Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Handeni na Ofisa Elimu wa Sayansi Kimu wilaya ya Handeni, Ester Ngao akizungumza na mwandishi wetu (hayupo pichani).
Mratibu wa Elimu Kata ya Chanika, Ramadhan Majogo.

Na Joachim Mushi wa TheHabari.com

HALMASHAURI ya Wilaya ya handeni imesema ipo tayari kuanza kuwasaidia kielimu wanafunzi waliopata mimba na kukatisha masomo, endapo Serikali itapitisha rasmi sera ya kuridhia kundi hilo la wanafunzi kuendelea na masomo katika mfumo wa elimu ya kawaida.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Ramadhan Diliwa alipokuwa akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu kufafanua mfuko wa elimu wilaya hiyo unavyotumiwa kuzisaidia familia zinazoshindwa kulipia gharama za elimu.

Mwenyekiti Diliwa alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuelezwa kuwa wapo baadhi ya wasichana ambao walirubuniwa wakiwa shuleni na kutiwa mimba kabla ya kukatishwa masomo, na sasa baadhi wapo tayari kurejea shuleni.

Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na mwandishi wa habari hizi kwa kushirikiana na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), umebaini uwepo wa idadi kubwa ya wasichana wanaokatishwa masomo kwa mimba jambo ambalo linaharibu maendeleo ya elimu eneo hilo.

Akifafanua zaidi Diliwa alisema halmashauri hiyo ipo tayari kuwasaidia wanafunzi hayo kupitia mfuko wa elimu wa wilaya hiyo, lakini kikwazo ni sera za Serikali bado hazijaridhia kitu kama hicho.

"Tunaweza kuwasaidia kundi hilo (wanafunzi waliopata mimba), lakini yapo masuala mengi ya kuangalia, je itawezekana kwa utaratibu gani na sera zinaruhusu kufanya hivyo...maana nilikuwa nasikia watu wakiizungumzia kuwa kundi hilo liendelee na masomo baadaye lakini sera bado hazijaridhia," alisema Diliwa.

Aidha aliongeza kuwa kwa sasa mfumo huo umewalipia gharama za masomo wanafunzi takribani 240 katika hatua balimbali za masomo, hivyo kuwahimiza familia ambazo zinakwama kabisa kuwalipia watoto wao ada wasiogope kuja ofisini ili watambuliwe kabla ya kuanza kusaidiwa.

Pamoja na halo ameitaka jamii kuacha kutoa visingizio vya wanafunzi kutiwa mimba kwa kile kutokuwepo kwa mabweni katika shule nyingi za kata, kwani hata zamani kulikuwa na shule za bweni lakini wapo baadhi ya wanafunzi walitiwa mimba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...