Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Idd Mponda akimkabidhi mwenge wa uhuru kwa katibu tawala wa wilaya ya Songea,Joseph Kapinga mara baada ya kumalizika kwa mbio za mwenge wilayani mbinga.
Mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Songea ambaye pia ni mkuu wa kikosdi cha 842 KJ Mlale,Meja Mpuku akipokea mwenge wa uhuru mpakani mwa wilaya ya mbinga na songea katika kijiji cha Liganga.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Songea (v) mkoani Ruvuma,Geofrey Guta (kulia) akimkabidhi mwenge wa uhuru kwa mkurugenzi wa manispaa ya Songea,Zakaria Nachoha mara baada ya mwenge wa uhuru kumaliza mbio zake katika halmashauri hiyo.
Mtawa wa shirika la St Benedictine Peramiho,Hyasinta Shayo akishika mwenge wa uhuru katika kijiji cha Peramiho A Wilayani Songea vijijini.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu Kapt Honest Mwanosa akiweka jiwe la msingi katika jengo la zahanati katika kijiji cha Namatuhi songea Vjijijini jana.ambacho hadi sasa kimegharimi kiasi cha zaidi ya shilingi 200 milioni.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kapt Honest Mwanossa akicheza ngoma ya muhambo ambayo ni maarufu kwa wenyeji wa wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma,mara baada ya mwenge kuwasili katika kijiji cha Kigonsera wilayani humo.
Mama huyu ambaye hakufahamika jina lake mara moja akiwa na furaha na wakimbiza mwenge katika kiijiji cha Namatuhi katika halmashauri ya wilaya ya Songea(v) jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2012

    Duh!kweli pesa ya ccm haina kazi.
    Mwenge unatakiwa kuwamulika wazembe ,wanyonyaji,mafisadi,nk nk.
    Ikiwa mambo yote haya bado yapo na yanaendelea huu mwenge una maana gani???ni uharibu wa pesa za walipa kodi.
    Mwenge uwe kwa miaka kumi kumi ili kutumia hiyo pesa kwenye mambo mengine ya maana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...