Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Narita Mjini Tokyo kwa ziara ya siku 6 ya Mwaliko wa Kikazi kutoka Bunge la japani. Kulia kwake ni balozi wa Tanzania Nchini Tanzania Mhe. Salome Sijaona. Mhe. Spika katika ziara hiyo ameongozana na Ujumbe wa Wabunge 5 kutoka Bunge la Tanzania.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika mazungumzo maalumu na Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya tsunami yaliotokea machi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana katika mji huo. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika mazungumzo maalumu na Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya tsunami yaliotokea machi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana katika mji huo. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani.
Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta akimuonesha katika ramani Mhe. makinda sehemu kubwa ya Maeneo yalioathirika na mafuriko hayo katika Mji wa natori.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi zawadi Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kufanya nae mazungumzo baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya tsunami yaliotokea machi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana katika mji huo.
Mhe. Spika akiangalia baadhi ya Mabaki ya wahanga wa Mfuriko hayo katika Shule ya awali ya YORIAGE ambapo picha na nguo za wanafunzi waliofariki zimehifadhiwa.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya wahanga wa Mafuriko ya Tsunami yaliyoikumba nchi ya Japan Mwezi Machi mwaka jana alipotembelea Mji wa NATORI, Uliopo mkoa wa MIAGA ikiwa ni mojawapo ya miji iliyokumbwa na mafuriko yaliyoikumba Japani Mwaka jana. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Spika wa Tanzania Mhe. Anne Makinda wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (Kulia) mara baada ya kuweka shada la Maua katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya wahanga wa Mafuriko ya Tsunami yaliyoikumba nchi ya Japan Mwezi Machi mwaka jana alipotembelea Mji wa NATORI, Uliopo mkoa wa MIAGA ikiwa ni mojawapo ya miji iliyokumbwa na mafuriko yaliyoikumba Japani Mwaka jana. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani. Kushoto ni Mhe. Tundu Lissu, Mhe. Anne Makinda, Mhe. Rukia Ahmed, Mhe. James Lembeli, Mhe Anne Kilango Malecela, Naibu meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta na Mhe. Godfrey Zambi.Picha Zote na owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2012

    Ubunge ni Umaskini

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2012

    Hivi kweli kwenye shughuli rasmi kama hiyo Mhe Tundu Lissu amejivali shati pekee na baadae kuongezea kikofia? Kazi ipo kwa Jamhuri!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2012

    Mama Makinda naona siku hizi umeamua mwendo wa suruali tu ila zinakupendeza uvaage hizo hizo vtenge hupendez sana

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 15, 2012

    Mama uza, si unajua ulisema haugombei tena 2015...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 15, 2012

    Mhe. Spika Anne Makinda:

    Hakuna kitu nisichokiunga Mkono ktk hii Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ktk 'Pilitical integration'

    Ni wazi kabisa kuwa tutaungana kwa mengi lakini ktk hili la Siasa kila nchi ya EAC ina aina yake ya Siasa, hivyo ni 'muhali' au ni vigumu kushirikiana Kisiasa!

    Kuwa ktk Jumuia sio kuwa kila kitu ni lazima tukubali, la hasha tutakubali kwa misingi ya tija!,,,kisichotufaa kimaslahi kamwe hatutakubali!,,,maana ya kuwa ktk Umoja sio kulazimishana na kuburuzana.

    Namuunga mkono Mhe. Makinda wiki iliyopita kwa msimamo wake aliomweleza Spika wa Rwanda na nchi zingine za EAC kuwa Ushirikiano wa Kisiasa sio suala la kuliharakisha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...