NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mh Ummy Mwalimu (pichani)  amejitolea kumsaidia mtoto ambaye mzazi wake alishindwa kumpeleka shule baada ya kufaulu kwa kile kukosa ada ya shule.


Akizungumza na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi, ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema ameguswa na habari hiyo iliyotolewa na mtandao huu juzi, hivyo yupo tayari kumsaidia mtoto huyo nawengine watakao kuwa na matatizo kama hayo eneo hilo.



Hata hivyo, Naibu Waziri Mwalimu, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kutokea Mkoa wa Tanga amesema anaamini mama wa mtoto huyo alikuwa muoga kuwasiliana na viongozi wa wilaya hiyo ya Handeni kwani wangelimsaidia na mtoto huyo kujiunga na shule.



"Kwanza napenda kuwapongeza kwa kuibua changamoto kama hizi, kimsingi nimeguswa na habari hiyo ya mtoto kushindwa kujiunga na shule kwasababu mzazi wake hana uwezo...naomba mnipe mawasiliano ili tuangalie namna ya kumsaidia," alisema Naibu Waziri huyo.



Alisema ipo haja ya halmashauri kufuata ushauri wa Serikali kwa kile kutenga asilimia 5 ya mapato yao kuwawezesha wanawake kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake, kwani endapo akinamama watawezesha wanaweza kufanya mabadiliko hata katika changamoto kama hizo.



"Unajua ukimuwezesha mwanamke unakuwa umeiwezesha jamii...endapo kila wilaya ikikubali kutenga asilimia 10 ya mapato yake, kwa ajili ya mfuko wa  maendeleo ya wanawake na ule wa vijana kwa kugawa asilimia tano tano kila upande tutasaidia mambo mengi, zikiwemo changamoto za maisha katika familia," alisema Mwalimu.



Juzi mtandao wa Thehabari.com pamoja na mitandao mingine washirika wa Thehabari.com walichapisha habari ya mmoja wa wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na masomo mwaka huu kushindwa kuendelea na shule baada ya mzazi wake mmoja (mama) kushindwa kumgharamia.



Mtandao wa Thehabari.com unafanya mawasiliano na mzazi wa mtoto huyo na kuangalia namna ya kuwakutanisha na baadhi ya wasamaria waliojitolea kubeba mzigo wa masomo kwa kijana huyo. Mtandao huu utaendelea kuwajulisha taarifa zaidi za tukio hili hadi pale mtoto atakapo jiunga na shule.


Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa 
 Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi akifanya mahojiano na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Watoto Mh Ummy Mwalimu ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Watoto, Mh Ummy Mwalimu (kulia) akimadilishana kadi za mawasiliano na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com, Joachim Mushi mara baada ya mahojiano ofisini kwake  jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2012

    Safi sana thehari.com kwa kazi hii kubwa. Wanamitandao mlioshirikiana na thehabari.com nawapongeza pia. Aluta kontinua!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2012

    Mtoto kukosa ada ya masomo,

    Matatizo kama haya na mchakato mzima wa Kuwafikia Viongozi ili kutatua shida unakuwa mgumu kwa vile PAMEJENGEKA KUTA MIONGONI MWA JAMII YETU KATI YA VIONGOZI NA WANANCHI,,,HUYO MAMA YAKE MTOTO HAKUWA MWOGA KUWAFIKIA VIONGOZI NA KUTOA SHIDA YAKE,BALI VIONGOZI HAWAFIKIKI KIRAHISI KUTOKANA NA HIZO KUTA ZILIZOPO MIONGONI MWETU!.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2012

    mungu akuzidishie moyo wa upendo sio kwamba unazo ni umejitolea na wengine uwe mfano kwenu jamani hali ni mbaya sana sema watu hawajui wanzie wapi. Huyo mtoto huwezi jua maisha yakiwa mazuri hawezi kukusahau kwa wema wako.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2012

    Safi sana! God bless you Mh Ummy.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2012

    Good gesture, but this is just a tip of the iceberg,there are many more children in similar situation, I do a lot of charity work back home,more people should do the same.
    Dr Gangwe Bitozi, Mamtoni.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 18, 2012

    Napenda wewe naibu waziri, Mungu akuongezee na usipungukiwe na chochote.

    ReplyDelete
  7. Mwenyeez Mungu akujaaliye na kukuzidishia kila lenye kheri na wewe na azidi kukujaaliya moyo huo wa huruma, Mana jambo la kutowa siku zote lataka moyo na katu sio utajiri, hongera sana Mh. Ummy kwa moyo wako huo wa huruma na upendo, Malipo yako utayakuta huko usoni twendako. M/Mungu akubarik.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2012

    Lakini hiyo ndio kazi yako Dada Ummy,wala sio kujitolea,ulitakiwa uwe mstari wa mbele kuhakikisha yatima na wasio na uwezo wanaenda shule,na ndio mana wizara yako ikaitwa maendeleo ya jamii nawatoto na sio kukaa kwenye viti tuu siku nzima,msisubiri kuletewa habari nyingine mzitafute.
    Nyinyi viongozi mpo mbali sana na jamii,hamko friendly

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...