Katibu mtendaji wa baraza la Taifa la mitihani Tanzania (NECTA),Dk. Joyce Ndalichako leo ametangaza matokeo ya Kidato cha Sita kwa shule zote  za Sekondari nchini,Katika Matokeo hayo,Shule iliyofanikiwa kuongoza ni MARIAN GIRLS iliypo mjini Bagamoyo.

Pia amepunguza adhabu ya miaka 3 na  kusema kuwa sasa adhabu itakuwa ni mwaka 1  kwa watahiniwa waliobainika kufanya udangayifu wa matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2011.


Matokeo hayo ni kwa hisani ya Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2012

    Mama Ndalichako..Zile shule za serikali zilizokuwa zinatamba enzi zetu zile wasichana peke yao na wavulana peke yao,'zimevurugika'..nimeona kumbe hata Bwiru boys ina wasichana,Tabora girls imejaa Wavulana!Sipingi mabinti zetu kusoma,ningekuwa mimi zile shule ningeziacha zilivyokuwa nikajenga zingine za mchanganyiko.Sijafanya utafiti lakini nadhani shule za boarding wasichana peke yao na wavulaba peke yao zinafanya vizuri zaidi..

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2012

    mdau hapo juu hizo shule hazijachanganyika kuna centres ambazo private cand.wanafanya mitihani kwenye hizo centres mfano unaweza kuta tabora boys centre na tabora boys sec school au ukakuta msalato centre na msalato sec school

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2012

    Kwa msaada zaidi 'Centres namba zake zimeanza na P' wakati 'shule namba zake zimeanza na S'.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2012

    St Matthews High school kaza soksi kwa masomo ya sayansi tafadhali...tunalipa pesa nyingi kwa ajili ya wanaochukua mwasomo hayo...vijana nao kazania wasilale hayo ni masomo makali

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 02, 2012

    Point yangu niliileta visivyo.Nilikuwa nasemea shule zilizokuwa za wavulana peke yao kuweka wanafunzi wa kike.Mfano mimi nimesoma Sengerema Sekondari school(A-level) tulikuwa wavulana tu Bwenini kuanzia O hadi A level.Sasa hivi wameweka mabinti wanasoma Day scholar hapo O-level..Sengerema ilikuwa inafanya vizuri sana kabla ya Co-education.Sasa hivi imeporomoka,Offcourse, kinaweza kuwa na sababu nyingine.zipo shule nyingi zimekuwa hivi,,nilipouliza nikaambiwa eti wanaweka mabinti kupunguza vurugu na migomo kwenye shule hizo!ndiyo ilikuwa point yangu kuu hapo..siyo suala ya Private wala school candidates

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...