Na Mary Ayo

DIWANI wa kata ya Masieda Joseph Darabe ameiomba serikali kutekeleza mradi wa maji uliofadhiliwa na benki ya dunia uliopo masieda wilayani mbulu ili uweze kuingizia halimashuri hiyo mapato sanjari na kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo

Aliyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii kuhusiana na mradi huo ambao ulishafanyiwa utafiti kwa kipindi nyuma

Alieleza kuwa kata hiyo ni miongoni mwa vijiji kumi ambavyo vilibahatikana mradi wa maji ambao unafadhiliwa na benki ya duniahivyo ni vema serikali ikaharakisha mradi huo ili halimashauri hiyo iweze kuingiza mapato kutokana na mradi huo

Aidha bw Darabe alisema kuwa wafadhili wa bank hiyo tayari walishatembelea eneo hilo ambapo utafiti ulionyesha kupatikana kwa lita laki moja kwa siku ambapo amesema kuwa endapo serikali itatoa kipaumbele kuharakisha mradi huo ni wazi kuwa halimashauri hiyo nayo itanufaika na mapato

“ninaiomba serikali ianze mapema kutekeleza mradi huu wamaji ambao umefadhiliwa na benki ya dunia na hata katika mto udahaya ambapo dhahabu inapatikana mabomba yakiwekwa ni wazi kuwa hata serikali nayo itanufaika na mapato hayo”alisema

Kwa upande mwingine bw darabe alisema kuwa halimashuir ya kijiji hicho kwa kupitia mkutano mkuu wameweza kupokea mrad iwa shilingi laki saba kwa mwezi kutoka kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu ya ya miamba ambapo dhahabu hizo zimeanza kupatikana mara baada ya wachimbji hao kufanya utafiti wa kina katika mto udahaya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...