Home
Unlabelled
Mahojiano na Mhe. Zitto Kabwe - Tanzania kuelekea 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Zitto ameongea points za msingi kabisa. Ila wasiotaka watakataa kwa sababu wana maslahi binafsi, hivyo ni lazima watetee mifumo ya zamani tuliyoichoka.
ReplyDeleteKuna watu wanapinga mfumo wa majimbo kwa kisingizio kwamba utatugawa. Mimi binafsi napenda kuungana na Zito kuuunga mfumo wa majimbo kwani utayapa majimbo mamlaka zaidi ya kuamua mambo yake wakitumia rasilimali walizo nazo na hivyo kuleta ushindani badala ya mfumo wa sasa ambapo kila kitu kinaamuliwa Dar.
ReplyDeleteNaungana pia na Zito kupinga kuwepo kwa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuteuliwa na Raisi. Tumewaona wengi hawafanyi kazi kwa manufaa ya wananchi bali kwa manufaa ya raisi. Wananchi tuwaunge mkono CHADEMA katika mambo haya ili katiba iyaweke vizuri kulingana na matakwa yetu.
Hongera Mh Zito kwa kuweka wazi nia yako ya kuutaka uraisi. Hata hivyo ni mapema mno kwani utakumbana na wapinzani wengi. Labda kama umejipima ukaona utakuwa na uwezo wa kupambana nao.
ReplyDeleteUlitakiwa utangaze nia hiyo baada ya 2015. Nina uhakika ukigombea 2015 hutapata kwa sababu bado umri wako ni mdogo na unajua katiba haijabadilishwa ili mtu kama wewe ugombee, pia CHADEMA bado hamjakubalika kwa wananchi wengi hasa kwa wazee na watu wa vijijini. Hili silisemei kwa wewe tu ni kwa yeyote mtakayemuweka 2015 hata kama atakuwa Slaa, Lissu, Mbowe au Halima Mdee.
Tupo pamoja na wewe mheshimiwa kabwe gombea urais mwaka 2015 na tutahakikisha tunakupa nchi hayo uliyoyasema ndio watanzania tunayoyataka
ReplyDeletenaungana na wewe bila pingamizi yoyote tumechoka na utawala mbovu wa maguvu na mafisadi.
mdau mahakama kuu ya dunia
The hague.
Jamani huyu mchangiaji aliyepita anaishi wapi? Kwani Nasari aliposhinda uchaguzi juzi ni mjini? Na hata mheshimiwa Zitto mwenyewe alikoshinda uchaguzi uliopita ni mjini? Sasa kama walishinda si ndiyo kuonyesha dhahiri Chadema imekubalika tena katika mazingira magumu ambapo viongozi wote wa halmashauri n.k ni makada wa Chama Tawala. Hebu fikiria kwanza ndiyo unchangie vitu vya msingi kama wenzako walio na mtazamo chanya. Na kama hujui, tukijua nia yake mapema basi tutapata fursa nzuri zaidi ya mpima.
ReplyDeleteGombea mwaka 2015 .Una point za msingi za kuchaguliwa kuwa Rais.
ReplyDeleteTanzania inahitaji watu kama wewe.
HANA LOLOTE NAYEYE AKIINGIA NI HAYOHAYO TU WOTE MAKELELE SASA KULA TU NDIO NIA YAO. WOTE NI NJAA TU! CCM PIA AHADI ZILIKUWA HIZOHIZO WAKIFIKA HAPO W/HOUSE HAKUNA KITU!!! MIMI KURA NO! NO!
ReplyDeleteMgombea binafsi ameruhusiwa 2015??
ReplyDeleteDavid V
mheshimiwa nashukuru sana kwa maoni yako na kwanza nakupongeza sana kusema muungano ni lazima urindwe kwa ali na mali na kweli mimi ni mwanaccm nakuunga sana kwa ilo jambo la muungano na kupenda tuwe na mawaziri wakuu wa bara na visiwani,hongera nailo jambo nakuunga sana ili maendeleo yawepo pande zote mbili.
ReplyDeletecha pili ni lazima tuuandikekatiba ya inayotufaa sisi na iwe mfano kwa africa,
Mimi si chadema wala ccm. ila marais wanaohitajika kwa nchi hii hapa tulipo ni wanne. wale amabao wanaweza kukemea na kusikilizwa! na nitakayempigia kuara ni awe ametoka kati ya hawa wanne - sio kwa mpangilio wa muhimu.
ReplyDelete1. Edward Lowasa
2. Zito Kabwe
3. Pombe Magufuli na
4. Samweli Sitta