Ankal Michuzi, Hivi karibuni nilikuwa na jamaa zangu kama watatu, Tukiwa tumekaa maeneo flani tukipiga story za hapa na pale, mmoja wetu akaanza kulalamika hali ya uchumi mbaya, na anahangaika kumalizia nyumba yake na kusema gharama alizotumia mpaka sasa ni mamilioni ya fedha na hajafika hata nusu kupata " his Dream House", Mi nikatamka na kusema, kama hali ndio hii basi itabidi niangalie njia nyingine ya kujenga nyumba ya kisasa ambayo nitakaa na familia yangu na kufurahia. Nikasema ntaangalia ikiwezekana nijenge nyumba kwa kutumia Containers. Jamaa walicheka, na kusema eti sasa hapo nimechemsha, ila leo nikaingia ofisini na nika google na kuona nyumba hizi zinavutia sana. Ukipata designer mzuri na engineer wa ukweli sio magumashi.
Nafikiri ndoto zangu zitatimia, Ni kujua tu gharama za container urefu na gharama za shughuli zote. Nimeona nikitumie pia wewe uangalie, nafikiri zinavutia na ntaweza kulala usingize mnono, Hata nikiambiwa nibomoe kama wanataka kupitisha barabara( Bomoa Bomoa ) Naweza kuokoa sehemu kubwa ya mali yangu. Watanzania tusiwe na dharau kwenye ubunifu. Ubunifu hauna mwisho, kila siku kuna idea mya zenye manufaa na zinazoendana na hali ya uchumi wetu. Tusijilazimishe kujenga majumba makubwa matokeo yake tunashindwa kumaliza.Sina mengi, embu angalia mwenyewe, tena nimeweka na moja ya Ramani.



Ubunifu mwingine hovyo. Ndo maana likaitwa container na si nyumba. Kama ndo mawazo ya kwamba bomoa bomoa basi tatizo ni kwako kwa nini ung'ang'ania viwanja ambavyo havijapimwa au kununua kiwanja ambacho si halali?
ReplyDeleteKinachovutia ni hizo urniture humo ndani na sio nyumba acha kujidanganya
ReplyDeleteUshauri wako si mbaya kwakweli ni mzuri sana. Hata mie nimekuwa nikiliwaza hilo. Ni pale tukiacha ubinafsi na tukajiunga katika communities twawezafanya kitu cha maana. Maana wengi hulalamika nyumba kama kwa mfano uloonyesha hapo, ataongelea usalama. Kwakweli mkijiunga watu mkajenga ukuta mkaweka ulinzi wa kueleweka then mkajenga nyumba zenu simple tu tena zenye ubunifu wa hali ya juu, mbona inatosha.
ReplyDeleteWatz tunapenda kuigana tuuuuu na kamwe hatuwazi zaidi ya tulichoona wengine wamefanya na tunaishia hapo.
Nimeipenda post yako. yaliyokukuta nami pia yalinikuta siku za nyuma kidogo nilipoleta hoja hii pale Jamiiforum, Inakatisha tamaa lakini mimi pia ni ndoto yangu natumai kwa research niliyofanya naweza kusimamia mwenyewe nikisaidiwa na mafundi( wataalaamu wa ujenzi) na kutimiza ndoto hiyo nadhani hapo ndio wengi wataweza kufumbua macho na kuona kuwa inawezekana.kila la kheri najua inawezekana.
ReplyDeleteContainer moja tupu bongo milioni ishirini utakuwa umesevu nini?
ReplyDelete