Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na ujumbe wa Tanzania wakilisha samaki katika Bustani Maalum iliyopo katika Malazi ya Viongozi katika Mji wa Kyoto wakati walipofanya ziara ya kutembelea Mji huo leo asubuhi. Mhe. Spika na Ujumbe wa wabunge watano wapo Nchini Japan kwa mwaliko maalum wa Kibunge ikiwa ni sehemu ya kukuza demokrasia ya Nchi hizi Mbili.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitizama vivutio vilivyopo katika mojawapo ya Madhehebu ya Kijapan (Temple ) wakati walipofanya ziara ya kutembelea Mji huo leo asubuhi. Mhe. Spika na Ujumbe wa wabunge watano wapo Nchini Japan kwa mwaliko maalum wa Kibunge ikiwa ni sehemu ya kukuza demokrasia ya Nchi hizi Mbili. Kushoto kwake ni Mhe. Anne Kilango Malecela
Mhe. Spika akipata maelezo kuhusu utalii na vivutio vilivyopo katika madhehebu hayo wakati wa ziara ya maeneo mbalimbali katika mji wa Kyoto
Mkuu wa dhehebu mojawapo la watu wenye asili ya Japan (Kushoto) (Master of Tenryu – ji Temple) akionesha namna ya kuabudu kwa hisia kwa waumuni wa madhehebu hayo wakati Mhe. Spika na Ujumbe wake walipo tembelea dhehebu hilo kujifunza tamaduni za watu wa Japan. Kutoka kulia ni Mhe. Tundu Lissu, Mhe. Godfrey zambi, Mhe. Anne kilango, Mhe. Anne Makinda (Spika) na Mhe. James Lembeli
Mhe. Spika na Ujumbe wake wakipata maelezo kuhusu dhehebu hilo la Tenryu – ji Temple na jinsi wanavyo abudu
Mkuu wa dhehebu mojawapo la watu wenye asili ya Japan (kulia) (Master of Tenryu – ji Temple ) akionesha vivutio mbalimbali na nakshi zilizomo katika dhehebu hilo wakati ujumbe wa Tanzania ulipofanya ziara kutembelea vivutio mbalimbali katika Mji wa Kyoto. Spika na Ujumbe wa wabunge watano wapo Nchini Japan kwa mwaliko maalum wa Kibunge ikiwa ni sehemu ya kukuza demokrasia ya Nchi hizi Mbili. Picha na Owen Mwandumbya
Tatizo viongozi wetu kwa watu mnaenda sana na mnaona vitu vingi vizuri ila hamna wivu wa maendeleo kuwa mkirudi nyumbani nanyi mjaribu...sijui ni lana sijui ni nini?hapo mnaona mambo mengi mazuri lakini maskini wa Mungu nyie mkishapanda ndege basi mnarudia joho lenu la uvivu wa kufikiri na kuishi kwa mazoea. sijui tutambike kwa kitimoto ndio laana hii itaishaaa?
ReplyDeleteTembea Uone
ReplyDeleteDavid V
Ndio mmeshasilimishwa hivyo kama hamjui. Sasa hivi kungfu imeingia ndani ya damu, ni nyinyi tu sasa kuitumia.
ReplyDeleteTatizo hamkopi mazuri ya huko ili mpendezeshe nchi yetu pia mnafurahia kusafiri tuuuu. Mama Makinda suruali zinakutoa bomba kwelii
ReplyDeletekila siku nchi bado ni changa sijui itakuwa lini? Maana wenzetu wamekuwa wakuubwa siku nyingi na wengine tulizaliwa miaka sawa na wamekuwa kasoro bongo tu, bado ni changa na maufisadi yote hayo. Hata kama mnakwiba kuweni kama hapo kwa watani wajadi angalao waonyesha matumaini ya maendeleo na sio kina siye umimi umeota sugu!
ReplyDeleteMtoa maoni wa kwanza unataka kutuchekesha...viongozi wetu wivu wa maendeleo wanao sana....maendeleo wanayafanya majumbani mwao.....Hakuna binadamu aliyekamilika asiwe na wivu wa maendeleo
ReplyDeleteMIMI NAWASHANGAA SANA VIONGOZI WETU!! YAANI KAMA NI KUSAFIRI WANASAFIRI SANA!! KWANINI HAWAJIFUNZI HAYO WANAYOYAONA HUKO WAYALETE NYUMBANI? HIVI HAWAONI, TATIZO SAFARI ZAO NI KULIPANA POSHO ZAIDI
ReplyDeleteAsante Michuzi ni jambo jema je Viongozi wetu wanajifunza nini kuhusu Utamaduni? Tumieni fikra kujenga utamaduni lazima sehemu kama machimbo ya Amboni yaboreroshwe Imaya ya Mkwawa, Irangi kondoa lakini kwa sasa sehemu kama Makumbusho ya Taifa imegeuzwa Bar wakati sehemu ile ilitakiwa uonyeshwe Utamaduni wetu. Badala ya kutukuza tamaduni za Cheza kama Rihana vaa kama Jay -Z AIBU.
ReplyDeletemazingira mazuri huko nje, tena karibu na mjini. Hapa nenda bonde la msimbazi ambapo ndipo palitakiwa kuwa sehemu ya ku-breeze, utakachokikuta msimulie na rafiki yako!! Kwa bahati mbaya kuna makampuni yameweka matangazo katikati ya mikoko, ambayo ndio kamsitu pekee katika jiji la Dar!! Mnaweza kuwashauri waamishe matangazo ili msitu ujifunge vizuri??
ReplyDeletemama makinda alisema ubunge ni umasikini na hatogombea tena hivi kweli ubunge ni umasikini? au changa la macho?
ReplyDelete