Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri. Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.
Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:
“Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge”
Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.
Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.
Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria. Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.
Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.
Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
06 Mei, 2012
_______________________
Kaazi kweli kweli, malalamiko yote hayo yametokana na kutokusoma na kuielewa katiba inasema nini.
ReplyDeleteHivi mimi huwa nashangaa watu wengine wanavyojifanyaga wanajua kila kitu, yaani huyo Rais na wasaidizi wote hao including Makamu wa rais, Mwanasheria Mkuu hawajui kitu isipokuwa mtu mmoja tu? Nendeni shuleee eeh! Na mkienda shulee someni acheni kudesa na kukariri itawasaidia kwenye thinking zenu
Jaji Werema ni mbunge wa wapi? Mbona ameandika "Mb"? Tafadhali atufafanulie na hili kikatiba.
ReplyDeleteBravo, watoa dukuduku
ReplyDeletebila ya malalamiko elimu ya uma ingetolewa lini?.
Mnyagatwa USA
Na JE, SUALA LA MNZANZIBARI KUWA WAZIRI KWENYE WIZARA ISYO YA MUUNGANO HILO SIO LA LIKATIBA NA WALA HALIJAVUNGA SHERIA NA HATI ZA MUUNGANO?
ReplyDeleteMimi naanza kufurahishwa sana na serikali yetu ya sasa maanaimeanza kuota masikio. Enzi hizoooo hata mpige kelele mgalegale chini, ufafanuzi kama huu hautolewi ili watanzania wote wakaelewa na kujifunza mwenendo mzima wa jambo linaloendelea. Sasa malalamiko yakitokea tu serikali inajibu na kutoa ufafanuzi ili kudumisha mahusiano mazuri kati ya serikali na wananchi wake. Juzi moto umewaka Bungeni, serikali imeonyesha mrejeo nyuma, Jana tu upinzani umeibua suala la ukiukwaji wa katiba ya nchi katika uteuzi alioufanya Rais, na leo tena sio siku ya kazi mrejeo nyuma umesikika. Tunashukuru upinzani kwa kupandikiza vijisikio kwenye kichwa cha serikali sasa inaanza kusikia.
ReplyDeleteWe mdau wa kwanza sheria haina bingwa wake hata kama ulienda shule ya sheria ukawa bingwa inawezekana ukakosea kuitafsiri sheria ndo maana hata mahakamani mhukumiwa ana haki ya kukata rufaa na rufaa ikasikilizwa na akashinda japo mwanzo alishindwa. Binafsi nlisikia pia ningependa kupata ufafanuzi wa uteuzi mwingine wa Rais. Hizi wanaziita siku hizi changamoto za Muungano. Ni kuhusu uteuzi wa Dr. Mwinyi kua waziri wa Afya
ReplyDeleteKatiba haimzui Rais wa Jamhuri ya Muungano kumteua mwananchi wa Jamhuri ya Muungano kutoka sehemu yoyote ile ya Jamhuri ya Muungano kuwa waziri wa wizara yoyote ya serikali ya Jamhuri ya Muungano.Labda kama mnataka kuwe na makatazo na vizuizi aina hiyo basi mpelekeeni jaji Warioba sasa na Tume yake kama kero yenu ya muungano ili hilo liingizwe kwenye katiba mpya.
ReplyDeleteMjadala huu mzuri, nimeupenda; tusiishie hapa kama liko linalotukera kikatiba, tukashtaki kwa Warioba sasa!
Anoni wa pili. Mwanansheria Mkuu kwa nafasi yake ni Mbunge ndani ya Bunge la Jamhuri. Na anashiriki katika vikao. Vilevile anashiriki kikao cha Baraza la Mawaziri kwa nafasi yake. Soma katiba yako.
ReplyDeleteHii ni Live bila chenga:
ReplyDeleteJaji Werema maefafanua vizuri sana, tatizo ni kuwa wengi huwa wanakurupuka tu kutoa malalamiko na kuwa na sintofahamu nyingi tu.
Nasikia pana Mwana mama mmoja Mbunge wa Kuteuliwa Viti Maalum alipoona Mhe. Raisi amewapa Uteuzi wa Ubunge wengine watatu (3) na halafu akawapa Unaibu Waziri wanamama hao (2) na Mwanaume Uwaziri Kamili, huyo Mwanamama aliyekuwa Viti Maalum ikamkera!
Angalieni watu hawa wenye tamaa ya Madaraka ni watu hatari sana ktk jamii yetu, alitaka labda Unaibu Waziri apewe yeye Viti Maalum!
Hivi jamani unapokuwa Mwanasiasa (tena Mbunge wa upendeleo wa Viti Maalum) ni lazima wakati wote watu wakufikirie kukupa Madaraka zaidi kama Uwaziri?
Jamani, Mzanzibari yeyeote ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwahiyo kama sifa anazo anaruhusiwa kuwa Waziri kwenye serikali ya Muungano, lakini kwa upande mwingine Mtanzania Bara haruhusiwi kuwa waziri katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Dr. Mwinyi anaruhusiwa kabisa kuwa waziri katika wizara ya Afya. Tanzania Bara hatuna serikali kama ilivyo kwa Zanzibar. Mheshimiwa Rais hajakosea kabisa kumteua Mzanzibari kwenye serikali ya muungano. Tatizo Wabara wengi wanachanganya Serikali ya Muungano na Tanzania Bara (isiyo na serikali).
ReplyDeleteMimi nafikiri Katiba imekiukwa. Hata Tume ya Uchaguzi inapomtangaza mshindi wa kiti cha Rais, mshindi huwa ni Rais mteule hadi atakapoapishwa na kula kiapo cha Urais. hali kadhalika mbunge anapotangazwa anakuwa mbunge mteule hadi atakapokula kiapo cha ubunge.....hii iko wazi, vinginevyo, mwanasheria mkuu anataka kutuambia kuwa hivi viapo havina maana na umuhimu kihivyo....
ReplyDeleteMr.Michuzi,
ReplyDeleteTunaomba kwenye hizi pages za taarifa zako, toa option ambayo itamruhusu mtu kama ameipenda au ameiona ni ya muhimu anaweza ku"LIKE" au aweze kui-post/ ku-share kwenye Facebook maana yawezekana sio wote wameiona, lakini akahitaji kuwafikishia jamaa zake hasa mambo muhimu kama haya yenye Elimu ya Uraia ndani yeke.
Regards,
Raisi amekiuka katiba. Jaji Werema anapiga siasa badala ya kusimamia katiba. Naomba tuonyeshwe mahala popote huko nyuma ambapo Raisi (yeyote, Nyerere, Mwinyi na Mkapa) aliwahi kuteua mawaziri ambao hawajaapishwa kuwa wabunge bado? Naomba tuletewe mifano na sio kukanusha tu.
ReplyDeleteHalafu Wizara ya Afya vilevile Raisi amevunja katiba. Hii sio wizara ya Muungano. Mbona Jaji werema anachagua lipi la kujibu? Hii imelalamikiwa mbona hajasema kuwa ni sawa kwa Raisi kumchagua mtu toka upande wa pili wa Muungano kwenye wizara isiyo na Mambo ya Muungano? Tunaomba utolee ufafanuzi la hilo Jaji Werema.
Nawasilisha.
Mdau#1
HIVI MBARA ANAWEZA KUWA WAZIRI KATIKA SERIKARI YA MAPINDUZI ZANZIBAR ?
ReplyDeleteKatiba yetu bado ina mapungufu sana. Ningeshauri katika mchakato wa kuandika katiba mpya, "madaraka ya Rais" yapunguze, ili asiwe anafanya maamuzi bila kukiuka sheria (katiba) ya nchi. Maana ukisema tu, hakuna umuhimu wa mbunge kula kiapo, basi mi sioni umuhimu wa wabunge kuapa pale bungeni..
ReplyDelete