanza kumwaga el nino.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...