Mkuu wa idara ya masoko na Mawasiliano wa NMB,Imani Kajula (wa pili kulia) akimkabithi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mlimani wakati wa uzinduzi wa NMB Financial Fitness.
viongozi wa NMB na Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mlimani wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika darasa la saba.
Wanafunzi wa Mlimani wakisoma jarida la NMB financial fitness.
BENKI ya NMB ilizindua mkakati wa kukuza uelewa wa masuala ya kifedha kwa wanafunzi wa shule za msingi unaoitwa NMB Financial Fitness. Uzinduzi wa mpango huu ulifanyika shule ya Sekondari ya Pugu.
Mpango wa NMB Financial Fitness unalengo la kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha, huduma za kifedha, uwekaji akiba, kujenga uwezo wa kupanga matumizi na mengine mengi.
Miaka michache iliyopita Utafiti uliofanywa na Financial Sector Deepening Trust yaani FSDT unaonyesha kwamba ni 12% ya watanzania ndio wenye akaunti za benki, moja kati ya sababu kubwa zinazoelezwa kuwa chanzo cha uwiano huu ni uelewo mdogo wa masuala ya kifedha.
Wachumi wanaamini kuwa maendeleo yoyote ya nchi yanachangiwa na uwekaji akiba wa wananchi wake.
Mpango wa NMB Financial Fitness utafanyika nchi nzima na jumla ya vijarida 50,000 vitagawiwa kwa wanafunzi, hususani wa darasa la saba. Baada ya uzinduzi wa kitaifa, wiki hii kulifanyika uzinduzi wa kanda ya Dar es salaam katika Shule ya msingi Mlimani.
Akizungumza wakati wa kuzindua mpango wa NMB Financial Fitness kwenye shule ya msingi Mlimani, Mkuu wa Idara ya Masoko ma Mawasiliano Imani Kajula alisema ‘’ NMB inataka vijana sio tu wawe fiti kimwili bali pia fiti kwa uelewo wa masuala ya fedha, NMB inatambua kwamba maamuzi sahihi na matumizi sahihi ya fedha sit u yanaleta maendeleo kwa mtu binafsi bali pia kwa taifa kwa ujumla.
NMB kupitia mkakati huu inagemea familia za wanafunzi pia zitafaidika na kijarida cha NMB financial fitness’’


.png)
.png)
.png)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...