balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. James Msekela akitoa hotuba yake wakati wa Sherehe ya Muungano wa Tanzania nchini Italy.

Ile sherehe ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa ikisubiriwa na wengi mjini Roma, ilifanyika jumamosi tarehe 12 Mei 2012.Sherehe ilifanyika kwenye ukumbi wa Karispera club 69, uliopo katikati ya mji mkuu Roma na kuudhuliwa na Watanzania wengi kutoka sehemu mbalimbali za Italia. 

Mgeni rasmi alikuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. James Msekela, ambaye kwa mara ya kwanza alikutana na Watanzania kwa pamoja kutoka kila kona ya Italia. 

Kwenye sherehe hii, balozi Msekela aliishukuru Jumuiya ya Watanzania Roma kwa kuandaa sherehe hii muhimu kwa Taifa la Tanzania kutokana na dhumuni lake la kusherekea muungano ambao ni moja ya ngao ambazo tuliachiwa kama urithi na baba wataifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume. 

Balozi Msekela pia aliwaelezea Watanzania kuwa amefurahishwa sana na umoja ambao ameuona kwenye siku chache toka kufika kwake nchini Italia na kuwaomba Watanzania waendelee na moyo huu wa ushirikiano maana ndio kitambulisho cha Tanzania nje ya nchi. 

Balozi alihaidi kushirikiana na hizi jumuiya za Kitanzania hapa Italy na kuwaomba wasisite kwenda kumuona pale watakapo kuwa wanaitaji ushauri na msaada wa aina yeyote toka ofisini kwake.

Kwa picha zaidi tembeleeni blog ya Jumuiya ya Watanzania Roma hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.

Mungu Ibariki Tanzania
Wadau Mbali mbali waliohudhulia Sherehe hizo wakiwa ni wenye furaha ya kutosha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2012

    Mjomba Chibiriti sijamwona jamani bado yuko Cecena?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2012

    Naona meza zetu zinafananiamo na za wa Roma.....

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2012

    Duhhh Mtikisiko wa 'Kifedha na Kiuchumi' umeipiga vikali Ulaya!

    Sio Ugiriki pekee kumbe?

    Naona meza nyeupeeeeee, wamejitahidi wamefurukuta pana (chupa Moja kubwa ya ...maji ha 'uhai' ....hahahahaha....na chupa kubwa tupu moja ya Soda), meza hazina vinywaji sio kama Wandugu kule Marekani na Canada ambako aslalaleee kila siku pati, meza zinajaa masanga na mapochopocho kibao!, watu wanakula na kunywa hadi kuchweee !!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2012

    Ulaya nzima ina njaa, lakini wale jamaa Watanzania hasa wale wa Ugiriki na Katibu wao wa Jumuiya ni wabishi sana kukubaliana na ukweli kuhusu zahama ya njaa!

    Angalia wanajitetea kwa picha , eti ohhh tunajirusha ,ohhh hatuna matatizo, ohhh hayo magazeti tu,

    Vipi mbona meza zipo tupu ktk Hafla zenu?
    Njaa ina siri?,
    Penye neema pana jificha?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 16, 2012

    NJAA HAINA UBAUNSA!

    Haya ni maneno yameandikwa ktk Chota matope la matairi ya nyuma la basi moja aina ya Toyota-DCM linalofanya huduma za abiria kati ya MBAGALA RANGI 3 hadi MWENGE.

    Ni maneno yenye maana kama yakizingatiwa.

    Mtu mzima ameumbiwa hekima na suala linajidhihirisha kwa macho, kwa meza ktk Pati yenu huko Roma zinavyoonekana zikiwa tupuuu, pana dalili hapo!

    Inaeleweka kuwa Mtikisiko wa Kifedha na Kiuchumi unaendelea kuunguruma Dunia nzima.

    Wandugu majuu inaonekana kabisa kengele imelia na njaa ni kali huko Majuu na hasa Ulaya kama vipi tuwatumie vigunia vya mihogo mibichi, mahindi na maharage ili mpoze makali ya njaa,,,ni kama maneno ya basi hapo juu yanasema 'NJAA HAINA UBAUNSA'!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...